Uchaguzi 2020 Godbless Lema achukua fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Wakala wake

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
74,125
2,000
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini (Chadema),Godbless Lema ametangaza nia ya kugombea nafasi ya ubunge ndani ya chama hicho baada ya kuchukua fomu makao makuu ya chama hicho na kuahidi ushindi was kishindo.

Akikabidhi fomu hiyo kwa mke wa Lema,Neema Lema baada ya Lema kuwa safarini, katibu wa chadema wilaya ya Arusha ,Mosses Nanyaro alisema kuwa chama hicho kimejipanga kutoa mgombea aliyebora ili kulirejesha jimbo hilo kwa kishindo kwa kuwa anaamini bado chadema inakubalika Arusha Mjini.

Nanyaro alisema kuwa utaratibu wa chama hicho katika nafasi ya ubunge ni kuwa na wagombea wapatao watano watakaotia nia ila hadi sasa waliojitokeza ni wanne akiwemo Lema aliyeamua kujitangaza huku wengine majina yao yakibaki siri.

Akiongea kwa niaba ya Lema ,Neema alisema kuwa ameamua yeye na watoto wake kumchukulia fomu mume wake kwa kuwa familia inaunga mkono jitihada zake za kisiasa .

"Ninauhakika iwapo chama kitampitisha Lema, chadema itashinda ubunge Arusha mjini asubuhi na mapema ,kwani mambo yaliyofanywa na baraza la madiwani wa chadema katika jiji la Arusha ni kielelezo tosha cha ushindi" Alisema Neema.

Hii ndiyo Taarifa zinazozunguka kwenye vijiwe vyote vya Arusha

FB_IMG_1594294148358.jpg

Taarifa hii inazima kabisa uvumi wa Mh Lema kwenda kwenye majimbo Mengine

Pichani : Mwakilishi wa Mh Lema akichukua fomu kwa niaba yake

ZOEZI LA UCHUKUAJI FOMU (CHADEMA) ARUSHA MJINI.  Maandalizi ya awali ya zoezi la ( 334 X 640 ).jpg

=====

Godbless Jonathan Lema alizaliwa Octoba 26, 1976. Ni mwanachama wa Chadem, aliekuwa mbunge wa Arusha Mjini tangu 2010 hadi 2020
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
23,798
2,000
Sioni vizuri huyo aliyeshika fomu ni mwanaume au mwanake simwelewi mwelewi
 

bwege nazi

JF-Expert Member
Sep 25, 2018
705
1,000
Anaomba ridhaa kisupastaa.. eti katuma mwakilishi amchukulie fomu, wabongo bwana!
 

NAWATAFUNA

JF-Expert Member
Nov 14, 2019
4,117
2,000
Kwenye picha kuna babu kushoto anauso wa mbuzi.kanuna kama kamfumania mtu anamla pinti yake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom