Sasa ndio mimi na wewe tunajiuliza "Ina maana Mungu haoni yote hayo"..?
Kwanini aruhusu wachache wenye tamaa zao kuwashughulisha wengine wasiojiweza..?
Kwanini hutaki tumlaumu wakati yeye Ni muweza yote..?
Ndio nikasema hapo awali kuwa Mungu ametuumba na KUTUPATIA UHURU wa kuamua vipi tutaishi hapa Duniani.
Na kwa sisi wenye Imani na Mungu tunakubali bila shaka yyt kuwa LAZM kuwe na Hukumu mbele
Ili wale ambao waliutumia uhuru wao Vibaya WAADHIBIWE na wale walioishi kama mwanaadamu yyt anavyotakiwa kuishi Waweze KULIPWA MAZURI kwa Utu wao.
Wewe na mimi hatuhitaji Kuambiwa na Mungu kuwa KUBAKA,KUIBA,KUONE WANYONGE na Ubaya wwt havistahiki kumfanyia binaadamu mwingine.
Sasa Mungu angetuumba bila kutupa uhuru huu tulionao (yaani tuwe kama Robot) basi pia tungesema Mungu hakutenda haki.
Katunyima uhuru tunafanya Anayotaka yeye tu.
Binaadamu ni kiumbe mbaya sana km hatokwenda sambamba na Kanuni za kibinaadamu alizoumbwa nazo.
Sasa tusimlaumu MUUMBAJI kwa Makosa na matatizo tunayoleta wenyewe kwa tamaa zetu binafsi.
Lkn kumbuka IKO SIKU YA MALIPO INAKUJA.
manake kubali kataa lkn Binaadamu hayupo hapa Duniani kula kuzaa na kulala tu. Na mwisho kufa na hapo ndio mwisho wake.
Manake kwa kuamini hivyo ni kukubali kwamba binaadamu kawepo hapa Duniani kwa sababu za kipuuzi kabisa kitu ambacho sio.
Kama mbuzi ana SABABU NZURI tena MAALUM ya KUWEPO hapa Duniani basi Binaadamu ana Sababu kubwa tu tena ya maana zaidi ya KUWEPO Hapa. Na sio kula kuzaana, na mwisho kufa bila chochote baada ya hapo.