Habari gani uliiona kubwa kwa mwaka 2013? (Kimataifa)

Status
Not open for further replies.
Shambulio la westgate ilikua habari kubwa zaidi sababu kulikua na majibu ya kusubiri na kabla ya majibu ya kuhusu tukio kupatikana kulibidi mjadala mkubwa wa kukisiakisia wako magaidi wangapi,ni kwa nini,wameshaua wangapi,ni akina nani n.k
 
Habari kubwa iliyotikisa dunia ni huu mwendelezo wa mapinduzi kwa nguvu ya watu Maarufu kama ARAB SPRING ambayo kwa mwaka 2013 .MFANO Kuondolewa madarakani kwa Muamal Gadafi(libya),hossen muballak(misri) nk kwasababu viongozi hawa wamekaa muda mrefu madarakani pia baadhi wameuwawa kikatili nk kifo cha Gadafi
 
Habari wana JF,

Sisi China Radio International, Idhaa ya Kiswahili (CRI Swahili), tungependa kupata maoni yako juu ya habari ambayo unaamini ilikuwa habari kubwa kwa mwaka 2013. Aidha, habari 10 zitakazopigiwa kura/pendekezwa ndizo tutazitangaza kuwa habari 10 kubwa zilizopendekezwa na watanzania kupitia mitandao ya kijamii (JamiiForums ukiwa mmojawapo).

Wale watakaotoa maoni ambayo yanashawishi kuwa habari flani ilikuwa kubwa kwa mwaka 2013 na sababu zilizojitosheleza kuonyesha ukubwa wa habari yenyewe watazawadiwa na majina yao yatatangazwa kupitia chaneli yetu ya Kiswahili (CRI Kiswahili). Kuna zawadi takribani 15 na tumewasiliana na Uongozi wa JF ili ufanikishe utoaji wa zawadi hizo kwa washindi.

Tumependekeza habari 15, yawezekana hizi tulizopendekeza zikawa hazitoshi na kuna habari mnaona ingepeswa kuwekwa kwenye orodha, tutaikubali endapo utaambatanisha na sababu za kwanini habari hiyo iwekwe kwenye orodha na huenda ikashinda pia.

Habari 15 tulizopendekeza ni hizi:

1. Shambulizi la kigaidi kwenye jengo la Westgate mjini Nairobi

2. Kimbunga cha Haiyan nchini Philippines kilichosababisha vifo vya watu zaidi ya elfu 6

3. Umoja wa Afrika kujadili uwezekano wa kujitoa ICC

4. Kifo cha aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini hayati Nelson Mandela

5. Makubaliano kuhusu suala la nyuklia kati ya Iran na nchi tano wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama

6. Mgogoro wa Syria na tishio la Marekani kushambulia nchi hiyo baada ya kudaiwa kutumia silaha za kemikali

7. Kuondolewa madarakani kwa Rais Mohamed Morsi wa Misri na mgogoro uliofuata

8. Sakata la Edward Snowden na mpango wa upelelezi wa mawasiliano wa Idara ya Usalama ya Marekani (NSA)

9. Kufungwa kwa shughuli za serikali ya Marekani baada ya bunge kukataa kupitisha bajeti

10. Kupinduliwa kwa Rais Francois Bozize wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na mgogoro uliofuata

11. Kufungwa bajeti ya marekani namba tisa
 
Kwa upande wangu habari ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela inafaa kuwa habari kubwa ya mwaka 2013. Hii ni kutokana na matukio yaliojitokeza kama ifuatavyo;

1.Kuhudhuliwa na viongozi wakubwa duniani, akiwemo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, Rais wa Marekani Barack Obama, Rais wa Cuba Raul Castro na wengine wengi.

2.Hotuba ya Rais wa Marekani ambayo ilipokelewa kwa shangwe na waombolezaji.

3. Kushikana mikono kwa Rais wa Marekani Barack Obama na Rais wa Cuba Raul Castro.

Kwa haya machache na mengine na matukio mengine mengi yanaifanya habari hii kuwa habari kubwa ya mwaka 20131
 
kupatikana kwa papa mpya wa kanisa katoliki Francis,ni tukio kubwa mwaka huu,maana kiongozi huyu kwa kawaida uongozi wake hudumu hadi kifo,labda akijihuzuru kama mtangulizi wake Papa Benedict wa 16
 
HUGO TEVES Mbabe Wa Ulimwengu alianguka Mwaka Huu. Naipa Nafasi Kubwa Sana Habari Hii Kutokana Na Historia Yake Kabla Ya Kufikwa Na Mauti, Hugo Teves, Comred, Alitambulika Na Ulimwengu Kutokana Na Msimamo Wake Alio Nao. Anakumbukwa Sana Kwa Jinsi Alivyependwa Na Laia Wa Venezuela Na Kujenga Nchi Yenye Usawa. Alikuwa Mashuhuri Sana Hasa Kwa Hotuba Zake Kali Aliposhambulia Madola Makubwa Ya Ulimwengu Kama Marekani. Kifo Chake Kilitikisa Vyombo Vya Habari Vya Ulimwengu. Alizikwa Na Ukafanyika Uchaguzi Ambapo Madulo Aliyekuwa Makamu Wa Rais Aliibuka Mshindi. Vyombo Vya Habari Viliwahi Kumnukuu Hugo Wakati Wa Kifo Cha Kanal Muammar Ghadafi Akisema ''utawala Wa Mayang-king Hautaweza Kuitawala Dunia!"
 
MARGRETH TSATCHER Iron Lady Alianguka Mwaka Huu. Napendekeza Habari Hii Iwemo Kwenye Orodha Kutokana Na Umaarufu Wa Chuma Hiki Cha Kike Na Hata Vyombo Vya Habari Vilivyo Chukulia Kwa Uzito Swala Hili. Wakati Wa Utawala Wake Mama Huyu Alikuwa Na Msimamo Wake Na Hakukubali Kila Ushauri, Aliandamwa Na Mavugu Vugu Mbalimbali, Kama Lile La Wafanyakazi Lakini Aliapa Kuwa Sito Badilisha! Hapa Alikuwa Anagoma Kubadili Sera Zake, Dunia Iliamia England Kilipo Tangazwa Kifo Chake. Africa Tutamkumbuka Kwa Kuliachia Huru Koloni La Zimbabwe Ingawa Alikuwa Na Mikwaruzano Na Viongozi Kama Nyerere!
 
Habari ilikuwa kubwa kwa mwaka 2013 ni kifo cha aliekuwa raisi wa afrika kusini nelson mandela >sababu ulimuhusisha mtu mashuhuli duniani, pia matukio yaliyo fuata kama kuudhuliwa na viongozi wakuu wa nchi mbalimbali duniani,, kupeana mkono raisi wa kyuba na usa pia ibada ya mazishi kuonesha karibu na tv zote duniani. Hivi vinafanya habari hii kuwa kubwa zaidi kwa mwaka 2013.
 
Jamaa aliyepanda ktk mnara za simu akitaka jirusha km hatoonana na dhaifu kwa kubambikizwa kesi kibao na apolisi
 
Habari wana JF,

Sisi China Radio International, Idhaa ya Kiswahili (CRI Swahili), tungependa kupata maoni yako juu ya habari ambayo unaamini ilikuwa habari kubwa kwa mwaka 2013. Aidha, habari 10 zitakazopigiwa kura/pendekezwa ndizo tutazitangaza kuwa habari 10 kubwa zilizopendekezwa na watanzania kupitia mitandao ya kijamii (JamiiForums ukiwa mmojawapo).

Wale watakaotoa maoni ambayo yanashawishi kuwa habari flani ilikuwa kubwa kwa mwaka 2013 na sababu zilizojitosheleza kuonyesha ukubwa wa habari yenyewe watazawadiwa na majina yao yatatangazwa kupitia chaneli yetu ya Kiswahili (CRI Kiswahili). Kuna zawadi takribani 15 na tumewasiliana na Uongozi wa JF ili ufanikishe utoaji wa zawadi hizo kwa washindi.

Tumependekeza habari 15, yawezekana hizi tulizopendekeza zikawa hazitoshi na kuna habari mnaona ingepeswa kuwekwa kwenye orodha, tutaikubali endapo utaambatanisha na sababu za kwanini habari hiyo iwekwe kwenye orodha na huenda ikashinda pia.

Habari 15 tulizopendekeza ni hizi:

1. Shambulizi la kigaidi kwenye jengo la Westgate mjini Nairobi

2. Kimbunga cha Haiyan nchini Philippines kilichosababisha vifo vya watu zaidi ya elfu 6

3. Umoja wa Afrika kujadili uwezekano wa kujitoa ICC

4. Kifo cha aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini hayati Nelson Mandela

5. Makubaliano kuhusu suala la nyuklia kati ya Iran na nchi tano wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama

6. Mgogoro wa Syria na tishio la Marekani kushambulia nchi hiyo baada ya kudaiwa kutumia silaha za kemikali

7. Kuondolewa madarakani kwa Rais Mohamed Morsi wa Misri na mgogoro uliofuata

8. Sakata la Edward Snowden na mpango wa upelelezi wa mawasiliano wa Idara ya Usalama ya Marekani (NSA)

9. Kufungwa kwa shughuli za serikali ya Marekani baada ya bunge kukataa kupitisha bajeti

10. Kupinduliwa kwa Rais Francois Bozize wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na mgogoro uliofuata

11. Kurushwa chombo cha anga ya juu cha ‘China Change 3' na kutua kwenye mwezi

12. Kufikiwa kwa makubaliano ya biashara ya raundi ya Doha

13. Kupungua kwa tatizo la uharamia katika pwani ya Somalia na Ghuba ya Aden

14. Tukio la ubakaji nchini India lilisababisha kifo cha msichana mwanafunzi

15. Kufichuka kwa siri ya kutumia dawa za kuongeza nguvu kwa mwendesha baiskeli Lance Armstrong

Karibuni

Wachina kukamatwa na shehena kubwa ya meno ya Tembo leo tarehe 31.12,2013 katika Bandari ya Dar Es Salaam
Ni habari ya Kimataifa kwakuwa
1. inahusisha zaifa zaidi ya moja,
2. Nchi ya Tanzania na China ni rafiki sana hususan CCM ambayo hata Balozi wa China nchini Tanzania aliweza kuvaa sare za chama na kuhudhuria mikutano ya CCM
3. Nchini Tanzania kumekuwa na kasi kubwa ya kupungua kwa Tembo amabao ni moja ya vivutio vikubwa katika utalii nchini Tanzania.
4. Hili suala limepelekea kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri nchini Tanzania
 
kifo cha Nelson Madiba Mandela wa africa kusini.msiba ulioshitua mataifa mengi na kufanya mataifa mengi takribani ya 99% kupandisha bendera nusu mringoti kuomboreza msiba mkubwa.Uzalendo wa ujasiri wa kupigania uhuru,ubaguzi wa rangi,unyanyasaji na uzaririshaji wa makaburu ulimpelekea kufunga jera kwa miaka kazaa na mateso.Tanzania ilikuwa kinara juu ya msaada wa kielimu na mafunzo mbalimbali kwa wazalendo wa afrika kusini na kupelekea uhuru kupatikana.mzee atakumbukwa kwa mambo mengi aliyoyafanya kuiletea maendeleo nchi yake na funzo kwa mataifa yote, na hasa tabia ya kusamehe maadui zake na kuondoa tofauti zao.
 
kwangu mimi kama mtanzania niliguswa sana na lile tukio la ARUSHA SOWETO Watanzania wengi kabla hatujapata taarifa kamili moja kwa moja tulijua ni AL~SHAABABU washa tia timu BONGO
 
habari number 1. Shambulizi la kigaidi
kwenye jengo la
Westgate mjini Nairobi..
Kwani walikufa watu wengi na wasio na hatia pia walijeruhiwa ndugu na jamaa zetu, shambulio hilo pha lilisababisha watalii kupungua kuingia afrika mashariki kwa ujumla kwa kuhofia ugaidi...
 
hiko kimbunga sikukisikia, ila wale KDF wa kenya waliokuwa wanatoka na vifuko vyeupe westgate nilisikia

ila mandela baba lao
 
Funga mwaka ni habari ya tar 31.12.2013,ambapo shehena kubwa ya meno ya tembo ilikamatwa,ikihusisha meli ya kivita ya china.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom