Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,285
- 2,595
Hatimaye Google wameachia update mpya kwa watumiaji wa simu za Google Pixel ili kuondoa changamoto ya kukatika kwa mtandao.
Si unakumbuka wiki kadhaa zilizopita tuliposti makala kuhusu changamoto zilizowakumba watumiaji wa Simu za Google Pixel 6 series, 7 series, 8 series, 9 na 10 Series.
Update mpya imekuja kuweza kutatua changamoto mbalimbali;
🛜 tatizo la simu kupoteza network au ukipigiwa unaambiwa haupatikani.
🪫 Tatizo la betri la simu yako kuisha Haraka.
📸 Kamera kupoteza ubora kwenye kupiga picha.
📲 Kioo Cha simu kucheza cheza (display flickering) na mistari inajitokeza.
🔥 Simu kupata Sana Joto balaa nk.
Kama ulikumbana na hii Changamoto unapaswa kufanya update ili kuweza kutatua hizo shida kwenye kifaa Chako, Google wametoa update ili kuweza kujianda watumiaji wa Android kupokea toleo jipya la Android 17 wiki ijayo.
Pia update hii ni Muhimu ili kuongeza Usalama zaidi kwenye vifaa vya Google Pixels hakikisha unafanya update 👋.