mwana wa Tanzania
Member
- Nov 27, 2019
- 35
- 145
Mtandaoni zinasambaa taarifa kuhusu aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kupata hifadhi ya Kisiasa Nchini Canada.
Kinadharia Hifadhi ya Kisiasa hutolewa kwa mtu ambaye kutokana na shughuli zake za Kisiasa anapata matishio ya Usalama wake aghalabu kutoka kwa Vyombo Vya Ulinzi na Usalama vya nchi husika.
Je, ni kweli Lema ameenda kutafuta hifadhi ya kisiasa?
HAPANA, Lema sio mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa na hatari kwa taifa kiasi kwamba Vyombo vya Ulinzi na Usalama pengine vipange njama za kumdhuru ili kulinda maslahi ya nchi, Lema alikuwa mbunge wa jimbo la Arusha, nje ya jimbo hilo hafahamiki kabisa.
Ukweli ni kwamba Lema amekimbia nchini kwa kivuli chake mwenyewe (sababu binafsi) ambazo ni pamoja na:-
Aibu ya kushindwa ubunge, baada ya Lema kukosa ubunge aliokuwa nao kwa zaidi ya miaka kumi huku akijinasibu kwamba yeye ni Rais wa Arusha, ilimjia aibu atatazamwa vipi na wananchi hivyo akabuni mkakati wa kutafuta maisha nje ya nchi.
Lema alikosa shughuli (ajira) ya kufanya yenye kipato cha kutosha, kitendo cha Mrisho Gambo kuibuka mshindi wa Ubunge Jimbo la Arusha Mjini kilimaanisha Lema alipoteza kazi ya ubunge ambayo kwa zaidi ya Miaka kumi, Lema kama ambavyo amekuwa akijinadi kuwa ni mtoto wa mjjni akawaza ataiendeshaje familia yake akaiona fursa ya kubuni matishio ya kisiasa ili mabeberu wampatie hifadhi ya Kisiasa huku wakimpatia fedha za kugharamia maisha yake.
Lema amekimbia madeni ya Benki, bila shaka mtakuwa mnakumbuka kauli aliyowahi kuitoa Mhe. Spika Job Ndugai kwamba Lema anadawa zaidi ya Milioni 600, katika mazingira ambayo Lema amepoteza ajira ambayo alikuwa anategemea kumsaidia kulipa deni akaona isiwe tabu ngoja nibuni sababu ya kukimbia hayo madeni.
Lema amekimbia kesi za uchochezi, upotoshaji zinazomkabili katika Mahakama mbalimbali ikiwemo ya Mkoani Singida ambapo alipotosha kuhusu idadi ya watu waliokufa. Kuna kila dalili Lema amebaini kesi nyingi atakutwa na hatia hivyo ameamua kujiongeza ili kuepuka kwenda jela.
Watanzania tuwe makini na kauli za Wanasiasa wa Upinzani kipaumbele chao cha kwanza ni maslahi binafsi halafu Taifa baadae, tuendelee kuilinda na kuijenga nchi yetu kwa wivu mkubwa "Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe"