Hivyo vitu utakavyojinyima ni kwa faida yangu na maisha yangu.
kama vina hasara alishindwa mungu kuvitoa mpaka akusisitizie kwenye vitabu vyake kua uviepuke??
1. Usizini - faida unauepusha mwili wako kwa magonjwa na migogoro.
Uzinifu ulianza kabla ya biblia kuwepo, biblia imekuja kuandika kitu ambacho imekikuta. Sasa watu walioishi kabla ya biblia kuwepo waliepuka vipi hili jambo? kama hawakuweza kwanini mungu hakuwapa elimu hii ili wapate faida watu wake? Kama waliweza kuepuka, biblia ilikuja kuandika katazo hili kwa dhumuni lipi? wakati watu waliweza kuepuka bila msaada wa maandishi hayo?
2. Usiue - sio utu na uungwana kuondoa maisha ya binadamu mwenzako, pengine anafamilia inayomtegemea mbaya zaidi utaadhibiwa na sheria za nchi wakati na wewe unategemewa na ndugu zako
Kuua kulikuwepo kabla ya biblia haijaandikwa, mvunjaji wa sheria hii kwanza ni mungu mwenyewe aliyewapa sheria hiyo kua usiue halafu yeye mwenyewe akaua maelfu kwa maji na moto (hapa hata yeye alijutia kua hatateketeza tena ulimwengu kwa moto) kwaiyo mizani yetu ya uungwana inatuambia Mungu si muungwana kaangamiza maelfu kwa ukatili ambao hata yeye alijutia.
Pili mungu huyu tunaona anavunja sheria kwa kuua hadi vitoto vichanga katika vitabu vyake alivyokua anatoa adhabu ya kuua kila mtoto katika nchi ya misri kwa watu ambao hawakupaka damu ya kondoo kwenye milango yao ili kumkomoa farao katika yale mapigo kumi. Huu ukatili ukionekana umefanywa na binadamu kila mtu hatapendezewa nao ila kafanya mungu watu bado wanamtolea na sadaka
3. Usiibe - Mwenzako ametafuta mali yake kwa jasho kwanini unaiba sasa, kufuata hii amri au katazo litakusaidia usiuwawe au kuumizwa kwenye wizi na usimrudishe nyuma kimaendeleo yule unayemuibia.
Kuiba kulikuwepo hata kabla biblia haijaandikwa. Mfano mdogo mababu zetu ambao walikua wakiishi bila biblia waliweza kupata maadili mazuri bila kutegemea hizi riwaya. Mababu zetu waliweza kujua kua wizi ni jambo baya bila hata kusoma vitabuni, sasa unavyoleta nukuu kutoka vitabuni unamaanisha bila kuandikwa jambo hilo humo lisingewezwa kuchukuliwa kwamba jambo baya??
4. Waheshimu baba na mama yako:- ni jambo jema kuwaheshimu wazazi wetu kwa kutuleta duniani na kutulea na kutuongoza katika njia ipasayo. Usipowaheshimu utakosa mawaidha, busara zao na mafundisho yao kwako.
Kwanza swala la heshima halitakiwi liwe na mipaka, kwamba watu fulani tu ndio waeshimiwe afu wao wasiheshimu wengine
Kuna habari kua kuna mzee nuhu alikunywa pombe akalewa akakaa vibaya (uchi) mtoto wake mmoja alivyomuona akamcheka baba yake wenzake walivyomuona baba yake katika hali hiyo wakamsitiri baba yao, baba huyo baada ya pombe kumtoka akampa laana huyo mtoto kwa kosa la kumcheka. Sasa hapo nani hana heshima kati ya baba na mtoto?? Pili vigezo gani Mungu alitumia kuiruhusu laana hiyo imfike huyo mtoto???
Jibu ni baba ndiye hana heshima huwezi ukanywa konyagi bila kula halafu ukalewa ukakaa m@tko wazi utegemee mtoto asicheke, mtoto hana kosa kwasababu tunaweza kusema ni akili za kitoto tu
hii pia inaleta ukakasi sana. Biblia imesema adam na eva walikua na watoto wawili ambao wote ni wakiume, so dunia nzima ilikua na jumla ya idadi ya watu wanne yaani mwanamke mmoja wanaume wa tatu. Huyu mmoja akafa yule mwingine akaoa na kuzaa watoto sasa hapa huoni kwamba alilala na mama yake?? Heshima gani hiyo ya kulalana ndugu kwa ndugu??
5. Usimtamani mke wa jirani yako, Ng'ombe wake:- hili katazo linakuepusha na migogoro na jirani yako, linakuepisha na kwenda kuuwawa au kuumizwa au kushtakiwa na serikali kwenye wizi wa mali ya jirani yako.
tamaa mbaya eh?? Mbona mungu naye anawivu anatamani aabudiwe yeye tu hii kwako imekaaje??
Kwahiyo hata kama huamini Mungu lakini kuwepo kwa hizi sheria zake na nyingine kwako ni faida na si hasara
kwanza kabisa kuwapo kwa hizi sheria si kwamba taratibu hizi si kwamba zinafatwa kwasababu biblia imeandika, hapana. Nataka nikuambie kwamba biblia imekuja imekuta watu wakiendelea kuepuka mambo hayo. Makatazo au mahalalisho ya vitu havitegemei permit kutoka kwenye biblia ili lionekane jambo zuri au baya kwa jamii. Mbona biblia haija orodhesha makosa ya cyber criminals watu wana crack na ku hack vitu utatumia sheria ipi katika biblia kukataza jambo hili??