Godbless Lema avuliwa ubunge

Status
Not open for further replies.
Wakuu ukombozi wa Tanzania unahitaji uvumilivu wa hali ya juu. Na ukombozi unapatikana kwa bei kubwa sio kirahisi kama tufikiriavyo.
Kwa jinsi Dr. Slaa na uongozi wa CHADEMA walivyo na intelijensia ya hali ya juu, hili swala naamini walishalijua mda mrefu na tayari wana mpango mkakati unaotekelezeka ili jimbo lirudi mikononi mwa CHADEMA. Tuwe na subira na tuwaamini viongozi wetu wa chama.
 
No doubt about that mkuu, ujue ile hukumu aloiandika mwingine tena imeandikiwa Dar na aloisoma mwingine kabisa. CCM waelewe kuwa kadiri wanavyozidi kutumia dora, ndivyo wanavyozidi kujivua nguo!
 
Hata akivuluwa ubunge..magamba hawatalichukua jimbo hilokamwe.


Wananchi walitaka waruhusiwe Arusha isitawalike tena lakini uongozi wa Chadema uliwasihi watulie na wakakubali kutulia... hivyo kama itaibuka fujo yeyote ijulikane waanzilishi ni CCM ili kuishaeua Chadema.
 
Nishawahi kusema njia ya kukijenga chama ni pamoja na hizi chaguzi.Kwa ujumla i real see changes.CDM kwa uchaguzi wa Arusha itakuwa imewafungua na kuwaonesha watanzania njia.Yaani hata CCM waje wote akiwapo M/kiti wao, CDM is going to win na Lema anakuwa Mbunge tena...
 
Naipenda sana hii. Kwa kweli hii ni fursa nzuri ya CDM kuweza kufanya kazi ya kujiimarisha zaidi ingawa hatuna wasiwasi wo wote kwamba jimbo la Arusha Mjini literejea mikononi mwa CDM tu. Wacha watangaze huo uchaguzi!!!
 
Wakuu atakayebahatika kuipata hukumu husika tunaomba ailete hapa jamvini ijadiliwe kwa misingi ya ueledi. Nawasilisha ombi langu wakuu.
 
Kuna watu wanasema anachotakiwa kufanya Lema ni kusimama na kuthibitisha yeye ndiye Godbless Lema ana anagombea tena ubunge. Mambo ya campaign na kura aisihangaike nayo watu watu wanajua nini cha kufanya. Bring on NEC & Tendwa!
 
haha haaaa nimefurahishwa sana nilivyo sikia kua jamaa wa ccm wanaruka sarakasi na TAULO kinachofata hapo ni kuexpose utupu asee..!
 
samahani wataalamu, nisaidieni nataka kujua je bwana lema anaruhusiwa kugombea tena?
Ndiyo, anaruhusiwa kugombea tena na hivyo tutamrudisha mjengoni kwa kishindo kikuu. Yaani CCM wamechemka kinoma, yaani wao walifikiri kuwa Lema angekata rufaa ambayo ingepigwa pigwa kalenda mpaka 2015. Tumewafunga goli la kisigino. Ndani ya siku 90 tunamjengoni. wakijaribu kuchakachua, watakua wameanzisha umwagaji wa damu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom