Government Ban Job Recruitment Agencies!

Government Ban Job Recruitment Agencies!

Kuban hizi recruitment agenciea serikali imekurupuka, kuna watu wanazitegemea sana, eengine wanafanya kazi ktk hizi agencies, wamejiajiri na zinalipa kodi kwa nchi, cha msingi ni kuzibana hizi agencies zifate sheria za ajira na kuacha kunyonya nguvu kazi ya nchi kweli graduate unamlipa 270,000/= na wewe unaingiza zaidi ya mara mbili huu ni unyonyaji
Umeshaambiwa Erolink wanadaiwa back taxes na serikali takriban 3 billion TZS
 
Nakubaliana na wewe kwenye hiyo point, lakini nchi nyingi hasa zilizoko ndani ya European Union zimetengeneza sheria to the effect that secrecy/confidential clauses za aina hiyo kwenye mikataba ya kazi are unenforceable. Kwa mfano, hiyo sheria ya EU imekuwa implemented in the United Kingdom through the Equality Act 2010.

According to section 77 of that Act, "A term of a person's work that purports to prevent or restrict the person (P) from disclosing or seeking to disclose information about the terms of P's work is unenforceable against P in so far as P makes or seeks to make a relevant pay disclosure."

It goes on to state that "A term of a person's work that purports to prevent or restrict the person (P) from seeking disclosure of information from a colleague about the terms of the colleague's work is unenforceable against P in so far as P seeks a relevant pay disclosure from the colleague; and “colleague” includes a former colleague in relation to the work in question."

Further, "A disclosure is a relevant pay disclosure if made for the purpose of enabling the person who makes it, or the person to whom it is made, to find out whether or to what extent there is, in relation to the work in question, a connection between pay and having (or not having) a particular protected characteristic.

Although this section does not outlaw secrecy/confidential clauses, it does make them unenforceable in certain circumstances.

I think the United States is moving in the same direction. See, for example, the First Circuit case of NLRB v. Northeastern Land Services (2011) in which it was held that "confidentiality clauses in employment contracts can constitute a per se violation of employees' protected employee rights under the National Labor Relations Act (NLRA) if the clauses can be read as prohibiting all discussions of wages, hours, and working conditions." Beware Of Broad Confidentiality Clauses In Employment Contracts—And The Expanding Application Of The National Labor Relations Act - Employment and HR - United States

Kwa huku kwetu, there is still a long way to go maana hata anayemwajiri Rais hajui anamlipa kiasi gani sembuse mwajiriwa kujua mshahara wa mwajiriwa mwenzake? Halafu kuna wale ambao wakiulizwa kwa mema tuu anajiboost kuwa analipwa mara tatu ya the actual salary ili ku-impress aliye mbele yake au ku-cover rushwa anazochukua.

Bado nina wasiwasi kama mleta mada ameiripoti hiyo habari kama ilivyotolewa. A blanket ban for all recruitment agencies? I don't think so.

Tunahitaji sheria kama hiyo ya EU, na publicity ya kuiandama ili iwe hai.
 
Erolink Tanzania General Manager Natasha Ng’wanakilala
Source: ippmedia

Inasemekana kuna watu waliokuwa wameajiriwa nao waliandika barua The Guardian ndo wakai-publicize.

When asked about payment discrepancies, Ms Ng’wanakilala declined to comment advising that payments were confidential under the contract agreement with the workers.

When asked about the discrepancies between the salaries of permanent and temporary staff at client companies, she advised that the policies were arranged by the client companies.

The Tanzania Employment Service Agency (TaESA) confirmed that all outsourcing agencies are supposed to work in accordance with the country’s labour laws and the directives of the International Labour Organisation (ILO).

- See more at: Tanzania – Recruitment agencies accused of exploitation
 
Sidhani kama njia muafaka ilikuwa ni kuzipiga marufuku hizo recruitment agencies, bali kuhakikisha kuwa zina-operate kwa mujibu wa sheria au taratibu zilizowekwa.

Ilichotakiwa kufanya serikali ni kulinda maslahi yake pamoja na haki za wale wanaojiriwa na kufanya kazi kupitia recruitment agencies.

Kama recruitment agencies haitafuata sheria au taratibu zilizowekwa, then kuwe na enforcement actions, following by huge fines. Lazima watatii tuu.

Lazima kuwe na restrictions and responsibilities on recruitment agencies na biashara zao, but siyo kuzipiga marufuku. Funga zile ambazo zimekataa kufuata sheria na taratibu tuu.

Kama hii habari ni kweli, then this is the worst decision for the government. Pia ni ushahidi kuwa serikali inashindwa ku-regulate the emerging businesses across the country.

Siamini kama recruitment agencies is a bad business for the country kiasi cha kuzipiga marufuku. What is bad is the failure of the government to regulate these agencies.

I think kilichopigwa marufuku siyo recruitment agencies bali ni recruitment process outsourcing. Kwa hiyo, agencies kama Radar Recruitment hawadhuriki na huu uamumzi.

Lakini kuna baadhi ya makampuni yanafanya both as recruitment agencies as well as recruitment process outsourcing. Kwa maana hiyo itabidi hizo kampuni ziachane na recruitment process outsourcing na kubakia kama recruitment agencies. Mfano: Erolink | Developing today's managers into tomorrow's leaders.

Hakuna button ya UNLIKE mbona? Mods msaada pls...
 
TAMKO LA SERIKALI KUHUSU KUSITISHA UTARATIBU WA KUKODISHA WAFANYAKAZI UNAOFANYWA NA BAADHI YA WAKALA BINAFSI WA HUDUMA ZA AJIRA

1. Wizara ya Kazi na Ajira imekua ikipokea malalamiko toka kwa wadau mbalimbali kuhusu utaratibu wa udalali wa kukodisha wafanyakazi katika makampuni unaofanywa na baadhi ya Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira nchini.

2. Wizara imefanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hili na kubaini kuwa utaratibu wa kukodisha wafanyakazi unaofanywa na baadhi ya Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira ni kinyume cha Sheria ya Huduma za Ajira Na. 9 ya Mwaka
1999 [Sura 243 kama ilivyorejewa Mwaka 2002]. Kwa mujibu wa Kifungu 4 cha Sheria hii, majukumu ya msingi ya Wakala wa Huduma za Ajira ni kuwaandaa na kuwaunganisha Watafuta Kazi na Waajiri kwa kutoa mafunzo na ushauri elekezi kwa watafuta kazi, kutafuta fursa za ajira na kutoa taarifa za soko la ajira. Hivyo, Mawakala hawapaswi kuwa waajiri wa wafanyakazi waliowatafutia kazi kwa niaba ya Waajiri wengine.

3. Aidha, uchunguzi umebaini kwamba utaratibu huu ni ujanja unaotumiwa na baadhi ya Waajiri na Mawakala kwa lengo la kukwepa kodi na kujipatia faida kwa kukwepa kutoa haki za msingi za wafanyakazi kwa mujibu wa Sheria za Kazi. Baadhi ya makampuni yanayokodisha wafanyakazi yamefanyiwa uhakiki na TRA na kubainika kukwepa kodi ya mapato ya ajira (PAYE) na na kodi ya mapato ya kampuni kinyume na Kifungu cha 7 cha Sheria ya Kodi ya Mapato ya Mwaka 2004 [Sura 332 kama ilivyorejewa Mwaka 2008].

4.Uchunguzi huu umebaini athari mbalimbali kwa wafanyakazi wanaoajiriwa kwa utaratibu huu. Athari hizo ni pamoja na:

Wafanyakazi kukosa haki ya hifadhi ya jamii kama vile likizo ya uzazi na matibabu kinyume na Sheria mbalimbali za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii;

Uwepo wa ubaguzi katika malipo ya mishahara kwa kazi ya aina moja kinyume na kifungu cha 7(10) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na.6 ya mwaka 2004 ambacho kinamtaka mwajiri kuchukua hatua stahiki kwa kuhakikisha kuwa wafanyakazi bila kujali jinsia zao wanalipwa mishahara linganifu na ya haki kwa kazi yenye uzito na thamani sawa;

Kukosa fursa za kujiendeleza kielimu na mafunzo;

Kukosekana kwa usalama na uhakika wa ajira ;

Wafanyakazi kulipwa mishahara ya kima cha chini kinyume na sekta wanayofanyia kazi.


5. Kwa taarifa hii, Wizara ya Kazi na Ajira imeamua kusitisha mara moja utaratibu wa Mawakala kuwaajiri wafanyakazi wanaowatafutia kazi. Aidha, Mawakala na Kampuni husika waliopo katika utaratibu huu kwa sasa wanapaswa kuwahamisha wafanyakazi waliokodishwa kutoka kwa Wakala kwenda kwa Kampuni husika. Waajiri na Wakala wanatakiwa kukamilisha zoezi hili ndani ya kipindi cha mwezi mmoja na kuwasilisha taarifa za utekelezaji kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi na Ajira kabla au ifikapo tarehe 28/02/2014.

6. Uchunguzi zaidi unaendelea kubaini kama kuna wafanyakazi wa Kigeni wanaohusishwa katika utaratibu wa kukodishwa ili hatua zinazotahili ziweze kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwataka waombe vibali vya ajira kwa mujibu wa Sheria ya Uhamiaji Na.7 ya mwaka 1995 na Sheria ya Huduma za Ajira Na.9 ya mwaka 1999. Wageni watakao kidhi vigezo wataajiriwa na kampuni walipokodishwa; ambazo kwa wakati huo zitakua ndiyo mwajiri wao.

7. Wizara ya Kazi na Ajira inawaelekeza Wakala wa Huduma za Ajira nchini kwamba, kwa utaratibu wa sasa watapaswa kuwasilisha barua za maombi ya usajili wa Uwakala kwa KAMISHNA WA KAZI kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Ajira Na. 9 ya mwaka 1999 [Sura 243 kama ilivyorejewa Mwaka 2002] ili waweze kufanya shughuli za Uwakala wa Huduma za Ajira kisheria. Maombi haya yawasilishwe ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tangu kutolewa kwa tangazo hili. Baada ya muda huo Wakala asiye na kibali cha Kamishna wa Kazi hatoruhusiwa kuendesha shuguli za huduma za ajira nchini. Aidha, Mawakala watakaopata leseni ya Kamishna wa Kazi yatakua yakitangazwa ili yatambuliwe na Umma.

8. Nasisitiza, maelekezo haya yatatolewa kwa Makampuni na Wakala waliohusishwa katika uchunguzi kwa ajili ya utekelezaji.


IMETOLEWA NA

GAUDENTIA MUGOSI KABAKA (MB)

WAZIRI WA KAZI NA AJIRA
27/01/2014
 
Kati ya maamuzi mazuri ambayo mama atakumbukwa kwa kuyafanya ni hili maana ndugu zetu wanafanya kazi ila nauli tunatoa sisi. Msimamo uwe pale pale!
 
Kama kuna kitu ambacho kimekuwa kikichefua moyo wangu, ni pamoja na hili la makampuni kuwaona wafanyakazi wao kama viraka tu! Nimekuwa nikijiuliza hawa recruters agences wanamilikije idadi kubwa ya wafanyakazi wakati ofisi zao zipo kwenye mikoba tu?! Na kwanini mfanyakazi wa kampuni unayofanyia kazi pindi upatwapo na tatizo, kampuni inakuambia kuwa wewe si mwajiriwa wetu bali wewe ni wa agent aliyekuleta! Hili lipo tanzania tu. Kwa tangazo hili la wafanyakazi kumilikiwa na kampuni wanazofanyia kazi ni la kupongezwa sana. Kama si matamshi ya kisiasa ngoja tusubiri matokeo ndani ya hizi cku 30.
 
Kuban hizi recruitment agenciea serikali imekurupuka, kuna watu wanazitegemea sana, eengine wanafanya kazi ktk hizi agencies, wamejiajiri na zinalipa kodi kwa nchi, cha msingi ni kuzibana hizi agencies zifate sheria za ajira na kuacha kunyonya nguvu kazi ya nchi kweli graduate unamlipa 270,000/= na wewe unaingiza zaidi ya mara mbili huu ni unyonyaji

Mkuu mbona hueleweki?
 
Kuna baadhi ya mambo yanaweza kuwa controllable lakini kuna mengine itakuwa ngumu tu hususani linapokuja suala la maslahi ya wafanyakazi. mambo kama michango ya NSSF na mengine kama hayo ni controllable lakini upunjaji wa maslahi itakuwa ngumu coz' hawa nao ni wafanyabiashara unless kama serikali i-intervene relationship kati ya employers and recruitment agencies. Nasema wa-intervene coz' wengi wao uhusiano uliopo ni kwamba employer anamlipa recruitment agency na recruitment agency ndie anajua anamlipa nini employee! So, ili waweze kutengeneza faida kubwa zaidi, wanalazimika kuwapunja wafanyakazi coz' kwa kadri wanavyowapunja zaidi ndivyo wanavyopata nyingi zaidi. Na employers huwa wanai-favor njia hii ili kujivua gharama za "other benefits" kv matibabu, likizo,n,k coz' hata kama mtu anafanya Tigo lakini anakuwa si mwajiriwa wa Tigo bali ni wa yule aliyemleta! Na kama ukizingua, employer wala hana haja ya kupoteza hata dakika moja kwako; anakurudisha tu waliokuleta na yeye ku-demand immediate replacement na legal problems zote zinakuwa kwa agent na sio kwa employer! Sasa huu uhusiano wa kuwa mfanyakazi anakuwa chini ya agent (in contrast na ile system kwamba employer anamlipa tu agent kumfanyia recruitment lakini mkataba anaingia mfanyakazi na employer) unam-favor sana employer wakati unamuumiza mfanyakazi! Na hata linapokuja suala la promotion sijui wanafanyaje manake ukienda kwenye kampuni yenye wafanyakazi wa aina mbili, kutoka kwa agent na wale employed na employer mwenyewe, basi kuna hatari favor wakawa wanapata wale wa employer mwenyewe coz' hawajibiki kwa huyu wa kuletwa!!

Kaka Uko smart HECKO
 
Nchi hii wafanyakazi ni slaves,si hao recruiters pekee hata serikali ni wanyonyaji namba moja wa wafanyakazi.
 
Hili jambo linahitaji umakini sana. Kwanza, ni lazima kufafanua vizuri walengwa hasa ni kina nani. Nimeona hata ofisi nyingi tu za serikali au mashirika ya umma kwa sasa wana outsource baadhi ya kazi (mf: usafi, ulinzi, huduma za ndani, catering, madereva, etc). Sasa kama hoja ni kuwa kwa ku outsource huduma hizo wanaoajiriwa "wanapunjwa", then hata serikali na mashirika ya umma pia yatakumbwa na katazo hili?

Waziri anagusia pia mishahara, lakini anasahau kuwa kama ni kupunja serikali ndiyo inayoongoza - rejea malalamiko ya walimu, madakatari etc. Kwa hiyo pamoja na kuyabana makampuni ya kibinafsi, na serikali pia iangalie waajiriwa wake.

Jingine ni impacts za katazo hilo - kuna watu watapoteza ajira, kuna makampuni sasa itabidi "yafe" maana hayana biashara tena, baadhi ya kazi zinaweza kuwa exported kwenye nchi ambazo zina sharia nafuu (eg. makampuni ya simu yanaweza kuhamishia call centre zake Kenya, India etc), gharama za huduma/bidhaa zinaweza pia kupanda - mishahara na marupurupu mengine ni gharama ambazo mwisho wa siku zinakuwa factored in kwenye bei ya huduma/bidhaa husika. Au mishahara ya wafanyakazi waliopo inaweza kushuka ili kuongeza mishahara ya hao wengine ambao watatoka huko walipokuwa outsource na kuajiriwa moja kwa moja na kampuni husika.

Je makampuni ambayo yalikuwa yanafanya huduma hiyo yatakubaliana kirahisi na katazo hili. Kama ilikuwa biashara halali miaka mitano iliyopita, iweje leo inakuwa haramu (bila hata mabadiliko yoyote ya sheria)?
 
Inasemekana kuna watu waliokuwa wameajiriwa nao waliandika barua The Guardian ndo wakai-publicize.

When asked about payment discrepancies, Ms Ng’wanakilala declined to comment advising that payments were confidential under the contract agreement with the workers.

When asked about the discrepancies between the salaries of permanent and temporary staff at client companies, she advised that the policies were arranged by the client companies.

The Tanzania Employment Service Agency (TaESA) confirmed that all outsourcing agencies are supposed to work in accordance with the country’s labour laws and the directives of the International Labour Organisation (ILO).

- See more at: Tanzania – Recruitment agencies accused of exploitation

I still thing government kma kawaida is taking simple solutions for mambo magumu.

Mimi am concerned hili la expatriates (ofcoz I mean wahindi coz ndo waliojaa)

kuna kampuni kibaooo hata uperform VP at the end of the day u will have an expatriate boss tena wengine goes further na kutafutia boss mweupe. yani promotion katka senior level mgt is purely racial based.

this one much worse than hawa wakina erolink. nenda Quality Group kwa Manji utafikiri upo Mumbai
 
Waje mtaani tuanze kutafuta nao kazi waone hali halisi.
Yaani hapa nafananisha, Askari magereza mwenye roho mbaya, nae kafanya kosa hafu kafungwa gereza ilo ilo, anakutana na wafungwa aliokua anawafitini.
 
Hawa jamaa wamenitesa sana...Mpaka nikatoswa na Demu wangu Halima,mana najulikana nafanya kazi,napata mshahara lkn hata demu wangu akija gheto hakuti mabadiliko,Room iko vilevile,tena chumba kimoja kapeti ya plastic...hakuna friji ya soda wala maji...nikinunua soda naweka kwa Mangi dukani ili zipate ubaridi,hii ilimuudhi sana Halima my sweet heart
Kamshahara hakatoshi hata kumtoa out...akija nikitoa nauli tu baasi ujue bajeti nzima inayumba.Kweli Erolink mmenitesa sana...nikaonekana ni mwanaume nisiye na mipango,sina malengo wala ujuzi wa kutumia kipato changu,Halima akanikimbia akijua mi si husband material,Asante Mama Gaudensia Mugosi Kabaka ni siku nyingi nilifunga na kuomba hawa Erolink wapate mkono wa sheria.
Nilijituma hadi overtime ili nimkumbuke Mama kule kijijini kwa vitenge na batiki,lkn hata hivyo vijihela vya overtime hivi ”vibepari“ uchwara vya Erolink vilinidhurumu...sikuwa na jinsi zaidi ya kupata hela ya kula na nauli ”from hand to mouth“,mshahara wangu haukuwahi kukutana,nakajiuliza au mimi sina nidhamu ya pesa??...Erolink umenitesa sana,ukanikimbizia Halima wangu,ukanikosanisha na masela kijiweni waliojua nawabania hela za stamp kutuma application kisa mie nina kazi kumbe laa..
Mpaka kesho mafao yangu ya NSSF sijawahi kuyapata sbb hawakuwa wanapeleka,baadae nikagundua kampuni iliyoniajili ilikuwa inanilipa laki nane na sitini,lkn ”wajanja“ Erolink walikuwa wananipa laki mbili na tisini.
Japo nilijinyofoa kwa kuchelewa lkn walininyonya sana na kusababisha kumpoteza Halima wangu,ufanyakazi wangu haukuwa na manufaa...kwangu hata May Mosi haikuwa na umuhimu...
Walinifanya nijikite katika ujasiliamali kuliko kiajiliwa...Nitakukumbuka Halima,kwenye simu yangu nimekusave ”Halima-Erolink“
 
Hahaaaaa Halimaaaaa rudi kwa mpenzi wako,mkoloni mnyonyaji kapigwa ngumi ya uso na kibanga Kabaka

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom