Habari katika picha: Kilichojiri Arusha Jan 5, 2011

Habari katika picha: Kilichojiri Arusha Jan 5, 2011

Mji wa Arusha jana uligeuka uwanja wa vita kufuatia polisi kutumia risasi za moto na mabomu ya machozi dhidi ya wafuasi wa Chadema ambao waliandamana kwa amani huku kukiwa na amri ya mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema kuyazuia.

-MwanachamaMwanadamizi, Bi Josephine Mshumbusi akivuja damu baada ya kupata kipigo kutoka kwa polisi katika eneo la Tanki la maji mkabala na ofisi za Takukuru jijini Arusha.

-Picha za viongozi wa Chadema wakiongoza maandamano Arusha. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Chadema, Dk Slaa, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godless Lema.

-Askari wa kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Arusha akimkamata mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema kisha kumpeleka katika kituo cha polisi cha kati mkoani humo jana.
 
Attachments

  • DSC06896.jpg
    DSC06896.jpg
    38.9 KB · Views: 678
  • DSC06897.JPG
    DSC06897.JPG
    43.6 KB · Views: 368
  • DSC06906.JPG
    DSC06906.JPG
    52.9 KB · Views: 380
  • DSC06895.JPG
    DSC06895.JPG
    38.7 KB · Views: 360

Hivi polisi wakati wakifanya haya kuna watu wowote wa huduma ya kwanza au ndio kazi yao kupiga tu na utajua wapi kwa kutibiwa? Kweli Tanzania naipenda sana ila Viongozi wetu wanafanya nichukie hata kwetu.
 
Poleni viongozi wetu, huu moto umewashwa tunaomba usizimike mpaka katiba mpya ipatikane.
Hatutaki tume itakayoundwa na Mkwere kucollect maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya, tunataka tume huru itakayoshirikisha asasi mbalimbali za kiraia, pamoja na vyama vya siasa.
 
Mji wa Arusha jana uligeuka uwanja wa vita kufuatia polisi kutumia risasi za moto na mabomu ya machozi dhidi ya wafuasi wa Chadema ambao waliandamana kwa amani huku kukiwa na amri ya mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema kuyazuia.

-MwanachamaMwanadamizi, Bi Josephine Mshumbusi akivuja damu baada ya kupata kipigo kutoka kwa polisi katika eneo la Tanki la maji mkabala na ofisi za Takukuru jijini Arusha.

-Picha za viongozi wa Chadema wakiongoza maandamano Arusha. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Chadema, Dk Slaa, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godless Lema.

-Askari wa kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Arusha akimkamata mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema kisha kumpeleka katika kituo cha polisi cha kati mkoani humo jana.
 
Huyo mwanamama anaevuja damu usoni mbona anafanana na yule mama aliekuwa akigombewa na kigogo mmoja wa upinzani na mwanaume mwingine?
 
Katika gazeti la mwananchi toleo la leo ametajwa kuwa huyo mwanamama ndiye mchumba wa Dk Slaa. Jina lake anaitwa Josephine Mushumbusi. Hakuna kigogo wa upinzani aliyekua akimgombea. Ila kuna mtu alijitokeza na madai yake binafsi nadhani hilo linajulikana vizuri na jamii yetu.
​
 
Chama cha majambazi kimetekeleza azma yake. Watanzania ifike mahali tukatae utawala wa aina hii.
 
Huyu mama anaevuja damu si ni yule anaegombewa na wanaume wawili kila mmoja akisema ni mke wake? au nimemfananisha?
 
huwa nafarijika sana kuona watu wenye nia ya dhati na nchi yetu haswa nikimuona Prof. Kahigi huwa nakumbuka mbali sana prof amekuwa ktk kila harakati tangu ajiunge nasi hata jana pia alikuwa mstari wa mbele. Tupo pamoja daima
 
Wewe kweli kalagabaho, hujui kuna sheria tanzania ya kwamba ukiishi na mwanamke zaidi ya miezi sita anakuwa na
kila haki kuitwa mkeo na siyo lazima uwende kanisani au mahakamani kwani hizo ni formalities tu.

Atayajulia wapi hayo huyo konokono?
Huyo mwambie kuna aina mpya ya pedi anaweza kuibandika akakaa siku nzima bila kuibadilisha ndio atakuelewa na kutuliza makalio yake umueleze inapatikana wapi...
 
rev masanilo is an agent of ccm and its mafisadi. The days to hide the truth have gone. What we need to get informed more is the malicious conduct of the sitting government of ccm which can into power by force. The end of sufferings from ccm is coming. God bless josephine! God bless dr.slaa.time will tell! We are ready for fighting to the end until truth is known.

tupo pamoja.........rev amenza kuvurunda
 
Hivi Hizi Post Zako kama Kumi kuhusu Arusha zi ungeziunganisha... na kuelezea hisia zako zote kuhusu maandamano ya Arusha kwa pamoja kuliko kufungulia kila idea inayokuja kichwani Topic yake.

Au mwenzangu unaonaje? Nadhani ungefanya hivyo ushauri wako ungewafikia wote kwa pamoja..
 
CCM wasingehujumu uchaguzi
CDM wasingeandamana
Na mauaji yasingetokea.

JEYKEY=MARALIA SUGU=DSM=BONGOLALA

Proved
 
huu jeykey, zomba,kishongo na dar es salaam ni watu wapuuzi sana
 
Back
Top Bottom