Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 498
- 785
Dar es Salaam, kama jiji kubwa na kitovu cha uchumi wa nchi, linapaswa kuwa mfano bora wa usafi na upangaji wa mazingira. Hata hivyo, hali halisi inayoonekana mitaani inazua maswali mengi kuhusu uwajibikaji wa viongozi na utekelezaji wa majukumu yao.
Katika maeneo kama Makumbusho, Kijitonyama, Sinza na Kawe, Mikocheni ni jambo la kawaida kukutana na mitaro iliyojaa taka, maji machafu yaliyotuama na harufu isiyovumilika. Hali ni hiyo hiyo pia katika maeneo ya Posta na Kariakoo, ambayo ndiyo sura ya jiji kwa wageni wengi sio ajabu kuona maji taka ya chemba na uchafu vikizagaa kwenye maeneo hayo.
Kinachotia wasiwasi zaidi ni kwamba taka zimezagaa katika mitaa mingi bila kuwa na miundombinu ya kutosha ya ukusanyaji na utupaji inayolingana na kasi ya ukuaji wa jiji. Jiji linaendelea kupanuka kwa kasi, lakini mifumo ya usafi wa mazingira inaonekana kubaki nyuma. Hili linaibua swali la msingi: je, mipango ya usafi ipo kweli, au ipo kwenye makaratasi tu?
Mbali na taka, pia kuna tatizo la maeneo mengi kuto fyekwa. Kuanzia Temeke maeneo ya ambayo yapo penbezoni mwa barabara, Mbezi Beach, Kimara na meneo mengine majani marefu yamekuwa sehemu ya mandhari ya kawaida. Hali hii si tu inapunguza hadhi ya jiji, bali pia inachangia kuongezeka kwa mazalia ya mbu na hatari za kiafya kwa wakazi. Usafi wa mazingira si suala la mandhari tu, bali ni suala la afya ya umma na ustawi wa jamii.
Wengi wanakumbuka kipindi cha uongozi wa hayati Rais Dkt. John Magufuli, ambapo kulikuwa na msisitizo mkubwa wa usafi wa mazingira. Ingawa kulikuwa na changamoto zake, mpango ule ulikuwa na mwelekeo, ulikuwa shirikishi, na ulihamasisha uwajibikaji kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja hadi taasisi. Leo hii, juhudi kama hizo zinaonekana kufifia, na pengo hilo linaonekana wazi mitaani.
Swali la kujiuliza ni hili: licha ya kuwepo kwa viongozi na wataalamu wa mazingira katika kila wilaya, kwanini bado hatuoni ubunifu wa wazi na hatua madhubuti za kuboresha hali ya usafi? Je, tatizo ni ukosefu wa rasilimali, usimamizi dhaifu, au kutopewa kipaumbele kwa suala hili?
Ni wakati sasa kwa viongozi kuwajibika na kuweka mikakati inayoonekana na kupimika. Wananchi pia wana wajibu wa kushiriki, lakini uongozi thabiti na mifumo madhubuti ni msingi wa mabadiliko. Bila hatua za makusudi, Dar es Salaam itaendelea kupoteza hadhi yake na kuhatarisha afya za wakazi wake.