Ngambo Ngali
JF-Expert Member
- Apr 17, 2009
- 3,517
- 1,367
kwa hiyo unataka mengi aitishe mkutano awaambie mwananchi wachangie, au mengi ni kiongozi wa mtaa ziliko ofisi IPP wa kitogoji, kwani jukumu la usafi au kujenga barabara ni mengi?..atajenga barabara ngapi maana ninavyojua mengi anamakampuni mengi sana..huna lolote wewe umetumwa na mafisadi tuNyie Wapambe wa Mengi,
Haya yambo kayapigia sana kelele humu ndani Mzee Mwanakijiji. Haya mambo ya ohh mbona siko peke yangu, ohh ni jukumu la serikali, ohhh kifo cha wengi harusi, ndiyo yanayotufanya milele tubaki palepale.
Mengi ni mtu maarufu sana na milele popote alipo ataonekana yeye. Kusema kuna wengine pale basi si awaite na kuwaambia wachangie kujenga hiyo barabara? Anasubiri na yeye kila kitu maana kashalipa kodi?
Nikiwa naishi Ilala Flats, tulikuwa na jirani yetu mmoja Mhandisi, Mzee Ngonyani. Kutokana na mabomba ya maji machafu kuziba, maji taka yalikuwa yakimwagika nje na kutoa harufu mbaya sana, wenyewe wakisema MAFURIKO. Yakitokea kinachofanywa mnafunga madirisha ya upande huo. Mhandisi huyo alifika point akachoka, akaja kuitisha mkutano kuwa ataenda kununua mabomba na kugharamia ujenzi wake. Wanaotaka kumsaidia wamsaidie na wasiotaka waache. Huwezi amini, wote walitoa hela. Tatizo dogo lipo kwa Msomali, yeye siku zote anasema "hana muda, wampe gharama na yeye atatoa pesa - Yes alitoa hela..." Wakati mwingine ni vitu viko ndani ya uwezo wetu ila tunakosa KIONGOZI. Kila mtu au anaona hilo HALIMHUSU au anasubiri FULANI aanze.
Tusiwe waoga namna hiyo. Mwambieni Mzee ashirikiane na jirani zake hao wenye mashine za kufulia sijui, na wenye viwanda wengine, unaweza kukuta wakapata hata msaada kutoka EU kama wao ni masikini saana na ile barabara ikajengwa kwa Zege ili kuhimili mizigo mizito kutoka kiwandani. Cement Tanzania ipo, mawe na mchanga upo, shida iko wapi? Ni pesa tu. Hao watu kama wameweza kuwa na Viwanda, kinawashinda nini kujenga barabara au Parking?
Mnaweza kumtetea sana ila ukweli ni kuwa UJUMBE UMEMFIKIA. Na kama nyie ni Wapambe wake basi MFIKISHIENI. Siku anafungua na aseme kuwa wameijenga kwa ushirikiano na wenzake. Labda itakuwa mfano kwa watu wengi huko mitaani kushirikiana na kuweka mazingira yao katika hali safi. Tunaisubiri saana serikali wakati serikali yenyewe ni ya CCM (Chama Cha Mafisadi).
kwa hiyo unataka mengi aitishe mkutano awaambie mwananchi wachangie, au mengi ni kiongozi wa mtaa ziliko ofisi IPP wa kitogoji, kwani jukumu la usafi au kujenga barabara ni mengi?..atajenga barabara ngapi maana ninavyojua mengi anamakampuni mengi sana..huna lolote wewe umetumwa na mafisadi tu
Nchi nzima iko shaghalabagala sasa kwa nini unam single out Mengi? Mavumbi umeyaona ofisini kwake tu? Sinza hakuna mavumbi? Tandale hakuna mavumbi? Upanga hakuna mavumbi? Sengerema hakuna mavumbi? Kisesa je?
Sasa kama mavumbi ni commonplace Tanzania kwa nini umlaumu yeye tu? Tujilaumu sote kama taifa na si mtu mmoja mmoja kwa vile tu wanahadhi fulani.
Ngabu,
Kwa bahati mbaya, watu au maeneo yenye wakazi ambao wanakipato cha juu yanakuwa singled out. Unajua kwa nini? Kwa sababu huko ndiko ambako mtari umechorwa juu sana. Hivi unajua kwa nini watu wanaponda barabara za mitaa ya Mikocheni na Mbezi Beach? Ushasikia watu wanaponda njia za mitaa ya Manzese, Tandika, Buguruni, na kadhalika?
Watanzania kweli nchi yetu imejichokea, na hatujui nini kazi ya kodi zetu. Sasa leo hii Mengi awakusanye wenye viwanda wenzake wafanye harambee wajenge barabara na kodi wanazolipa zitafanyia nini?
kwa hiyo unataka mengi aitishe mkutano awaambie mwananchi wachangie, au mengi ni kiongozi wa mtaa ziliko ofisi IPP wa kitogoji, kwani jukumu la usafi au kujenga barabara ni mengi?..atajenga barabara ngapi maana ninavyojua mengi anamakampuni mengi sana..huna lolote wewe umetumwa na mafisadi tu
Nchi nzima iko shaghalabagala sasa kwa nini unam single out Mengi? Mavumbi umeyaona ofisini kwake tu? Sinza hakuna mavumbi? Tandale hakuna mavumbi? Upanga hakuna mavumbi? Sengerema hakuna mavumbi? Kisesa je?
Sasa kama mavumbi ni common place Tanzania kwa nini umlaumu yeye tu? Tujilaumu sote kama taifa na si mtu mmoja mmoja kwa vile tu wanahadhi fulani.
Watanzania kweli nchi yetu imejichokea, na hatujui nini kazi ya kodi zetu. Sasa leo hii Mengi awakusanye wenye viwanda wenzake wafanye harambee wajenge barabara na kodi wanazolipa zitafanyia nini?