ngebo
JF-Expert Member
- Sep 8, 2017
- 1,684
- 2,133
- Thread starter
- #181
eh mkuu yani bongo tamaa nyingi sana mtu anataka akiuza kitu auze mara mbili ya bei ndio hapo anaona amewini biashara, tena sana sana hawa wanaouza vitu kutoka china, kisa basi kaenda china anakuja kukulalia kwa kuuza kwa faida ya 100% , angalau angechukua 40% ya bei ndo iwe faida
Siku moja natafta s10+ kuna duka liko Viva Tower wakawa hawana s10+ ila ipo s10 ya kawaida wakaniambia bei 2.9m, nilishangaa sana. Watanzania tamaa ndio inasababisha biashara haziendelei, kutaka faida kubwa kupita kiasi.
Juzi moja nikaenda dukani kutafta raba simpe za kuvaa, mtandaoni wanauza 30k hadi 35k, wanaziita za Uganda, nikasema kabla sijaagiza mtu alete ngoja niende hapa duka la jirani, jamaa ananiambia 85k, nikamuonyesha mtandaoni wanauzaje, akaanza kusema kila mtu ana biashara yake, nikamwambia ukiendelea hivi hata hili duka utauza na litakufa.
Nenda tigo shop ulizia s10+ utaambiwa 2.6m, unajiuliza wao wanazinunua wapi? Note 10+ 3.1m. Bei unayonunua simu Bongo ukiagiza nje unapata kwa nusu yake.