Google waja na mpinzani wa WhatsApp

Google waja na mpinzani wa WhatsApp

Wanatuletea kitu kipia tena. Sisi kazi yetu kutumia tu,ngoja nikakariri Apartheid policy in South Africa.
 
Link ya app kwa anaye hitaji hii hapa

Google Allo 1.0.006_RC18 APK Download by Google Inc. - APKMirror


Kama unahitaji msaada version ipi ya kuinstall niambie tu aina ya simu yako na nitakushauri version ya kupakua..

Kwa kifupi app ni nzuri nimeichezea Jana lakini haina mzuka kivile pia haina end to end encryption kama whatsapp (hadi utumie incognito chat) anyway kwa sasa nimedelete Facebook messenger na whatsapp zinanitosha.. Na feature yao ya Google assistant inasaidia wamarekani kibongo bongo haina maana.
 
Tuende mbele turudi nyuma... Kama si kukosa promo... Hakuna kama BBM ktk ukanda huu wa chating... Chunguza
 
usiandike sentesi moja neno google na security, kama unafikiri google atakutunzia data zako kiusalama bila kukuchunguza karibu internet.

google ndio kampuni kubwa kushinda facebook kwenye matangazo, hivyo anahitaji hizo data zako zaidi kushinda fb,
 
IMG
 
kampuni ya Google Jana ilizindua messaging app mpya inayoitwa. allo itakayokuwa ikitumia namba za simu kama mtandao wa watsapp allo imetofautiana kidogo na whatsapp kwani inakupa vitu vingi katika kureply SMS. je Google wataweza kufua dafu au ndo watakuwa kama telegram... tusubiri

Sio rahisi sana lakini yes tusubiri...Google ina rekodi Ya kushindwa kutengeneza app ndogo za kuwezesha mazungumzo kama Whatsapp, viber,line na telegram hivi...walikua na Google plus, hangouts..n.k zote zilishindwa japo zilikuwepo muda kiasi..Mwaka jana wamefunga app yao nyingine Ya Picasa...ila kwenye search engine ni balaa, hasa kupitia Google.com na YouTube.
 
Wasichoelewa Ni kuwa hawa watsup,Google,fb nyuma ya pazia wote Ni kitu kimoja NASA na mwisho wa siku info zenu zote zitaenda kwa hao wanaozihitaji so hakuna PA kukimbilia
 
Wamekuletea na Duo......video calling yaani ni shwar mbayaaaa
Hii Duo naikubali, iko vzr sana kuliko hata Skype!
Hata nikiwa safari, huwa nawasiliana na Mke wangu kwa raha zote, huku HALOTEL ikifanikisha mawasiliano yangu Muruaaaa kabisa.
 
Wasichoelewa Ni kuwa hawa watsup,Google,fb nyuma ya pazia wote Ni kitu kimoja NASA na mwisho wa siku info zenu zote zitaenda kwa hao wanaozihitaji so hakuna PA kukimbilia
Ni NSA mkuu sio NASA,

NASA ni wale wanaorusha vyombo angani vinavyoenda mwezini au mars
 
naona kweye app store wameandika Google Allo coming soon😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀
 
Pia watakuja na smartphone zao za "Google pixel" hawa jamaa wameamua kuingia wenyewe kwenye hardware baada ya kuwapigia debe Samsung kwa muda mrefu

Sent from mTalk
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Tuende mbele turudi nyuma... Kama si kukosa promo... Hakuna kama BBM ktk ukanda huu wa chating... Chunguza
Yahoo marketing department yao haipo vizuri kwa kweli, searching engine yao ya yahoo wameishindwa, blackberry imewashinda, bbm pia, yahoomail.... waiuze tu yahoo
 
Wasichoelewa Ni kuwa hawa watsup,Google,fb nyuma ya pazia wote Ni kitu kimoja NASA na mwisho wa siku info zenu zote zitaenda kwa hao wanaozihitaji so hakuna PA kukimbilia
Mkuu NASA imeingiaje hapo,au wanataka kutupeleka mars, ingekuwa NSA ningekuelewa kidogo
 
Back
Top Bottom