😛eace:😛eace:😛eace:😛eace:😛eace:😛eace:😛eace:😛eace:😛eace:😛eace:😛eace:😛eace:😛eace:😛eace:
sasa nimeamini chadema mnapenda damu hata mawakala wenu mumewaua ili mpate sympathy
Mlalamikaji Mussa Mkanga hajui kusoma ila baada ya kesi utasikia ni mkuu wilaya ya Narung'ombe lindi,nchi ii bana ukiwafurahisha tu...
Huyu ushenzi wake ni upi mkuu? mbona anaonekana ni mstaarabu sana! nampa heshima zangu kwa heshima ya Marehemu Hayati sokoine!
Ndugu zangu,
Kuna kila dalili, kuwa tunakokwenda ni kubaya. Tumefika mahala sasa, kuwa kwenye siasa tunaingiza hulka za ushabiki wa Simba na Yanga. Hii ni hatari kwa taifa.
Jana alhamisi, kabla ya jua la saa sita mchana, habari zililipuka na kusambaa kote nchini; Mahakama imemvua Ubunge Godbless Lema.
Ni ukweli, Godbless Lema ni mbunge kijana na maarufu sana hapa nchini. Lakini, imefika wakati Watanzania tukubali na tuamini, kuwa Mahakama inafanya kazi kama mhimili huru wa dola hata kama kunahitajika, kupitia Katiba mpya ijayo, kuboresha mhimili huo ili uaminike zaidi.
Ni kwa mantiki hiyo, kuwa mahakama ni mhimili huru wa dola, tumeshuhudia hata Serikali ikifikishwa Mahakamani na hata kushindwa kesi. Tumeshuhudia , katika historia ya nchi hii, Wabunge wa CCM , bila kujali majina na umaarufu wao wakifikishwa mahakamani na kushindwa kesi.
Kwa Godbless Lema, kutoa hadharani madai kuwa Rais wa nchi anahusika na hukumu yake ni kauli ya bahati mbaya sana anayopaswa yeye mwenyewe Lema, na chama chake, kuacha kuendelea kuitoa, haina mantiki. Inaidhalilisha Mahakama. Ni kauli iliyotolewa kwa haraka na isiyo na tija kwa taifa.
Tukubali kwa sasa, kuwa kule Arusha hukumu imeshatolewa. Kuna fursa pia ya kukata rufaa ya hukumu hiyo kwenye Mahakama iliyo juu zaidi. Hakika, kwa Godbless Lema na chama chake, huu ni wakati kutafakari hukumu hiyo na kuona ni namna gani ya kwenda mbele kisheria au kisiasa.
Haiwezekani kwa sasa kudai kuwa CCM inahusika na hukumu hiyo. Wakati kimsingi CCM imepata 'hasara nyingine ya kisiasa' kwa matokeo ya hukumu hiyo. Kwa anayechambua kwa undani sana, hukumu ya Lema ya kuvuliwa ubunge imekuja katika wakati mbaya sana kwa chama tawala, CCM.
Ni hukumu inayomtangaza na kumwongezea umaarufu Godbless Lema na chama chake cha Chadema. Leo, bila kufuatilia mwenendo wa kesi husika, kuna wanao-sympathy na Godbless Lema na Chadema, wakiamini CCM imetumia Mahakama kumhujumu Godbless Lema na Chadema. Na kama Lema atasimama tena kuwania kiti hicho, basi, yumkini kura zake zitaongezeka maradufu. Lema ana hakika ya kura nyingi pia za ' kuonewa huruma'.
Na ukweli mwingine ni huu, katika nchi yetu kwa sasa kuna kundi jipya la wapiga kura. Hawa naweza kuwaita " Wapiga kura dhidi ya hali iliyopo"- Aina hii ya wapiga kura inaundwa kwa idadi kubwa na waliokuwa wapiga kura wa CCM katika chaguzi za miaka ya nyuma na ambao sasa hawaridhiki na hali iliyopo ndani na nje ya chama chao.
Ndio, hawa ndio waliokuwa wapiga kura wa CCM na ambao sasa wanawachanganya sana CCM. Ndio hawa waliompigia kura Nassari Arumeru, ndio hawa waliowahakikishia viti vya udiwani Chadema kule Ruvuma, Mwanza na Mbeya.
Maana, ni wapiga kura wa kundi hili unaoweza kuwaona wakijaa kwenye mikutano ya kampeni za CCM, lakini, kwa vile hawapati majibu ya maswali yao ya namna gani CCM na Serikali yake, si tu itakavyorekebisha, bali inavyorekebisha sasa ' Hali iliyopo', basi, siku ya kupiga kura wanatumbukiza kura zao kwa wapinzani.
Ndio, ni ukweli pia , kuwa ' Ndani ya nyumba ya CCM' kwa sasa hakuna amani na utulivu. Makundi na mbio za kuelekea kwenye Urais 2015 zinawaacha wana-CCM wakivurugana wenyewe kwa wenyewe.
Focus sasa haiko kwenye kutekeleza ahadi lukuki walizowaahidi wapiga kura kwenye kampeni zilizopita. Kwa sasa kuna wenye kufikiria hatma zao za uongozi. Kuna waliojikita kwenye mnyukano wa kimakundi kwenye vita ya kuelekea Urais wa 2015. CCM ya sasa inaonekana kuwa mbali na wananchi na kero zao zinazowakabili. CCM ya sasa imeacha kuwa ' Kimbilio la Wanyonge' kama wakati mmoja alivyopata kukiri Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa. CCM ya sasa ni kimbilio la ' wenye nacho' wakiwamo wafanyabiashara.
Ndio, CCM imeanza kulipa gharama ya wananchi kutoridhika na ' Hali iliyopo'.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
sawa ridhiwan kikwete lakini mahakama ya kweli ni wananchi,fanyeni mpango kutengua na urais babako!nimepitia threads nyingi na sehemu nyingi ili kuona mawazo ya wanachadema na viongozi wao. Nilichoona ni kuwa hawaaamini kama mahakama imetenda haki. Bali si hilo tu wamediriki kuhisi kuwa ati mahakama imeamuriwa na ikulu kufikia maamuzi yaliofikiwa
nimesikitishwa sana na watu ambao siku zote hujihesabu makini kwa kauli zao za kuhusisha ikulu na mahakama katika maamuzi.
Inawezekana hukumu haikuwa tamu kwao, na wanahisi hawajatendewa haki, na ndio maana kwenye sheria kukawa na haki ya kukata rufaa ili kuhakikisha haki inatendeka. Kwa hio ndugu zangu wa chadema kama mnahisi haki haijatendeka fateni taratibu za kisheria kudai haki zenu badala ya kuhubiri chuki na uongo
ndani ya chadema mna wanasheria wengi tu, watumieni ktk kuhakikisha haki inatendeka. Na si kuwa nyny mkishinda tu haki imetendeka mkishindwa haki haijatendeka huko ni kutokuwa watu wa haki.