Aleluyah!
Imefika wakati watu wa Mungu mumuogope Mungu. Ninapata hisia kuwa Uongozi ulipo madarakani hauna hata chembe Moja ya utu na hawaamini kuwa Mungu yupo. Namshangaa Anndanenge na IGP kwa kupigana na watu wasio na hatia wnao dai haki zao.
Leo hii ni Hasara kiasi gani wameliingizia taifa letu, Majengo yaliyo haribiwa na mengine kuwaka moto sababu ya mabomu ya machozi yaliyokuwa yanarushwa bila mpango, ni akina mama wangapi wajawazito waliohathirika na mabomu, biashara ngapi zimeharibika, watu wangapi wamejeruhiwa, wacha wale waliokufa.
Hii Damu iliyomwagika bila hatia hakika Mungu anaiona na damu hiyo itaendelea kulia kila kuchapo na hii nio kusema itaisha tu pale watakapo rudi na kutubu.
Mungu Awapongee majeruhi wote na kuwapa pole wote walifikwa na misiba ya ndugu zao wenye uchungu na Nchi yao.