Wana JF,
Nimesikia sasa hivi kupitia TBC 1 radio kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha iliyokuwa ikisikiliza kesi ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) imeshatoa hukumu asubuhi hii na kwamba Mhe. Gobbless Lema amenyang'anywa Ubunge mezani na Jaji Gabriel Rwakibarila.
Hivyo kuanzia leo Mhe. Godbless Lema si Mbunge tena na Jimbo la Arusha Mjini liko wazi.My take: Hukumu hii itaacha maswali mengi sana ndani ya mioyo na vichwa vya Watanzania. Kwamba hukumu ya Kesi hii ilikuwa imepangwa kimkakati na Chama Cha Magamba kwa kuitumia Mahakama kumnyang'anya Lema na CHADEMA jimbo hili kwa makusudi ili Uchaguzi urudiwe.
Inasikitisha kuwa sababu zilizotolewa na upande wa walalamikaji ambao ni WANACHAMA 3 WA CCM hazikuwa na uzito wa kutengua matokeo ya Ubunge wa Jimbo la Arusha mjini. Ikumbukwe kuwa mgombea wa Ubunge wa CCM Bi Matilda Buriani aliyebwagwa chini na Godbless Lema hakufungua kesi hiyo wala hakuwahi kutokea kwenye Mahakama hiyo kutoa ushahidi kwamba Lema alitoa kauli za udhalalishaji, matusi na kashfa kwa Bi Buriani. Kwanini mgombea wa CCM asemewe na watu wengine ilhali mwenyewe kakaa kimya??
CCM wamecheza rafu katika hili. Hata hivyo hata kama Uchaguzi utaitishwa leo hii WEMBE NI ULEULE ULIOMNYOA SIOI SUMARI KULE ARUMERU EAST. CCM wasifurahie kuwa wamepata mteremko wa kurudisha jimbo hilo mikononi mwao. Wasahau. Kama wanabisha waitishe Uchaguzi waone kilichomzuia kuku kukojoa. CCM kimedhihilisha kuwa ni Chama Cha Mafisadi na Chama Cha Mahakama-CCM. Hakika Tanzania bado tuna safari ndefu ya kufikia Demokrasia ya kweli!!
Nawasilisha.
<br><br>Pole sana broda jifunze hata sheria za mitaani zitakusaidia au muulize Warioba dhidi ya Kesi na Wassira jimbo la Bunda.<br>Hapana. Ndo imetoka hiyo. Labda mumsimamishe Slaa.
This is an insult. Hapa mnamaanisha sisi hatutakiwi CDM, maana yake na narudia tena maana yake CDM ni chama cha kikristo na wakristo tu!!
ccm na lowasa na hii serikali mnachotafuta arusha mtakipata
Upo sahihi kabisa mkuu. Hili ndilo ninaloliona na mimi. Arumeru mashariki si mhimu kwa CCM kama ilivyo Arusha mjini. Kwa CCM kuikosa Arusha mjini ni hasara kubwa sana. So watatumia hila na mbinu zozote ziwezekanazo kuhakikisha wanalipata lile jimbo. Lakini kama viongozi wa CHADEMA watakuwa imara, kufanya hivyo kwaweza kuwa ni jambo jema kwa kuwa kutasababisha Libya nyingine nchini. Na hivyo kuuondoa uongozi wa CCM madarakani kwa nguvu ya Umma na kuikana democrasia uchwara ambayo huwa daima inapokwa.Heshima kwako Mkuu Makene.
We hope Arusha ni ngome ya CDM no matter what lakini lazima tukio hili la kuvuliwa ubunge kwa Lema tulipe uzito stahiki. Kuna vita iko mbele ya kurejesha jimbo hili, tusiipuuze kama tulivyojipanga na kushinda Arumeru lazima tuweke juhudi zaidi kushinda Arusha Mjini.
Katika hili lazima ieleweke kwamba, CCM wamekuwa kwa muda wote wakilitamani jimbo la Arusha mjini na kutawala halmashauri hiyo ndiyo maana walikuwa radhi kupindisha sheria ili meya wao ashinde na walitumia kila aina ya umafia imekuwa.
Haitashangaza kama watafanya umafia na ujambazi dhidi ya Demokrasia kulichukua jimbo hili. We really need to be serious na kuweka mkakati wa makusudi dhidi ya mbinu chafu za CCM. Wako tayari kufanya lolote kupata wanachokihitaji. Mfano; ni tukio la kuwakatakata mapanga wabunge wa CDM kule Mwanza.
Nitaridhika kwamba mahakama inatenda haki iwapo tu, na matokeo ya ubunge wa segerea yatatenguliwa. Otherwise, mahakama za bongo zinafanya kazi ya kisiasa kuliko kazi za kitaaluma.CDM itashida ila itakuwa fundisho kwa wagombea kutumia lugha ya matusi na uongo ambao umekuwa fasheni.Hapo issue sio lowasa ila ni kulinda amani ya nchi kwa mtu kuamua kumtukana mwenzie