God was created when the first con-man met the first fool

God was created when the first con-man met the first fool

Kwetu uchagani miaka ya nyuma sana kabla ya wamisionari kuingia na kutangaza dini na kuileta biblia, wale wazee wa kichaga walikuwa wanaamini kuna nguvu iko mahali anaitwa Ruwa.

Walikuwa wanaamini Hii nguvu ukiiomba chochote inakupa kama kunyesha nchi mvua, kuepusha magonjwa na balaa.

Na wachaga kipindi hicho walikuwa na utaratibu wa kukutana chini ya mti mkubwa kuchinja mbuzi na kumwaga pombe ya mbege na kumuomba Ruwa awasaidie katika mambo mbalimbali

Wamisionari walivyokuja wakatangaza na kushawishi huyo Ruwa mnayemuomba ni Mungu, wakafundishwa neno la Mungu na maandiko ya biblia.

Mpaka sasa hivi Mungu anaitwa Ruwa lakini Ruwa original alikuwa Mungu wa wachaga nguvu isiyoonekana inayotenda makuu.

Mkuu
Bora wewe unahistoria ya kabila na tamaduni zenu na jinsi mlivyokua mnaabudu..

Hawa wafia dini wengi humu ni vilaza waliopitiliza hata hawajui hizi dini wanazofia zina umri gani ndani ya jamii ya mtanzania
 
Wame fail wapi?...Hata fundamentals za Modern Physics unazifahamu wewe?

Na hio First cause kwanini iwe ni Mungu Tena Specific God with Human attributes?....Kwanini kisiwe kingine
Si kila king'aacho ni dhahabu ... Lakini haimaanishi kuwa dhahabu haipo lazima uitafute use mweledi uweze kutofautisha dhahabu halisi na famba ... Si kila inayotajwa ni Sifa ya Muumba ni yake... Lakini haimaanishi kuwa hayupo inahitaji weledi, elimu na zaidi ya imani kutambua uwepo wake ...
 
Waziri hana mamlaka ya kuzuia zinaa kwasababu hana uwezo wote, angekuwa na uwezo huo angeweza kuzuia bila hata kututangazia.

Pili kama tu waziri ambaye hana uwezo wote anatamani kuzuia jambo hili lisiwapate raia wake inakuaje mungu mwenye uwezo wote na upendo wote kwa viumbe vyake ashindwe kuzuia jambo hili???
Ubishi wa kipumbavu haukuongezei chochote ktk maisha sana utaathiri jamii iliokuzunguka.
Umepewa uhuru wa kuishi utakavyo
Sasa unalaumu uhuru uliopewa?

Brbr zimewekewa speed limit sasa dereva akigonga wapita njia kwa kwenda speed kinyume na sheria utalaumu mtengeneza gari ?
bangi mnavuta kisha zinawatuma Kuiba mkipata kichapo mnamlaumu mwenye shamba la bangi .
Wenzako Bangi ni mboga na Dawa sio za kuvuta.
 
Mkuu
Bora wewe unahistoria ya kabila na tamaduni zenu na jinsi mlivyokua mnaabudu..

Hawa wafia dini wengi humu ni vilaza waliopitiliza hata hawajui hizi dini wanazofia zina umri gani ndani ya jamii ya mtanzania
Mbona unajichanganya, msingi mkuu wa Mada ni uwepo wa MUNGU hayo mambo ya dini achana nayo, kuna watu wengi wasiofuata dini yoyote ila wanaamini uwepo wa MUNGU...
 
Ubishi wa kipumbavu haukuongezei chochote ktk maisha sana utaathiri jamii iliokuzunguka.
Umepewa uhuru wa kuishi utakavyo
Sasa unalaumu uhuru uliopewa?

upumbavu kwako ni jambo la namna gani??

Kuamini habari za jua kuzama matopeni kwako ni jambo lenye fact sio?

Kuamini dunia ni bapa kwako ni jambo la fahari au ni upumbavu?

Upumbavu ulioathiri jamii ni pamoja na dini kutoa mafundisho ya kuogofya kwa jamii

Upumbavu ulioathiri jamii ni watu kuaminishwa kua jua linazunguka dunia

Upumbavu unaoathiri jamii ni pamoja na mafunzo ya kipumbavu kwa jamii kuwalaghai watu wajitoe muhanga watapata thawabu mbinguni

Upumbavu huo nilioutaja hapo juu unaweza kukuta unauunga mkono at the same time una declare kua unachukizwa na upumbavu

Brbr zimewekewa speed limit sasa dereva akigonga wapita njia kwa kwenda speed kinyume na sheria utalaumu mtengeneza gari ?
Huyo mtengeneza gari alishawahi kujinadi kua gari aliyoitengeneza imewekwa kiufanisi wa hali ya juu kiasi kwamba haitopata ajali ya namna yeyote ile??

Kama aliwahi kujinadi utasemaje hastaili lawama??

Mungu aliyejinadi kua ni mjuzi wa yite, mwenye upendo wote na muweza wa yote halafu kaumba ulimwengu huu wenye kuruhusu kila aina ya baya kwanini asilaumiwe kwa uzembe huo??

bangi mnavuta kisha zinawatuma Kuiba mkipata kichapo mnamlaumu mwenye shamba la bangi .
Wenzako Bangi ni mboga na Dawa sio za kuvuta.
Kama bangi ni mbaya unataka kuniambia mungu wako alifanya makosa kuiruhusu iote??
 
Mkuu nenda moja kwa moja kwenye hoja yako maana zinaeleweka kwa mtu yeyote anayeelewa kiingereza.

Kumbuka, sijapost quote yeyote ya Mungu na Dice...
Sijakuuliza, "Unajua kusoma lugha ya kingereza?", bali, "Je, umeelewa hizo quotes ulizo copy paste?". Tafadhali usisite kunijulisha kama bado hujanielewa.
 
Kama unataka kupata proves lazima upoteze mwili wako yan ufe mambo mnayo jadili ni ya 4D nyie mpo 3D vilaza zaid mpaka 2D
Usikute wakina tesla huko waliko wanaomba kurudi hata dak moja kutoa ushuuda ku konclude lakin haiwezekan
 
Mbona unajichanganya, msingi mkuu wa Mada ni uwepo wa MUNGU hayo mambo ya dini achana nayo, kuna watu wengi wasiofuata dini yoyote ila wanaamini uwepo wa MUNGU...

Wewe usio na dini huyo mungu umejifunzia wapii..?!
Au ww uwelewa wako wa huyo mungu ukiondoa imagination na illusion ubongoni mwako anafananaje huyo mungu wako..?!
 
Kama unataka kupata proves lazima upoteze mwili wako yan ufe mambo mnayo jadili ni ya 4D nyie mpo 3D vilaza zaid mpaka 2D
Usikute wakina tesla huko waliko wanaomba kurudi hata dak moja kutoa ushuuda ku konclude lakin haiwezekan

Kilaza mwenzetu umeyajuaje haya..?! embu tusaidie nasi tunaohoji tujue
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom