Habari gani uliiona kubwa kwa mwaka 2013? (Kimataifa)

Status
Not open for further replies.

CRI Swahili

Verified Member
Dec 21, 2013
19
20
Habari wana JF,

Sisi China Radio International, Idhaa ya Kiswahili (CRI Swahili), tungependa kupata maoni yako juu ya habari ambayo unaamini ilikuwa habari kubwa kwa mwaka 2013. Aidha, habari 10 zitakazopigiwa kura/pendekezwa ndizo tutazitangaza kuwa habari 10 kubwa zilizopendekezwa na watanzania kupitia mitandao ya kijamii (JamiiForums ukiwa mmojawapo).

Wale watakaotoa maoni ambayo yanashawishi kuwa habari flani ilikuwa kubwa kwa mwaka 2013 na sababu zilizojitosheleza kuonyesha ukubwa wa habari yenyewe watazawadiwa na majina yao yatatangazwa kupitia chaneli yetu ya Kiswahili (CRI Kiswahili). Kuna zawadi takribani 15 na tumewasiliana na Uongozi wa JF ili ufanikishe utoaji wa zawadi hizo kwa washindi.

Tumependekeza habari 15, yawezekana hizi tulizopendekeza zikawa hazitoshi na kuna habari mnaona ingepeswa kuwekwa kwenye orodha, tutaikubali endapo utaambatanisha na sababu za kwanini habari hiyo iwekwe kwenye orodha na huenda ikashinda pia.

Habari 15 tulizopendekeza ni hizi:

1. Shambulizi la kigaidi kwenye jengo la Westgate mjini Nairobi

2. Kimbunga cha Haiyan nchini Philippines kilichosababisha vifo vya watu zaidi ya elfu 6

3. Umoja wa Afrika kujadili uwezekano wa kujitoa ICC

4. Kifo cha aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini hayati Nelson Mandela

5. Makubaliano kuhusu suala la nyuklia kati ya Iran na nchi tano wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama

6. Mgogoro wa Syria na tishio la Marekani kushambulia nchi hiyo baada ya kudaiwa kutumia silaha za kemikali

7. Kuondolewa madarakani kwa Rais Mohamed Morsi wa Misri na mgogoro uliofuata

8. Sakata la Edward Snowden na mpango wa upelelezi wa mawasiliano wa Idara ya Usalama ya Marekani (NSA)

9. Kufungwa kwa shughuli za serikali ya Marekani baada ya bunge kukataa kupitisha bajeti

10. Kupinduliwa kwa Rais Francois Bozize wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na mgogoro uliofuata

11. Kurushwa chombo cha anga ya juu cha ‘China Change 3’ na kutua kwenye mwezi

12. Kufikiwa kwa makubaliano ya biashara ya raundi ya Doha

13. Kupungua kwa tatizo la uharamia katika pwani ya Somalia na Ghuba ya Aden

14. Tukio la ubakaji nchini India lilisababisha kifo cha msichana mwanafunzi

15. Kufichuka kwa siri ya kutumia dawa za kuongeza nguvu kwa mwendesha baiskeli Lance Armstrong

Karibuni..

*Tembelea ukurasa wetu wa Facebook kila siku ili kuhabarika kuhusu hali ya China kwa dunia kwa lugha ya Kiswahili | Bofya =>> CRI Kiswahili
 

LEO

Member
Oct 9, 2007
10
45
Kifo cha Nelson Mandela. Kilikusanya karibu viongozi wote wakubwa Duniani
 

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,909
2,000
Kifo cha aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini hayati Nelson Mandela ndiyo habari iliyopewa kipaumbele katika vyombo vya habari duniani kote..
 

zumbemkuu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
10,245
2,000
habari zote mlizopendekeza zilikuwa kubwa lakini hilo la kuondolewa madarakani kwa rais Mohamed Morsi liliteka vyombo vya habari kwa mda mrefu zaidi,
 

Super H

JF-Expert Member
Oct 6, 2012
1,059
1,225
Habari kubwa na ambayo sitokaa niisahu maishani ni shambulio la Alshabab kuua watu wasio na hatia Westgates na aibu ya majeshi ya Kenya kuiba mali badala ya kuokoa na kupambana na magaidi.

Na hadi leo hii hakuna ushahidi wa kuuawa hata gaidi mmoja
 

Blessed

JF-Expert Member
Nov 16, 2011
3,122
2,000
Habari ya Westgate.

Sababu:
- Ilidumu kwa muda mrefu
- Kenya ni majirani wa Tanzania hivyo ni wazi matatizo yao yalivuta hisia za watanzania kwa kiasi kikubwa.
- Watu wengi tulikuwa tunaangalia kwa hamu kuona hatima ya mateka wale
 

Kayoka

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
1,882
2,000
Habari namba 6 na namba 7 ziliongoza kuzungumzwa sana katka mwaka 2013 na naamini pia kwa mwaka 2014 bado zitazidi kuzungumzwa.

Yaani:
6. Mgogoro wa Syria
7. Mgogoro wa Misri
 

byancas

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
268
250
Tukio la ubakaji nchini India lilisababisha kifo cha msichana mwanafunzi, hili tukio lilitikisa sana dunia kwa maana vijana wengi nchini India imekuwa kawaida yao kufanya matendo ya kudhalilisha wakina dada, na hawa vijana walifanya kitu cha kinyama sana kumbaka na kumuua.

Macho na masikio ya Dunia yalikuwa katika kesi ile kuona wale vijana hatma yake itakuwa vipi na mwishowe mahakama ikatenda haki na kufanya kuwa fundisho kwa vijana wengine wenye tabia ile. Ilikuwa faraja kwa wakina mama na mabinti wanaofanyiwa vitendo vile bila sheria kuchukua mkondo
 

Joseph M. Bahayile

New Member
Dec 2, 2013
4
0
2: "Kimbunga ch Haiyan cha Ufilipino kilichoua watu zaidi ya 6000" ndicho kimetikisa dunia!

Kwa sababu:
-Kimeibua hofu, majonzi na simanzi kwa walimwengu wote
-Kimeleta hasara kubwa kwa taifa husika na ulimwengu mzima, mali kuharibika, miundo mbinu kuvunjwa n.k.
-Kimepoteza maisha ya wengi ambao ni nguvu kazi iliyotegemewa.
-Kimetufanya wengi tumsogelee Mungu kwa maombi, imani yetu ikakomaa.
-Kimeongeza idadi ya wategemezi; vilema, wajane na mayatima.

KILITIKISA DUNIA
 

isack raphael

Senior Member
Oct 26, 2013
131
195
Namba 4 kifo cha aliyekuwa rais wa afrika kusini.
Hii habari iligusa hisia za watu wengi sana na kuzungumzwa sana.
 

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
2,000
Tumependekeza habari 15, yawezekana hizi tulizopendekeza zikawa hazitoshi na kuna habari mnaona ingepeswa kuwekwa kwenye orodha, tutaikubali endapo utaambatanisha na sababu za kwanini habari hiyo iwekwe kwenye orodha na huenda ikashinda pia.

KIFO CHA NELSON MANDELA KWA MAONI YANGU ILIKUWA NI HABARI KUBWA DUNIANI.
Kwanza Lazima tukili kuwa Ukubwa wa Habari ni namna vile imesikika Ulimwenguni kwa ukubwa gani? Imepewa Umakini (Tension) kwa ukubwa gani na imekuwa Gumzo kiasi gani pia Imeandikwa kiasi gani?

Kifo cha Nelson Mandela naona ndio habari kubwa zaidi Duniani kwa Mwaka 2013 licha ya kuwa imetokea Mwishoni mwa Mwaka lakini ipo ndani ya 2013.

Sababu ni:
1. Imehusisha mtu ambaye ni mashuhuri Ulimwenguni kwenye medani zote, siasa, michezo, uchumi na Uhusiano wa jamii. Nelson Mandela katika maisha yake amedeal na mambo yote kwa wakati kadhaa(Michezo alileta kombe la Dunia Afrika katika historia ya Ulimwengu huu tangu kuumbwa)..

2. Nelson Mandela baada ya Kifo chake ndiye mtu aliyeongoza kwa kutafutwa kwenye GOOGLE kulikomtu yeyote Hapa Duniani kwa mwaka 2013. Hii inamaanisha habari za Kifo chake zilikuwa zimeenea sana Duniani na zilichukuliwa kwa Ukubwa wa aina yake ndio maana watu walilazimika kuzama mitandano kumjua huyu mtu ni alikuwa ni waaina gani n.k

3. Kifo cha MANDELA ndio kifo pekee kwa Karne kadhaa kilichokutanisha Marais karibia nusu ya Dunia kwenye Aridhi moja na kuna Nchi Marais wao wote (wastaafu na waliopo madarakani walifika) Afrika kusini. Hii ni wazi kuwa HABARI ZA KIFO CHA MANDELA ZILIKUWA NI KUBWA ULIMWENGUNI na ZIlipewa heshima na Umakini wa aina yake ambao utachukua Miaka kadhaa kuja kutokea tena. Isingekuwa habari kubwa na nzito basi tusingeona dunia ikijumuika pamoja na kusherekea maisha ya Madiba.

4. Tension kwa Vyombo vya Habari: Kifo cha mandela ndio habari iliyochukua zaidi ya robo tatu ya Vyombo vya habari vya serikali na vya Binafsi ulimwengu mzima kuonesha na kuripoti kile kinachoendelea kwenye msiba Ule. Kitendo cha Vyombo vya habari magazeti n.k kuwekeza macho yao zaidi ya Wiki nzima kwenye msiba wa Mandela hii ni wazi Kifo chake kilikuwa ndio habari kubwa zaidi kwa Ulimwengu mwaka 2013.
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom