Google pixel na kamera kali

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
Simu ya Google pixel 8 series imekuja ikiwa na uwezo wa kutoa picha Kali zenye mvuto ndani yake yaani unaweza sema uko mwezini.

Achana na kamera ya 50mp iliyopo ndani, kuna Teknolojia ya Akili bandia ndani ya kamera unaijua Lakini.

Kwenye upande wa video ina feature ya kuchukua video Kwenye mazingira ya kiza Yani unarekodi video Kwenye kiza kinene basi google pixel inatoa kama mchana vile.

Kuna feature nyingine ya uwezo wa kuediti picha yaani ikiwa umepiga picha unahitaji kuondoa kitu Kwenye picha au kukihamisha mahali Fulani basi google pixel 8 series imekuja na hiyo feature.

googlekamera%20%E2%80%93%201.jpg

Google pixel 8 Series pia ukiwa nayo utaweza kupokea Update ya software miaka 7 kuanzia Leo maana yake toleo la mwisho kupokea Update ni mwaka 2030.
 
Kawaida ya simu za Pixel huwa zinakuwa rated kwa mbwembwe nyingi mtandaoni, nilikuja kugundua ni kwanini. Samsung huwa zinakuwa na tetesi nyingi kabla hazijawa released.

Ukija kwenye uhalisia, kaa miezi sita halafu tafuta resale za flagships kwenye website za nje za kuuza simu used utakuta Pixel inaongoza na imeporomoka bei.

iPhone 15 sioni kama itafanya vizuri sana ila kutegemea Pixel 8 iizidi Samsung S24 inayokuwa released February mwakani sahau.

Ukienda kwenye benchmarks unakuta iPhone zinakuwa na marks za juu kidogo na hilo halifichiki kwenye matumizi.
 
Kawaida ya simu za Pixel huwa zinakuwa rated kwa mbwembwe nyingi mtandaoni, nilikuja kugundua ni kwanini. Samsung huwa zinakuwa na tetesi nyingi kabla hazijawa released.

Ukija kwenye uhalisia, kaa miezi sita alafu tafuta resale za flagships kwenye website za nje za kuuza simu used utakuta Pixel inaongoza na imeporomoka bei.

iPhone 15 sioni kama itafanya vizuri sana ila kutegemea Pixel 8 iizidi Samsung S24 inayokuwa released February mwakani sahau.

Ukienda kwenye benchmarks unakuta iPhone zinakuwa na marks za juu kidogo na hilo halifichiki kwenye matumizi.
Samsung bado ni unbeaten...

Hao Pixel ukitoa part ya camera, kwingineko ni majanga tuu...

The most user friendly phone ni Samsung tuu..
 
Nani amekwambia pixel sio camera hata performance ipo vizuri kuanzia ukaaji wa chaji,processer,music na vingine ni vile Tu mnanunuaga refurbished phones za makumbusho
Kwenye upande wa ukaaji wa chaji nadhani inategemea na uwezo wa betri kabla ya kujua umenuna Makumbusho.

Mfano mimi natumia pixel 4a 5G betri yake n 3800+ ambayo kwa kawaida kama unatumia simu sana basi haikutoshi, mwanzo nilikuwa natumia Tecno ina 5000 uwezo wa betri na sikuwahi kutembea na chaji.
 
Kwenye upande wa ukaaji wa chaji nadhan inategemea na uwezo wa betri kabla ya kujua umenuna makumbusho.

Mfano mm natumia pixel 4a 5G betri yake n 3800+ ambayo kwa kawaida kama unatumia simu sana bc haikutoshi, mwanzo nlkuwa natumia Tecno ina 5000 uwezo wa betri na sikuwahi kutembea na chaji.
Sasa Pixel 4a 5G ina Qualcomm Snapdragon 765G tena ni Mid-range Gaming processor afu unalinganishaje na Tecno yenye MTK Chip ambayo perfomance yake ni ndogo na hata ulaji wa chaji ni mdogo..
 
Nyie pigeni majungu ila Pixel ndio Simu

Kasoro ndogondogo kama chaji haiwezi kuwa kigezo cha kui undermine kwasababu tunatofautiana matumizi.

Hizo simu zenye 5000mAh nazo hazikupi guarantee ya kukaa na chaji kwa muda mrefu ikiwa simu hiyo itakuwa on display kwa muda.

Na hata Samsung zenyewe zenye kukaa na chaji zimeanza kutolewa juzi juzi tu hapo kwenye series ya A

Angalia flagship ya 2019 S10 alitoa ikiwa na battery ya 3400mAh.

Lakini mwaka huohuo Pixel alitoa naye flagship yake ya 4XL iliyokuwa na battery ya 3700mAh kubwa kuzidi Samsung. Lakini ukiangalia miaka hiyo wadau na wapenzi wa Samsung hawakuweza kutumia hoja ya battery kuonesha kwanini ni bora kuliko Pixel
 
Nani amekwambia pixel sio camera hata performance ipo vizuri kuanzia ukaaji wa chaji,processer,music na vingine ni vile Tu mnanunuaga refurbished phones za makumbusho
Tuanze kimojakimoja ulichotaja.
1. Battery na chaji. Pixel gani inakaa na chaji? Achana na za nyuma, Pixel 6 Pro ni 5000mAh ila fast charging yake ni ya kiwendawazimu, kwa 30W charger unapata almost 50% kwa 30 mins, speed ya kawaida kabisa. Ila ukija kuijaza simu unatumia masaa karibia mawili kwa 30W charger. Test benchs karibia zote zinakuta 6 Pro inachaji kwa 22W tu. Hiyo charging speed hata midranges za Xiaomi zinaizidi mbali.

2. Processor. Kuanzia 6 Pro Google walitumia Tensor ya kwao, ni processor ya kipumbavu. Kuna sababu kwanini Samsung flagships zake hawapendi Exynos yao wanachukua Qualcomm Snapdragon. Huwezi kurupuka ukatengeneza processor ndani ya miaka mitatu eti uwazidi Qualcomm. Suala la processor achana nalo Pixel haina uwezo mkubwa, nenda kwenye test benchs uone marks zake. Apple's Bionic series na Qualcomm's SD hazina mpinzani bado.

3. Music gani Pixel iko vizuri? Ina nini kwenye muziki. Kwamba speakers zake zimetengenezwa at least na teknolojia ya Dolby au? Pixel 7 na Pro zina speaker za hovyo. Nenda kwenye sound test uone rating.

Bado kwenye reliability issues, modem ya network sio strong, ukija kwenye screen hakuna 120Hz halisi, Google wanadai eti processor inafanya optimization yenyewe kujua demand hivyo inapandisha na kushusha Hz. Kwanini reliably wasiweke option ya wewe kuchagua kwenye settings unataka 60, 90 au 120. Mwisho wa siku kwenye testing hakuna ushahidi kwamba processor ina uwezo wa kutambua vizuri uhitaji na kujioptimize, failure hiyo.

Ulishawahi kutumia flagships shindani au umetumia Pixel pekee ukashangilia. Pixel ni camera, mengineyo sio simu ya kupigia kelele. Google ni waongo na wahuni wahuni kwenye taarifa zao disclaimer kibao na kujitetea mara under room condition, under our own testing results alafu kwenye real use unakuta matokeo tofauti sana na matangazo.

Hakuna flagships zinaongoza kulalamikiwa kama za Pixel na Xiaomi. Hakuna flagships zinarudishwa au kuuzwa mtumba miezi michache ya kununuliwa kama za Pixel. Na bei inaporomoka, na wazungu nao wananunua refurbished?
 
Kwenye upande wa ukaaji wa chaji nadhan inategemea na uwezo wa betri kabla ya kujua umenuna makumbusho.

Mfano mm natumia pixel 4a 5G betri yake n 3800+ ambayo kwa kawaida kama unatumia simu sana bc haikutoshi, mwanzo nlkuwa natumia Tecno ina 5000 uwezo wa betri na sikuwahi kutembea na chaji.
Unafanisha tecno na pixel mzee kuwa na heshima basi

Pixel 5a Lina betrre mah elfu 4 na Kitu

Na inakaa na chaji siku nzima nacheza game napicha nakula music Chuma Iko Dede

TATIZO wabongo mnakalili sana

Kuna simu za mtumba zimenyooka tunamia tuna mwaka Sasa
 
Tuanze kimojakimoja ulichotaja.
1. Battery na chaji. Pixel gani inakaa na chaji? Achana na za nyuma, Pixel 6 Pro ni 5000mAh ila fast charging yake ni ya kiwendawazimu, kwa 30W charger unapata almost 50% kwa 30 mins, speed ya kawaida kabisa. Ila ukija kuijaza simu unatumia masaa karibia mawili kwa 30W charger. Test benchs karibia zote zinakuta 6 Pro inachaji kwa 22W tu. Hiyo charging speed hata midranges za Xiaomi zinaizidi mbali.

2. Processor. Kuanzia 6 Pro Google walitumia Tensor ya kwao, ni processor ya kipumbavu. Kuna sababu kwanini Samsung flagships zake hawapendi Exynos yao wanachukua Qualcomm Snapdragon. Huwezi kurupuka ukatengeneza processor ndani ya miaka mitatu eti uwazidi Qualcomm. Suala la processor achana nalo Pixel haina uwezo mkubwa, nenda kwenye test benchs uone marks zake. Apple's Bionic series na Qualcomm's SD hazina mpinzani bado.

3. Music gani Pixel iko vizuri? Ina nini kwenye muziki. Kwamba speakers zake zimetengenezwa at least na teknolojia ya Dolby au? Pixel 7 na Pro zina speaker za hovyo. Nenda kwenye sound test uone rating.

Bado kwenye reliability issues, modem ya network sio strong, ukija kwenye screen hakuna 120Hz halisi, Google wanadai eti processor inafanya optimization yenyewe kujua demand hivyo inapandisha na kushusha Hz. Kwanini reliably wasiweke option ya wewe kuchagua kwenye settings unataka 60, 90 au 120. Mwisho wa siku kwenye testing hakuna ushahidi kwamba processor ina uwezo wa kutambua vizuri uhitaji na kujioptimize, failure hiyo.

Ulishawahi kutumia flagships shindani au umetumia Pixel pekee ukashangilia. Pixel ni camera, mengineyo sio simu ya kupigia kelele. Google ni waongo na wahuni wahuni kwenye taarifa zao disclaimer kibao na kujitetea mara under room condition, under our own testing results alafu kwenye real use unakuta matokeo tofauti sana na matangazo.

Hakuna flagships zinaongoza kulalamikiwa kama za Pixel na Xiaomi. Hakuna flagships zinarudishwa au kuuzwa mtumba miezi michache ya kununuliwa kama za Pixel. Na bei inaporomoka, na wazungu nao wananunua refurbished?
Unaandika Ukiwa ume copy na kupaste wapi watu tunatoa maon kwasababu ndo simu nazotumia Mimi Nina uhakika hata pixel 3a xl ujawahi Tumia embu ongeeni Vitu mkiwa experience

Nina pixel 5a na 4xl ziko bomba Kila idara

Marekani anatumia refubished kwani uko USA SI Kuna viwanda vyakufufua simu na vifaa vyote ya kielectronic
Hata pia maduka makubwa ya Vitu used ambavyo viko well condition Kuna tofauti Kubwa kati used na refurbished (simu zilifanyiwa marekebisho)

Mpaka Vya magari zipo Kuna GMC kibao Tu ambazo modified Kwa Huko USA sio big deal mtu Kutumia Kitu kilichofanyiwa maboresho (refurbished) alafu Unakuja Hapa unalalama oh pixel Mbovu sijui nini

Pixel itabaki kuwa pixel Tu

Bado ujasema wewe mpaka useme
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom