Government Ban Job Recruitment Agencies!

Government Ban Job Recruitment Agencies!

Hili jambo linahitaji umakini sana. Kwanza, ni lazima kufafanua vizuri walengwa hasa ni kina nani. Nimeona hata ofisi nyingi tu za serikali au mashirika ya umma kwa sasa wana outsource baadhi ya kazi (mf: usafi, ulinzi, huduma za ndani, catering, madereva, etc). Sasa kama hoja ni kuwa kwa ku outsource huduma hizo wanaoajiriwa "wanapunjwa", then hata serikali na mashirika ya umma pia yatakumbwa na katazo hili?

Waziri anagusia pia mishahara, lakini anasahau kuwa kama ni kupunja serikali ndiyo inayoongoza - rejea malalamiko ya walimu, madakatari etc. Kwa hiyo pamoja na kuyabana makampuni ya kibinafsi, na serikali pia iangalie waajiriwa wake.

Jingine ni impacts za katazo hilo - kuna watu watapoteza ajira, kuna makampuni sasa itabidi "yafe" maana hayana biashara tena, baadhi ya kazi zinaweza kuwa exported kwenye nchi ambazo zina sharia nafuu (eg. makampuni ya simu yanaweza kuhamishia call centre zake Kenya, India etc), gharama za huduma/bidhaa zinaweza pia kupanda - mishahara na marupurupu mengine ni gharama ambazo mwisho wa siku zinakuwa factored in kwenye bei ya huduma/bidhaa husika. Au mishahara ya wafanyakazi waliopo inaweza kushuka ili kuongeza mishahara ya hao wengine ambao watatoka huko walipokuwa outsource na kuajiriwa moja kwa moja na kampuni husika.

Je makampuni ambayo yalikuwa yanafanya huduma hiyo yatakubaliana kirahisi na katazo hili. Kama ilikuwa biashara halali miaka mitano iliyopita, iweje leo inakuwa haramu (bila hata mabadiliko yoyote ya sheria)?

well said.

ndio hzo sheria zinazo lalamikiwa waziri akiamka anatoa maamuzi ambayo implications zake zinaathiri taifa
 
Kama ni kweli itakuwa hivo tunashukuru pale Spanco saizi inaitwa ison bpo mshahara 270000 take home 230000 .Mafao wanachelewesha kuna mfanyakazi kaacha kazi mwezi wa 11 mwaka jana hajapata mafao mpaka sasa. Kazi ya kupokea simu ni ngumu asikwambie mtu. Mtu unafanya kazi mwaka mmoja mafao hayafiki hata million moja. Kama hayo mabadiliko ni ya kweli mtakuwa mmetutoa shimoni sisi tulioajiriwa na outsourcing agency.

UOZO WA AIRTEL NA SPANCO HUU HAPA

Mimi ni mfanyakazi wa Airtel kwa mara ya kwanza leo hii najitokeza katika kipindi hiki nikiwa na kero kutoka katika kampuni ya SPANCO ambayo ni kampuni iliyochukua tenda ya kuajili wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja.

  • SPANCO ni kampuni ambayo inasemekana kuwa haitambuliki na wala haijaliwa na nikampuni ambayo inalipa wafanay kazi wake mshahara ambao ni wa chini kupindukia kwa wafanya kazi wake ambapo mfanayakazi wa SPANCO analipwa sh. 270000 kama mshahara wake wa mwezi na uo sio net mshara anaokuja kuchukua baada ya makato ni karibia 190000 huyo ni muhitimu wa chuo kikuu.
  • Achilia mbali kiwango cha pesa wanacholipwa wafanyakazi wake kumekuwa na manyanyaso mbalimbali kwa wafanyakazi ikiwemo kufanya kazi kwa mda mrefu na pia wafanyakazi wake wanafanya kazi kwa muda wa mwaka mpaka miaka mitatu wakiwa wapo under probation period yani wanakuwa hawana mkataba wa kudumu na mshahara wa wafanyakazi haupandi mpaka mwaka upite hata kama umepanda cheo.
  • Jamani kiukweli kabisa tunaumi mazingira ya kazi ni magumu mbaya na kazi ni nzito haswa kulinganishwa na kile tunacholipwa naomba wadau wa maswala ya wafanyakazi na wasajili wa makampuni aje kutusaidia katika hili maana hivi sasa imefikia hatua kuwa kila siku wanaajili watu sio chini ya arobaini na kuachisha watu kazi bila hata notice wala nini yani unakuja kazini na kukuta kuwa system imekuondoa wakati jana ulifanya kazi bila ya shida sa kinachoumiza ni kunyanyasika na watu baki toka nje ya nchi yetu inhali sisi tupo ndani ya nchi yetu.
  • Achilia mbali hayo yote mpaka hivi sasa ninavyoongea AIRTEL umekuwa mtandao wakususa sua hata huduma zao zimekaa kiwiziwizi tu kwa mfano wateja wanakatwa pesa ovyo ovyo bila ya kuzitumia na wanaunganishwa katika mahuduma mbali mbali kwa lazima na wakitaka kuijiondoa hawaondolewi yani kwa kifupi mtandao unaelekea kubaya.
  • Kama mtahitaji uthibitisho wa salary slip ya mfanyakazi mmoja na mjionee malipo yake yanavyokuwa mimi ntakuwa tayari kuikabidhisha yakwangu ili mjionee hali halisi yani mtu unaingia kazini sa kumin na dk 10 na kutoka ni sa 7 usiku mpaka uje fika nyumbani ni sa 9 au sa kumi alfajiri kesho tena hvy hvy wiki nzima na mshahara ndio kama huo je ni haki kweli?
  • Kwa habari ambazo zipo zimezagaa hawa watu wa SPANCO wanaishi hapa TANZANIA kinyume na sheria na pia hii kampuni yao ya SPANCO pia haijasajiliwa mishahara ya wafanyakazi kutoa mbinde mpaka watu wawatishie ndio wanatoa mishahara.
  • Wafanyakazi wanakatwa makato ya PPF na NSSF kwa mkupuo na achilia mbali hayao hizo pesa wala hawazipeleki popote yani mtu anakatwa makato kama ayo na wakati hata kitambulisho cha NSSF na PPF hauna na ambaye anacho hela hawamuingizii wala nini.

UOZO WA AIRTEL NA SPANCO HUU HAPA. - TEAM TZ
 
Halima Erolink kuja huku umuuguze mwenzio jamani hahahahahahaaa piole sana Mpwa wangu tujitahidi tuachane na biashara zakuajiriwa
 
Now utanunua friji. Jamani Halima rudi kwa barafu.

...........Halima Erolink
 
Last edited by a moderator:
safi sana mama kabaka wametutesa saana halafu recruitment agencies nyengine zinaendekeza udini na ukabila hazipo professional kwa mfano utakuta zinafavour watu wa dinin flani au kabilaflani hii haifai watanzania wote ni wamoja, kosa umekalia kiti wewe wa dini flani au kabila flani ,piga chiiiiiiniiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Pole sana,ila mimi naona tatizo ni serikali yenyewe maana ndo inawajibu wa kusimamia hizi kampuni,afu nikiangalia sana naona kama ni siasa tu,mbona hajazungumzia suala la pesa walizoiibia serikali watachukua hatua gani?tumeishazoea katika taifa hili wenye pesa sheria haichukui mkondo wake,na siajabu huyo waziri siku hizo zikifika akajisahaulisha
 
Saizi hao Spanco wanajiita ISON BPO. Wapo pia pale makao makuu ya Tigo ya zamani. Mtu unafanya kazi ya customer care kitambulisho kinaonyesha unafanya kazi ya operation.
 
  • Thanks
Reactions: OMJ
Je makampuni ambayo yalikuwa yanafanya huduma hiyo yatakubaliana kirahisi na katazo hili. Kama ilikuwa biashara halali miaka mitano iliyopita, iweje leo inakuwa haramu (bila hata mabadiliko yoyote ya sheria)?

Kwa mujibu wa Wizara, haikuwa biashara halali. Ukipitia taarifa ya Wizara hapo juu inasema kuwa Kwa mujibu wa Kifungu 4 cha Sheria ya Huduma za Ajira Na. 9 ya Mwaka 1999, majukumu ya msingi ya Wakala wa Huduma za Ajira ni kuwaandaa na kuwaunganisha Watafuta Kazi na Waajiri kwa kutoa mafunzo na ushauri elekezi kwa watafuta kazi, kutafuta fursa za ajira na kutoa taarifa za soko la ajira. Hivyo, Mawakala hawapaswi kuwa waajiri wa wafanyakazi waliowatafutia kazi kwa niaba ya Waajiri wengine.

Kama hii ndiyo sheria, how come those companies zilifanya biashara ambayo hauruhusiwi kwa muda wote huo? Halafu walipohojiwa na The Guardian mwaka jana
Tanzania Employment Service Agency (TaESA) confirmed that all outsourcing agencies were supposed to work in accordance with the country's labour laws and the directives of the International Labour Organisation (ILO), which implies that their businesses were legal provided that wangefuata sheria zote.
 
Hahahhahahaaa Halima-Erolink.ila kweli majamaa ni balaa.Big up sana serikali kwa kupiga marufuku hawa Recruitment agents maana dah! Hawana huruma hata kidogo.
 
Hakuna button ya UNLIKE mbona? Mods msaada pls...

Sijui hata kama umejua nilichoandika. Unasoma juu juu tuu. Completely lack of attention to details.

Katafute kwanza maana na tofauti kati ya "recruitment agency" na "recruitment process outsourcing."
 
biashara kwenye ajira za watu, ni zaidi ya udananda.
 
Mama asante naomba mikataba ambayo tayari ipo NA hizo agence isitishwe Mara moja
 
Back
Top Bottom