Government Ban Job Recruitment Agencies!

Government Ban Job Recruitment Agencies!

Hizo recruitment agencie zinapaswa kuafauata sheria na pia serikali lazima ihakikishe zinakuwa regulated.Kuna unyonyaji,kiburi za lugha mbaya sana kwa watumishi wa hizo agency..kwa mfano Erolink!!
 
Hii ni kete ya serikali kubaki madarakani, wamefocus wakaona kuwa kwa kuwa adui zao kwa sasa ni vijana, na wengi wa vijana hawana ajira kwa sasa licha ya kuwa na sifa nzuri tuu.

Ila pamoja na trick hii ya kusaidia vijana wasio na ajira, wizara ikae ikijua bado nafasi nyingine ambazo zipo ndani ya uwezo wa watanzania wengi zimekaliwa na wageni, hatukatai wageni kufanya kazi nchini. Ila kuwe na ulazima wa wageni kuja kufanya kazi nchini.

Ukiachilia hilo, imefikia mpaka baadhi ya kampuni kazi zake zinakuwa conducted/performed toka nje ya nchi ilhali zilikuwa zikifanyika kutokea hapa nchini (mfano NMC Vodacom under NSN ilipelekea wazawa kupunguzwa kazi).
 
Binafsi nimeguswa na tamko la serikali kupitia Wizara ya Kazi na Ajira ya kusitisha utaratibu wa udalali wa kukodisha wafanyakazi katika makampuni unaofanywa na baadhi ya Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira nchini.

Nimewahi kuajiriwa katika system za hivyo na ni shahidi ni kiasi gani zinavyowasababishia wafanyakazi kero, hasa inapokuja swala la Kujiendeleza kimasomo na likizo. Pia imekuwa chanzo cha unyonyaji wa jasho la wafnyakazi kwani ili alipwe lazima hela yake ipitea kwa Kampuni iliyompatia kazi na hivyo anagawana nayo, mgawo ambao mara nyingi unampunja mfanyakazi huyo. Hii ni tabia common katika makampuni ya ulinzi kama KK Security na Venture Risk Management.

Naamini kama hili litatekelezwa lisaidia kuboresha maisha ya wengi na kwa niaba ya wote napongeza hatua hiyo.
 

Attachments

Kampuni kama Radar Recruitment robo tatu ya wafanyakazi wake ni wageni si watanzania tutegemee nini hapa. BG au British Gas imejaza wakenya kweli ndiyo hayo matokeo ya uchumi wa gas yatamnufaishaje mtanzania???
 
Bongo bwana, sasa huyu mama katumia sheria gani kuzifungia??!! Hao jamaa kama wako makini wakienda mahakamani wanashinda.

Tena tukufwatilia vifungu vya sheria ndio kabisaa, hawa outsourcing companies wanakiuka mnoo sheria za ajira.
Wasijaribu kwenda mahakamani.
 
Naona dhana nzima ya staffing services bado haijazoeleka na kueleweka Tanzania, kulingana na malalamiko ya watu humu.

Kwa uzoefu wangu sijawahi kuona sehemu yoyote ile ambapo mtu anatafuta kazi kupitia staffing agency halafu agency isipate asilimia fulani ya malipo kutoka kwa waajiriwa wake.
 
Kama kuna kitu ambacho kimekuwa kikichefua moyo wangu, ni pamoja na hili la makampuni kuwaona wafanyakazi wao kama viraka tu! Nimekuwa nikijiuliza hawa recruters agences wanamilikije idadi kubwa ya wafanyakazi wakati ofisi zao zipo kwenye mikoba tu?! Na kwanini mfanyakazi wa kampuni unayofanyia kazi pindi upatwapo na tatizo, kampuni inakuambia kuwa wewe si mwajiriwa wetu bali wewe ni wa agent aliyekuleta! Hili lipo tanzania tu. Kwa tangazo hili la wafanyakazi kumilikiwa na kampuni wanazofanyia kazi ni la kupongezwa sana. Kama si matamshi ya kisiasa ngoja tusubiri matokeo ndani ya hizi cku 30.

Habari hii si Tanzania tu, Marekani hii issue imekuwa bonge la industry kwa wajanja wachache. Mtu analipwa dola 60 kwa saa sehemu anapofanya kazi, lakini kwa agency kaambiwa analipwa dola 50 kwa saa, kwa kila saa anayofanya kazi agency inachukua dola 10. Maana yake akifanya kazi wiki moja masaa 40 agency inachukua dola 400, kwa mwezi inachukua dola 1600, kwa mtu mmoja tu.

Agency ikiwa na vichwa 100 tu vya namna hii, you are talking about $160,000 kwa mwezi.

Kazi yao kufungua kiofisi tu na kukuunganishia, kitu ambacho hata www.monster.com inaweza kufanya.

Ni wizi mtupu.
 
Nakusoma vyema sana mkuu... Ila nadhani wewe ndio hujamuelewa vizuri Waziri wa Kazi na Ajira.

Mkuu kasome tena post yangu. Mleta mada kadai kuwa "government ban job recruitment agencies". Ndo mie nikashangaa kusema that must be the worst decision to make.

Nikasema I think kilichositishwa ni recruitment process outsourcing na siyo recruitment agencies. Sasa hapo ni wapi sikumwelewa Waziri. Maybe sikumwelewa. Wewe umwelewaje Waziri? Tupe uelewa wako mkuu.
 
Naona dhana nzima ya staffing services bado haijazoeleka na kueleweka Tanzania, kulingana na malalamiko ya watu humu.

Kwa uzoefu wangu sijawahi kuona sehemu yoyote ile ambapo mtu anatafuta kazi kupitia staffing agency halafu agency isipate asilimia fulani ya malipo kutoka kwa waajiriwa wake.

Mimi sina tatizo na agencies kuchukua chao, mbona tushazoea hata madalali wa nyumba wanakuunganishia na kuchukua chao?

If this is a one time fee (for direct employment positions), sina tatizo, unawalipa gharama za uwakala wa kukuunganishia (ideally this should be done by the company you will work for to remove the appearance of a quid pro quo based placement and encourage merit based placement).

Tatizo langu linakuja pale agency inapochukua sehemu ya hourly wages/ salary kama vile baada ya kukuunganisha wanafanya sehemu fulani ya kazi zako, wakati wamekaa tu wanakusanya chajuu. Fine, kama umeajiriwa na agency kuna habari za kodi zao na makato and all that, wanaweza kuwajibika kwa hayo, hususan kama umeandikishwa kama muajiriwa wao na sio wa unakofanya kazi (consultancy based assignments), lakini hata katika hayo, mfanyakazi awe na haki basi hata ya kupata full disclosure. Kinacholipwa na anapofanya kazi ni kipi, agency yake inamkata vipi kwa ajili ya health insurance na mafao etc, na yeye anacholipwa ni kipi.

Sasa hivi unaona huyu Ng'wanakilala (is this Lulu?) kaulizwa kitu cha kwanza kusema ni ku cite confidentiality clauses.

I am all for the protection of a healthy business environment, I wrote a lenghty and balanced article at vijana.fm on the subject if I may say so myself. But at some point workers fundamental rights must be protected.

I am all for the free market, but the free market without some obvious regulations is not good even for itself.
 
Habari hii si Tanzania tu, Marekani hii issue imekuwa bonge la industry kwa wajanja wachache. Mtu analipwa dola 60 kwa saa sehemu anapofanya kazi, lakini kwa agency kaambiwa analipwa dola 50 kwa saa, kwa kila saa anayofanya kazi agency inachukua dola 10. Maana yake akifanya kazi wiki mbili masaa 40 agency inachukua dola 400, kwa mwezi inachukua dola 800, kwa mtu mmoja tu.

Agency ikiwa na vichwa 100 tu vya namna hii, you are talking about $80,000 kwa mwezi.

Kazi yao kufungua kiofisi tu na kukuunganishia, kitu ambacho hata www.monster.com inaweza kufanya.

Ni wizi mtupu.

Lakini, hivi kuna mtu ambaye anapitia hizi staffing agencies halafu hajui kwamba kama wakikutafutia kazi, tuseme temp-to-hire, na wao wanakuwa wanapata cha kwao mpaka utapoajiriwa 'permanently' na huko walikokutafutia kazi?

I thought that was common knowledge but the specifics are the ones that were supposed to be confidential?
 
Mkuu naomba nikusahihishe... nielewavyo...kilishizuiwa sio recruitment process outsourcing BALI ni labour brokerage. kuna tofauti hapo.

labour broker ni yule ambae mimi kama kampuni namwambia nahitaji assistant accountants 5, na yeye anawaajiri na kuwaleta kwangu mimi principal. in turn mimi namlipa mshahara wao plus namchaji commission-about 20% of salary..

Mkuu naona ni kitu kile kile. Labour brokering ni form ya recruitment process outsourcing inayofanywa sana Afrika Kusini.

"Labour brokering is a form of outsourcing practiced in South Africa (and formerly practiced in Namibia, where it was known as labour hire) in which companies contract labour brokers to provide them with casual labour. Labour brokers are different from recruitment agencies in that labour brokers handle almost all aspects of the worker's employment (including interviews, recruitment, HR, admin, payroll, transport, etc.), whereas recruitment agencies are only responsible for sourcing candidates for employment. In essence, rather than a company hiring a worker, it hires a labour broker who hires the worker in its stead." Labour brokering - Wikipedia, the free encyclopedia

Tayari imeshapigwa marufuku Namibia na huko kwa Madiba wanataka ipigwe marufuku.
 
Mimi sina tatizo na agencies kuchukua chao, mbona tushazoea hata madalali wa nyumba wanakuunganishia na kuchukua chao?

If this is a one time fee, sina tatizo, unawalipa gharama za uwakala wa kukuunganishia (ideally this should be done by the company you will work for).

Tatizo langu linakuja pale agency inapochukua sehemu ya hourly wages/ salary kama vile baada ya kukuunganisha wanafanya sehemu fulani ya kazi zako, wakati wamekaa tu wanakusanya chajuu. Fine, kama umeajiriwa na agency kuna habari za kodi zao na makato and all that, wanaweza kuwajibika kwa hayo, hususan kama umeandikishwa kama muajiriwa wao na sio wa unakofanya kazi (consultancy based assignments), lakini hata katika hayo, mfanyakazi awe na haki basi hata ya kuopata full disclosure.

Mazee, hiyo ya staffing agency kupata kiasilimia fulani kutoka kwenye wage mbona ni standard practice? Almost all of them do it.

Nimeshawahi kupokea temps kutoka Robert Half na mkataba wa makubaliano ya staffing uliweka bayana kwamba katika hourly wage ya temps wao watachukua kiasi fulani mpaka pale assignment itakapoisha au mpaka pale temps watakapoajiriwa. But in the meantime watakuwa ni waajiriwa wa Robert Half.

Kinacholipwa na anapofanya kazi ni kipi,

Sijui kwa Tanzania lakini kwa Marekani ukitaka kujua wao watu wa staffing agency wanachukua kiasi gani ni kiasi cha kuomba tu hizo taarifa na utapewa. Robert Half does that.

agency yake inamkata vipi kwa ajili ya health insurance na mafao etc, na yeye anacholipwa ni kipi.

Maelezo kama ya health insurance na other benefits mara nyingi huwa yapo kwenye employee handbooks na mi nazijua baadhi ya hizo agencies ambazo hutoa hizo benefits.

Sasa hivi unaona huyu Ng'wanakilala (is this Lulu?) kaulizwa kitu cha kwanza kusema ni ku cite confidentiality clauses.

I am all for the protection of a healthy business environment, I wrote a lenghty and balanced article at vijana.fm on the subject if I may say so myself,. But at some point workers fundamental rights must be protected.

I am all for the free market, but the free market without some obvious regulations is not good even for itself.

Kwa Tanzania huenda kabisa hiyo industry haiko regulated vizuri.
 
Lakini, hivi kuna mtu ambaye anapitia hizi staffing agencies halafu hajui kwamba kama wakikutafutia kazi, tuseme temp-to-hire, na wao wanakuwa wanapata cha kwao mpaka utapoajiriwa 'permanently' na huko walikokutafutia kazi?

I thought that was common knowledge but the specifics are the ones that were supposed to be confidential?

That's common knowledge.

What is not common knowledge is the percentage. Ukitaka kuulizia habari hizo tu unakuta kabla hata ya agency kuku interview ilikwisha kusainisha confidentiality clauses kwamba hutakiwi kujadili kule utakapofanya kazi watawalipa kiasi gani agency yako.

Watu wengi hufikiri kwamba tofauti ya wanacholipwa na agencies na agencies inacholipwa na kule wanakoishia kufanya kazi ni ndogo sana na inakuwa justified na gharama inazoingia agency (payroll, taxes, administration etc) lakini ukweli ni kwamba jamaa wanachukua hata zaidi ya 10 bucks an hour in some cases (US skilled workers).

10 bucks an hour that is a Walmart salary right there. Excuse me my Walmart crew.
 
Katika mambo machache niliyokubaliana na Papa mwenzangu Benedict XVI mojawapo lilikuwa hili la kupinga ajira zisizo za kudumu.

Watu wanashindwa kufanya mambo ya kudumu kwa sababu ajira zao zinaelea elea hewani.

Halafu, hii nchi inabidi tuelezane ukweli kwamba ujamaa ushazikwa.

I can almost hear mchonga on his Mbeya May day speech lamenting about the perils of the commoditization of labor.
 
That's common knowledge.

What is not common knowledge is the percentage. Ukitaka kuulizia habari hizo tu unakuta kabla hata ya agency kuku interview ilikwisha kusainisha confidentiality clauses kwamba hutakiwi kujadili kule utakapofanya kazi watawalipa kiasi gani agency yako.

Lakini hata kwa kawaida mambo ya salary mbona huwa ni confidential (at least on paper kwa sababu watu huwa wanaambizana anyway) katika sehemu nyingi tu.

Watu wengi hufikiri kwamba tofauti ya wanacholipwa na agencies na agencies inacholipwa na kule wanakoishia kufanya kazi ni ndogo sana na inakuwa justified na gharama inazoingia agency (payroll, taxes, administration etc) lakini ukweli ni kwamba jamaa wanachukua hata zaidi ya 10 bucks an hour in some cases.

Well ndo mambo ya free market economy na at-will employment hayo.
 
Mazee, hiyo ya staffing agency kupata kiasilimia fulani kutoka kwenye wage mbona ni standard practice? Almost all of them do it.

Nimeshawahi kupokea temps kutoka Robert Half na mkataba wa makubaliano ya staffing uliweka bayana kwamba katika hourly wage ya temps wao watachukua kiasi fulani mpaka pale assignment itakapoisha au mpaka pale temps watakapoajiriwa. But in the meantime watakuwa ni waajiriwa wa Robert Half.



Sijui kwa Tanzania lakini kwa Marekani ukitaka kujua wao watu wa staffing agency wanachukua kiasi gani ni kiasi cha kuomba tu hizo taarifa na utapewa. Robert Half does that.



Maelezo kama ya health insurance na other benefits mara nyingi huwa yapo kwenye employee handbooks na mi nazijua baadhi ya hizo agencies ambazo hutoa hizo benefits.



Kwa Tanzania huenda kabisa hiyo industry haiko regulated vizuri.

I have reason to believe that Robert Half being the leader that it has been for over half a century now, is operating far and beyond the "barely legal" standards used by the mushrooming mom and pops shops.

Kuna mama mmoja nusura apewe onyo na HR in one of these big global banks on Wall St, kisa aliwauliza consultants aliowaajiri yeye mwenyewe kwamba agencies zao zinawalipa kiasi gani.Turns out kumbe makubaliano kati ya HR ya bank na agency pamoja na makubaliano kati ya agency na consultants yalikuwa na confidentiality clause iliyokataza hawa consultants kujadili hili swali.

Marekani state laws pia zina complicate mambo, kwa hiyo mambo ya Gotham na kwa Atliens yanaweza kuwa si sawa.
 
Sidhani kama alimaanisha recruitment companies. Ila nafikiri alimaanisha outsourci ng companies. Yaani kampuni moja onachukua tender ya kufanya kazi flani kwenye kampuni nyingine. ile inayotoa tender inamlipa outsouced company hela nyingi na ile outsourced company inawalipa wafanyakazi ujira kidogo ili ibaki na faida.

Recruitment agents ni tofauti maana wao wanalipwa one time payment na mteja wao. Mara zote haiathiri mshahara wa mwajiriwa kwa sababu hakuna monthly payment.

Outsourcing ni trend ya kibiashara ambayo haiwezi kuondoka kwa maneno ya waziri. inaelekea waziri hajui inachokiongea kwa kuwa sera ya serikali ni kuoutsource non core activities. Na kazi kama ulinzi na usafi kwenye taasisi almost zote za serikali zimekuwa outsourced. Je ataanza kuwaajiri wote hao. Ni trend ya dunia nzima.

Is Erolink a Recruiting or Outsourcing agent?

Ukijibu hili, hukuwa na lazima ya kuandika maelezo yote hayo, kwani imetamkwa wazi wameiibia serikali about 3b.
 
Back
Top Bottom