Government Ban Job Recruitment Agencies!

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,168
8,142
Wadau, serikali imepiga marufuku mawakala wa ajira baada ya watu kulalamika! What do you say? Pamoja na mambo mengine, wadau wamelalamikia tabia ya kampuni hizi kutopeleka makato ya mifuko ya jamii.

MY TAKE: Nadhani hili jambo limechelewa manake nasikia baadhi ya kampuni za uajiri ni full dhuruma. Mathalani, nasikia SPANCO, wanalipa mshahara wa sh. 270,000/ kwa customer care. Kuna wengine viwango vyao vya mishahara wala hawaangalii qualification a muhusika; provided watu wana shida ya ajira, wanajua watu watachukua chochote wapewacho.
  • 28 January 2014


TAMKO LA SERIKALI KUHUSU KUSITISHA UTARATIBU WA KUKODISHA WAFANYAKAZI UNAOFANYWA NA BAADHI YA WAKALA BINAFSI WA HUDUMA ZA AJIRA

1. Wizara ya Kazi na Ajira imekua ikipokea malalamiko toka kwa wadau mbalimbali kuhusu utaratibu wa udalali wa kukodisha wafanyakazi katika makampuni unaofanywa na baadhi ya Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira nchini.


2. Wizara imefanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hili na kubaini kuwa utaratibu wa kukodisha wafanyakazi unaofanywa na baadhi ya Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira ni kinyume cha Sheria ya Huduma za Ajira Na. 9 ya Mwaka 1999 [Sura 243 kama ilivyorejewa Mwaka 2002]. Kwa mujibu wa Kifungu 4 cha Sheria hii, majukumu ya msingi ya Wakala wa Huduma za Ajira ni kuwaandaa na kuwaunganisha Watafuta Kazi na Waajiri kwa kutoa mafunzo na ushauri elekezi kwa watafuta kazi, kutafuta fursa za ajira na kutoa taarifa za soko la ajira. Hivyo, Mawakala hawapaswi kuwa waajiri wa wafanyakazi waliowatafutia kazi kwa niaba ya Waajiri wengine.


3. Aidha, uchunguzi umebaini kwamba utaratibu huu ni ujanja unaotumiwa na baadhi ya Waajiri na Mawakala kwa lengo la kukwepa kodi na kujipatia faida kwa kukwepa kutoa haki za msingi za wafanyakazi kwa mujibu wa Sheria za Kazi. Baadhi ya makampuni yanayokodisha wafanyakazi yamefanyiwa uhakiki na TRA na kubainika kukwepa kodi ya mapato ya ajira (PAYE) na na kodi ya mapato ya kampuni kinyume na Kifungu cha 7 cha Sheria ya Kodi ya Mapato ya Mwaka 2004 [Sura 332 kama ilivyorejewa Mwaka 2008].


4.Uchunguzi huu umebaini athari mbalimbali kwa wafanyakazi wanaoajiriwa kwa utaratibu huu. Athari hizo ni pamoja na:


-Wafanyakazi kukosa haki ya hifadhi ya jamii kama vile likizo ya uzazi na matibabu kinyume na Sheria mbalimbali za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii;


-Uwepo wa ubaguzi katika malipo ya mishahara kwa kazi ya aina moja kinyume na kifungu cha 7(10) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na.6 ya mwaka 2004 ambacho kinamtaka mwajiri kuchukua hatua stahiki kwa kuhakikisha kuwa wafanyakazi bila kujali jinsia zao wanalipwa mishahara linganifu na ya haki kwa kazi yenye uzito na thamani sawa;


-Kukosa fursa za kujiendeleza kielimu na mafunzo;


-Kukosekana kwa usalama na uhakika wa ajira ;


-Wafanyakazi kulipwa mishahara ya kima cha chini kinyume na sekta wanayofanyia kazi.


5. Kwa taarifa hii, Wizara ya Kazi na Ajira imeamua kusitisha mara moja utaratibu wa Mawakala kuwaajiri wafanyakazi wanaowatafutia kazi. Aidha, Mawakala na Kampuni husika waliopo katika utaratibu huu kwa sasa wanapaswa kuwahamisha wafanyakazi waliokodishwa kutoka kwa Wakala kwenda kwa Kampuni husika. Waajiri na Wakala wanatakiwa kukamilisha zoezi hili ndani ya kipindi cha mwezi mmoja na kuwasilisha taarifa za utekelezaji kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi na Ajira kabla au ifikapo tarehe 28/02/2014.


6. Uchunguzi zaidi unaendelea kubaini kama kuna wafanyakazi wa Kigeni wanaohusishwa katika utaratibu wa kukodishwa ili hatua zinazotahili ziweze kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwataka waombe vibali vya ajira kwa mujibu wa Sheria ya Uhamiaji Na.7 ya mwaka 1995 na Sheria ya Huduma za Ajira Na.9 ya mwaka 1999. Wageni watakao kidhi vigezo wataajiriwa na kampuni walipokodishwa; ambazo kwa wakati huo zitakua ndiyo mwajiri wao.


7. Wizara ya Kazi na Ajira inawaelekeza Wakala wa Huduma za Ajira nchini kwamba, kwa utaratibu wa sasa watapaswa kuwasilisha barua za maombi ya usajili wa Uwakala kwa KAMISHNA WA KAZI kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Ajira Na. 9 ya mwaka 1999 [Sura 243 kama ilivyorejewa Mwaka 2002] ili waweze kufanya shughuli za Uwakala wa Huduma za Ajira kisheria. Maombi haya yawasilishwe ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tangu kutolewa kwa tangazo hili. Baada ya muda huo Wakala asiye na kibali cha Kamishna wa Kazi hatoruhusiwa kuendesha shuguli za huduma za ajira nchini. Aidha, Mawakala watakaopata leseni ya Kamishna wa Kazi yatakua yakitangazwa ili yatambuliwe na Umma.


8. Nasisitiza, maelekezo haya yatatolewa kwa Makampuni na Wakala waliohusishwa katika uchunguzi kwa ajili ya utekelezaji.


IMETOLEWA NA

GAUDENTIA MUGOSI KABAKA (MB)
WAZIRI WA KAZI NA AJIRA
27/01/2014


 
Wadau ktk taarifa ya TBC1 Hivi punde,Waziri wa kazi bi Gaudensia Kabaka atangaza kusitisha kazi za hizi recruitment agent,safi sana sana sana Mama,sababu ni zinakosesha waajiriwa kukosa haki zao kama hifadhi za jamii,mafuzo kazini,mafao ya elimu,uzazi,mikataba mifupi na makato yasiyo kuwa na tija,yaani ni unyanyasaji tu,na mengine utakayoyaona......
Safi sana sana Wizara ya kazi...Now hata Urasimu hawa jamaa huchangia sana sana.Ni kilio cha Muda Mrefu cha Vijana.
Pia ni kinyume cha sheria ya ajira.....
Really tumefurahi sana sana.....Hongera sana sana Waziri KABAKA.
 
Hata mm nashukuru kwa kuna recruitment agency moja nilifanya nao kazi walikuwa wanalipa madereva shs 270000,baada ya miezi mitatu wakawapandishia mpaka mia 4 kumbe ndo ilikuwa their actual figure ya salary yao wanauzi sana
 
OK asante kaka kwa taarifa... Ila mm sioni umuhimu wa kufunguwa, sometimes wanasaidia sana kutafutia kazi vijana, badhii yao ndio wapo whuni ila agencies zingine wko safi sana
 
Wadau, serikali imepiga marufuku mawakala wa ajira baada ya watu kulalamika! What do you say? Pamoja na mambo mengine, wadau wamelalamikia tabia ya kampuni hizi kutopeleka makato ya mifuko ya jamii.

MY TAKE: Nadhani hili jambo limechelewa manake nasikia baadhi ya kampuni za uajiri ni full dhuruma. Mathalani, nasikia SPANCO, wanalipa mshahara wa sh. 270,000/ kwa customer care. Kuna wengine viwango vyao vya mishahara wala hawaangalii qualification a muhusika; provided watu wana shida ya ajira, wanajua watu watachukua chochote wapewacho.

Sidhani kama njia muafaka ilikuwa ni kuzipiga marufuku hizo recruitment agencies, bali kuhakikisha kuwa zina-operate kwa mujibu wa sheria au taratibu zilizowekwa.

Ilichotakiwa kufanya serikali ni kulinda maslahi yake pamoja na haki za wale wanaojiriwa na kufanya kazi kupitia recruitment agencies.

Kama recruitment agencies haitafuata sheria au taratibu zilizowekwa, then kuwe na enforcement actions, following by huge fines. Lazima watatii tuu.

Lazima kuwe na restrictions and responsibilities on recruitment agencies na biashara zao, but siyo kuzipiga marufuku. Funga zile ambazo zimekataa kufuata sheria na taratibu tuu.

Kama hii habari ni kweli na imeripotiwa bila kupindishwa, then this is the worst decision for the government. Pia ni ushahidi kuwa serikali inashindwa ku-regulate the emerging businesses across the country.

Siamini kama recruitment agencies is a bad business for the country kiasi cha kuzipiga marufuku. What is bad is the failure of the government to regulate these agencies.

I think kilichopigwa marufuku siyo recruitment agencies bali ni recruitment process outsourcing. Kwa hiyo, agencies kama Radar Recruitment hawadhuriki na huu uamumzi.

Lakini kuna baadhi ya makampuni yanafanya both as recruitment agencies as well as recruitment process outsourcing. Kwa maana hiyo itabidi hizo kampuni ziachane na recruitment process outsourcing na kubakia kama recruitment agencies. Mfano: Erolink | Developing today's managers into tomorrow's leaders.
 
kuna tatizo kwenye sera zetu, wamezifungia huku lakini zitaendeleza kazi zake kwa mlango wa nyuma, serikali iziruhusu ila iweke utaratibu unaoeleweka na wenye tija kwa taifa kama vile kukusanya kodi n.k
 
Sidhani kama njia muafaka ilikuwa ni kuzipiga marufuku hizo recruitment agencies, bali kuhakikisha kuwa zina-operate kwa mujibu wa sheria au taratibu zilizowekwa.

Ilichotakiwa kufanya serikali ni kulinda maslahi yake pamoja na haki za wale wanaojiriwa na kufanya kazi kupitia recruitment agencies.

Kama recruitment agencies haitafuata sheria au taratibu zilizowekwa, then kuwe na enforcement actions, following by huge fines. Lazima watatii tuu.

Lazima kuwe na restrictions and responsibilities on recruitment agencies na biashara zao, but siyo kuzipiga marufuku. Funga zile ambazo zimekataa kufuata sheria na taratibu tuu.

Kama hii habari ni kweli, then this is the worst decision for the government. Pia ni ushahidi kuwa serikali inashindwa ku-regulate the emerging businesses across the country.

Siamini kama recruitment agencies is a bad business for the country kiasi cha kuzipiga marufuku. What is bad is the failure of the government to regulate these agencies.

Sahihi kabisa
 
Back
Top Bottom