Government Ban Job Recruitment Agencies!

Government Ban Job Recruitment Agencies!

Kwa mujibu wa Waziri wa kazi na Ajira, sio kwamba hizi Recruitment Agency zimefungiwa zisifanye kazi, Recruitment agency zote hapa nchini zinafanya kazi kwa muji wa Sheria ya Huduma za Ajira Na. 9 ya Mwaka 1999 amabyo pia ilifanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Kama alivyo ainisha waziri, "Sheria ya Huduma za Ajira Na. 9 ya Mwaka 1999 [Sura 243 kama ilivyorejewa Mwaka 2002]. Kwa mujibu wa Kifungu 4 cha Sheria hii,
majukumu ya msingi ya Wakala wa Huduma za Ajira ni kuwaandaa na kuwaunganisha Watafuta Kazi na Waajiri kwa kutoa mafunzo na ushauri elekezi kwa watafuta kazi, kutafuta fursa za ajira na kutoa taarifa za soko la ajira. Hivyo, Mawakala hawapaswi kuwa waajiri wa wafanyakazi waliowatafutia kazi kwa niaba ya Waajiri wengine.

kama nilivyo ainisha kwa alama nyekundu hapo juu, Recruitment agency nyingi zinakiuka utaratibu huu na kufanya wao kuwa waajiri wakati kisheria wao na waunganishi kati ya mwajiri na watafuta kazi.
Mfano ni: Baadhi ya Bank teller wa National Bank of Commerce(NBC) na Vodacom Customer Care ambao wapo chini ya ERONLINK wao si waajiriwa wa NBC wala Vodacom, bali wao wameajiriwa na Eronlink. Hii ndio kitu waziri wa kazi anataka iachwe mara moja na kuifungia kabisa isifanyike tena.

Wafanya kazi waliopo katika mfumo huu wananyimwa haki zao za msingi na kufanya utaratibu huu kuwa ni mbaya na nikinyume na sheria ya Huduma za Ajira
.
 
Elly B sijaelewa tangazo hili vizuri. Mfano kampuni ya audit firm ikiombwa kupeleka staff wake kufanya kazi kwa mteja say "three months" hii itahitaji kibali cha commissioner? au nikiwakubalia wahitimu wasio na ujuzi kufanya kazi kwangu kwa kujitolea wakati wanatafuta kazi hii nayo itahitaji kibali? Kwa kiasi fulani Waziri amekurupuka kuna makampuni ambayo hayawezi kuajiri watu wa sekta zote mfano migodini ..canteen, dispensary, blusting, na ulinzi lazima wafuate mfumo huu wa kuajiri kampuni itoe wafanyakazi


Ni kweli sheria ina upungufu mkubwa sehemu flani. hasa pale ambapo kuna makampuni yamejisajili kama makampuni ya kutoa huduma. Sasa ukute leseni ni za huduma say ya Ulinzi na huduma nyinginezo! Hapo kuna shida kubwa.

Lakini say kwa migodini kinachofanyika ni Makampuni kuomba tenda kama za kusupply chakula. and so wanakuwa halali kuwaajiri wenyewe.

Kimsingi italeta mkanganyiko.
 
Kwa kweli huduma zao ni nzuri maana huwa zinawaunganisha watu na sehemu za ajira. Sasa kwa Tanzania karibu kila kitu ni balaa. Hakuna nafuu popote pale.



Kwani hao jamaa wa bongo wao wanatoa huduma gani sasa hivi? Wana temp-to-hire services? Hicho unachopendekeza wewe si kizuri kwa mtazamo wangu kwa sababu kitaibania sana hiyo sekta na itayanyima makampuni fursa ya kumtathmini mtu kwenye utendaji wake wa kazi.

Kwa sababu kuna makampuni mengine huwa yanatumia hao mawakala katika kutafuta prospective employees. Mtu anaajiriwa kwanza na wakala (na mshahara anakuwa analipwa na wakala) halafu wakala kulingana na sifa za mtu ndo anatoa assignment kwamba fulani atapangiwa sehemu fulani na kadhalika.

Huko unakoenda kufanya kazi waweza kukuta baada ya kipindi fulani (tuseme miezi miwili au mitatu) kulingana na utendaji wako wa kazi unaweza kuajiriwa na hivyo kuwa mwajiriwa wa kampuni ambayo ulipelekwa kufanya assignment na hiyo temp agency.

Kwa hiyo ni kama namna fulani ya kuchuja waajiriwa watarajiwa kuliko kuajiri tu mtu moja kwa moja bila kujua hata utendaji wake wa kazi kiuhalisia ukoje.
Mkuu Nyani Ngabu,
Uliyoyaleleza wewe yanafaa sana kwenye honest community lakini sio hii ya kwetu! Kwanza, be informed kwamba wafuasi wakubwa wa hizi recruitment agencies ni kampuni za simu; wale wale wanaotuhumiwa kutolipa kodi! As we all know, dishonest community can not pay tax willingly! Sasa basi, hiyo hoja yako kwamba baada ya kupelekwa kwa employer na agent, after two or three months of your successful performance employer anaweza kukuajiri moja kwa moja; hiyo chance ni ndogo sana coz' wanatumia recruitment agencies si kwa ajili ya kukwepa recruitment headaches bali wanafanya hivyo kwa ajili ya kukwepa gharama! Wanafahamu ukishakuwa chini ya agent, yeye hatawajibika kwako na mambo kama usafiri, medical expenses and the like...sana sana, ukimzingua, anakurudisha kwa agent on the spot na yeye ku-demand replacement instantly!

Lakini kwa upande mwingine, tukumbuke kwamba mishahara TZ ni midogo sana! Sasa, let's say employer X alikuwa anamlipa Customer Care Agent Sh.500K, wala si kwamba akianza kutumia Agent atampa Agent 800K ili asiathiri ile 500K, la hasha, in most cases, atatoa ile ile na labda juu kidogo! Matokeo yake kale ka 500K inabidi mfanyakazi agawane na Agent! Na huyu Agent anafanya biashara, whose main goal is to maximize profit. One of the technique to maximize profit is to minimize cost...kwa Agent, mfanyakazi ni Cost; kwahiyo kadri anavyomminya, ndivyo yeye anavyopata faida kubwa zaidi! Matokeo yake ndo unakuta Customer Care aliyeajiriwa na Voda wenyewe analipwa (say) sh. 800,00/- wakati yule aliyeletwa na Agent analipwa sh.400,000/-!

Lakini endapo Recruitment Agencies watabaki ku-recruit tu na contract ikawa kati ya mwajiri na mfanyakazi, haya mambo hayatakuwapo! Kwanza, unnecessary termination zitapungua coz' legal issues in case mfanyakazi anafungua mashitaka, zitawaangukia wao wakati kwa sasa, any legal problem ni burden ya Agent, as a result employer huwa ajali! Vilevile hata suala la promotion ni rahisi, coz' you're working for that employer na ni yeye ndie aliye responsible kwako in case of promotion! When you're working under Agent, kama unataka kudai hiyo promotion, basi nenda kamdai huyo aliyekuleta!

Hapa mimi nimezungumzia upande wa mwajiriwa; hayo ya PAYE watajuana wenyewe na serikali yao!
 
Last edited by a moderator:

kama nilivyo ainisha kwa alama nyekundu hapo juu, Recruitment agency nyingi zinakiuka utaratibu huu na kufanya wao kuwa waajiri wakati kisheria wao na waunganishi kati ya mwajiri na watafuta kazi.
Mfano ni: Baadhi ya Bank teller wa National Bank of Commerce(NBC) na Vodacom Customer Care ambao wapo chini ya ERONLINK wao si waajiriwa wa NBC wala Vodacom, bali wao wameajiriwa na Eronlink. Hii ndio kitu waziri wa kazi anataka iachwe mara moja na kuifungia kabisa isifanyike tena.

Wafanya kazi waliopo katika mfumo huu wananyimwa haki zao za msingi na kufanya utaratibu huu kuwa ni mbaya na nikinyume na sheria ya Huduma za Ajira
.
Mkuu umemuelewa Waziri kwa 100%, huo ndio msingi wa usitishaji huu! Kampuni nyingi za uwakala zinakiuka hicho kipengele; to mention few ni pamoja na Erolink, Infinity Communication, Spanco, NFT Consultant...hawa wote, unaingia nao wao mkataba na kugeuka kuwa waajiri badala ya recruitment agency huku wakipanga benefit ipi na ipi wampe mwajiriwa na ipi wasimpe!
 
Mh Waziri wa Kazi mama G. Kabaka ameongeza muda wa hizi kampuni uchwara ku comply na Matakwa ya serikali mpaka mwisho wa mwezi huu. Je Erolink na kukwepa kwao kodi wataadhibiwa? Tunasiki Evis kakimbia sijui kweli?
 
Mbona kimya mama Gaudensia vijana tilioajiriwa na hizi recruitment agency tunaumia sana mtuonee huruma mawaziri wetu.
 
Mfano hai ni hawa LENJENTZ wako huru kabisa na wanajitangaza humu jukwaani.
 
Last edited by a moderator:
Serikali hebu mtimize kile mlicho tuahidi maana sasa hivi hatuna tena matumaini wala hatuoni ukomo wa hayo makampuni...
 
Back
Top Bottom