Haaaa Mzee Mengi!!

Status
Not open for further replies.

Quemu

JF-Expert Member
Jun 27, 2007
984
128
Hivi mzee Mengi ameshindwa kabisa kujali barabara inayokwenda kwenye ofisi kuu za media stream yake? Yaani unakwenda kutembelea kwenye zile ofisi unakumbana na vumbi tu barabarani. Hiyo parking ya wageni wake ndio imenichosha kabisa.

Kwa "elite member" wa jamii yetu kama yeye (ambaye anajihusisha kwa karibu na shughuli za mazingira na kadhalika) ungedhani kuwa angeweka mfano madhubuti kwenye maeneo ya biashara zake.

Hebu jioneeni mazingira ya Ippmedia, ukilinganisha na yale ya TBC:

IPPMEDIA

Barabara ya kwenda Ippmedia
quemu-albums-tbc-vs-ipp-picture583-ipp6.bmp

quemu-albums-tbc-vs-ipp-picture577-ipp.bmp

Parking ya Ippmedia
quemu-albums-tbc-vs-ipp-picture585-ipp5.bmp

quemu-albums-tbc-vs-ipp-picture580-ipp3.bmp

quemu-albums-tbc-vs-ipp-picture579-ipp2.bmp

TBC

Barabara ya kwenda TBC

quemu-albums-tbc-vs-ipp-picture590-tbc5.bmp

quemu-albums-tbc-vs-ipp-picture589-tbc4.bmp

Parking ya TBC
quemu-albums-tbc-vs-ipp-picture588-tbc3.bmp

Nothing personal mzee.....ni kukumbushana tu!!!!
 
tangu lini Mengi ni fundi wa mabarabara, analipa kodi zote kwa mujibu wa sheria, bado unashauri ajenge barabara ya kwenda kwenye ofisi yake...nini kazi ya serikali ya mkoa kupitia halmashauri za jiji.
KAMA HUNA CHA KUPOST ZIMA COMPUTER YAKO
 
Sawa nitazima pindi Luku itakaponiishia dakika tano zijazo!

Kwa hiyo hata parking ya ofisi zake ni jukumu la halmashauri ya jiji?
 
Hivi mzee Mengi ameshindwa kabisa kujali barabara inayokwenda kwenye ofisi kuu za media stream yake? Yaani unakwenda kutembelea kwenye zile ofisi unakumbana na vumbi tu barabarani. Hiyo parking ya wageni wake ndio imenichosha kabisa.

Kwa "elite member" wa jamii yetu kama yeye (ambaye anajihusisha kwa karibu na shughuli za mazingira na kadhalika) ungedhani kuwa angeweka mfano madhubuti kwenye maeneo ya biashara zake.

Nadhani na wewe una ajenda yako. Ulitaka Mengi awafanyie kazi jiji wao waendelee kuponda raha wanakusanya kodi na kutafuna bata. Yeye alipe kodi, alafu ajenge barabara kwa kumfurahisha nani??

Wewe umejenga chochote wapi???
 
bado kutuambia kuwa mengi ajapaka nyumba yake rangi
parking ya ippmedia sio ishu ya kisiasa....
swali la barabara unglipeleka halmashauri ya jiji
 
Ok naona watu mmekazania hilo la barabara pekee kwa sababu angalau serikali inaweza kutupiwa mpira wa lawama kirahisi.

Vipi kuhusu hili la parking ya ofisi zake. Mbona mnajifanya hamlioni? Au na hili Serikali inahusika?

Mimi sijajenga popote pale kwa sababu sina uwezo wa kufanya hivyo. Pia, mimi sina uwezo wa kuwa na ofisi zangu. Isitoshe mimi sina hadhi ya kama mzee wetu ambaye anaonekana kwenye vyombo vya habari kila siku ikisimekana anajishughulisha na mambo mbalimbali ya kijamii, ikiwa pamoja na mazingira.
 
Ofisi si zake bana...sasa kama hataki kuziweka kama unavyotaka wewe tatizo lako nini? Kitu chake lakini bado unataka ku impose mambo kwa jinsi uyaonavyo wewe kuwa ndo sawa
 
Ishu inabaki palepale, ungetegemea kwa mtu wa hadhi nchini ambaye anajihusisha na ishu za mazingira ya jamii angeonyesha mfano kwenye mazingira yanayomzunguka.

Hivi umeshawahi kuona jinsi kulivyokuwa na vumbi pembezoni mwa ofisi zake? Only kama wafanyakazi wake wangekwenda kwenye chest x-ray exam ndivyo ingedhibitisha ni jinsi gani mazingira ya ofisi za mwanamazingira maarufu nchini yalivyokuwa.
 
Ofisi si zake bana...sasa kama hataki kuziweka kama unavyotaka wewe tatizo lako nini? Kitu chake lakini bado unataka ku impose mambo kwa jinsi uyaonavyo wewe kuwa ndo sawa

Sasa na wewe mbona unaanguka kwenye msemo wako maarufu (Miafrika Ndivyo Tulivyo). Yaani huoni kabisa (kwa hadhi yake na jinsi alivyokuwa mtari wa mbele kwenye shughuli za kijamii) mazingira ya ofisi zake yanavyomsuta?

Jamani yule ni role model kwa watu wengi tu (mimi mmoja wao). Kwa hiyo kila anachojihusisha kwenye jamii kinatugusa kwa namna moja au nyingine. Isitoshe, tunaainisha mazingira yanayomzunguka na na kile anachofanya kwenye jamii. Ndio maana ya kuwa "mfano" wa kuigwa huko...au?
 
Kwani Miafrika Ndivyo Tulivyo ni uongo? Kama unadhani ni uongo hebu kata mbunga Afrika kusini mwa jangwa la sahara ujionee...
 
Nakubaliana na mzee mtoa hoja kwamba kuna tatizo! Vile vibanda vya mama ntilie vichafu na vibaya bado viko kwenye ile barabara.

Kwa m2 wa Mazingira kama mzee Mengi.... ile barabaa inayoelekea kwake inatia kichefu chefu.
 
Sasa kama barabara inatia kichefu chefu, kwani ni jukumu la Mengi kuitengeneza?? Serikali kwa kupitia Halmashauri ya Jiji ndio inapaswa kujenga ile barabara.
 
tangu lini Mengi ni fundi wa mabarabara, analipa kodi zote kwa mujibu wa sheria, bado unashauri ajenge barabara ya kwenda kwenye ofisi yake...nini kazi ya serikali ya mkoa kupitia halmashauri za jiji.
KAMA HUNA CHA KUPOST ZIMA COMPUTER YAKO
Quemu umechokoza moto kwa taarifa yako fedha hizo badala ya kutengeneza parking zinafanya kazi hii ya kulipa vikaragosi vya kumtetea na kumtukuza utatupiwa matusi bure kama mzee kingunge alivyotukanwa na kilaini
 
''tangu lini Mengi ni fundi wa mabarabara, analipa kodi zote kwa mujibu wa sheria, bado unashauri ajenge barabara ya kwenda kwenye ofisi yake...nini kazi ya serikali ya mkoa kupitia halmashauri za jiji.
KAMA HUNA CHA KUPOST ZIMA COMPUTER YAKO''

Acha upuuzi mwenzako anapoandika jambo la msingi unamwambia azime kompyuta?Kama hujawahi kufika ITV/RADIO one ukaona parking ilivyo kaa kimya usilete ukenge hapa. https://www.jamiiforums.com/newreply.php?do=newreply&p=573174 https://www.jamiiforums.com/newreply.php?do=newreply&p=573174
 
Dah naona payroll bado inafanya kazi kweli kweli ukimgusa huyu mzee dah teh teh teh ...
 
Hivi mzee Mengi ameshindwa kabisa kujali barabara inayokwenda kwenye ofisi kuu za media stream yake? Yaani unakwenda kutembelea kwenye zile ofisi unakumbana na vumbi tu barabarani. Hiyo parking ya wageni wake ndio imenichosha kabisa.

Kwa "elite member" wa jamii yetu kama yeye (ambaye anajihusisha kwa karibu na shughuli za mazingira na kadhalika) ungedhani kuwa angeweka mfano madhubuti kwenye maeneo ya biashara zake.
Wakulaumiwa ni Mzee Mengi au Manispaa..na unawezaje kulinganisha TBC na IPP media...je vipi tukilinganisha choo chako na cha ikulu...Salaevo alijitolea kujenga barabara ya kwenda kwenye Min supermarket yake kama nusu km akaweka na kidaraja...TRA walihamia kwake wanataka kodi...
 
Tukiacha ushabiki ukweli ni kuwa suala la barabara sio kazi ya mengi.Mbona ukienda Slipway hali ni ileile?inawezekana wazee wa jiji hawatengenezi barabara mpaka uwagrease kidogo.Zile barabara nzuri kule oysterbay zina maana gani kiuchumi ukilinganisha na hizo za IPP na slipway amabao ni mataxpayers wakubwa na watoa ajira?Migombani street iliwekawa lami baada ya mwanamtaa kuwa rais ans sana wameirefusha mpaka Shoppers plaza.Sasa shoppers ans Slipwaya pana tofauti?
 
''tangu lini Mengi ni fundi wa mabarabara, analipa kodi zote kwa mujibu wa sheria, bado unashauri ajenge barabara ya kwenda kwenye ofisi yake...nini kazi ya serikali ya mkoa kupitia halmashauri za jiji.
KAMA HUNA CHA KUPOST ZIMA COMPUTER YAKO''

Acha upuuzi mwenzako anapoandika jambo la msingi unamwambia azime kompyuta?Kama hujawahi kufika ITV/RADIO one ukaona parking ilivyo kaa kimya usilete ukenge hapa.
Quemu umechokoza moto kwa taarifa yako fedha hizo badala ya kutengeneza parking zinafanya kazi hii ya kulipa vikaragosi vya kumtetea na kumtukuza utatupiwa matusi bure kama mzee kingunge alivyotukanwa na kilaini
ni ujinga kufikiri kuwa wajibu wa Mengi ni kujenga mabarabara, au miundo mbinu, anaweza kuchangia akitaka......
eti mengi kanunua Vikaragosi vya kumtetea...ni aina ya mawazo mgando bado hujatahiri ubongo wako sikushangaeni
 
Ok naona watu mmekazania hilo la barabara pekee kwa sababu angalau serikali inaweza kutupiwa mpira wa lawama kirahisi.

Vipi kuhusu hili la parking ya ofisi zake. Mbona mnajifanya hamlioni? Au na hili Serikali inahusika?

Mimi sijajenga popote pale kwa sababu sina uwezo wa kufanya hivyo. Pia, mimi sina uwezo wa kuwa na ofisi zangu. Isitoshe mimi sina hadhi ya kama mzee wetu ambaye anaonekana kwenye vyombo vya habari kila siku ikisimekana anajishughulisha na mambo mbalimbali ya kijamii, ikiwa pamoja na mazingira.

Quemu,
wenye akili timamu tumekuelewa, acha kujibizana na hao mahayawani, hii ndo JF kuna wenyenazo na hamnazo wala usishangae, wao huongozwa na jazba katika kutoa michango yao ya mawazo.

Usafi ni tabia ya mtu, Kama Mengi angekuwa na tabia hiyo basi mazingira ya ofisi zake yangekuwa mfano.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom