UAR mwarobaini kwa wanafunzi wanaenda kusoma nje ya nchi

Apr 9, 2022
66
32




Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Taasisi inayowakilisha Vyuo Vikuu vya nje ya Nchi Tanzania (UAR) Tony Kabetha ameiomba Serikali kutoa mikopo, kwa Wanafunzi wanaoenda kusoma nje ya Nchi ili kuwawezesha kufikia malengo yao pamoja na kuijenga Nchi yao kiuchumi.

Wito huo umetolewa kwenye maonyesho ya 18 ya Elimu ya Juu,Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Nchini( TCU) ambayo yanaendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.

Hata hivyo Kabetha anaeleza kwamba Wanafunzi wamekua na kiu ya kwenda kusoma katika vyuo vya nje lakini wanashindwa kutokana na gharama kuwa kubwa, hivyo anaiomba Serikali kuwapa mikopo inayolingana na wanafunzi wanaosoma hapa Nchini ili waweze kwenda kusoma na kuweza kuja kuijenga nchi kiuchumi.

“Tanzania ni nchi inayoendelea hivyo inahitaji wawekezaji wengi wa tenkolojia, tunakaribisha wawekezaji ambao unakuta wamesoma kwenye vyuo hivihivi ambavyo vijana wa kitanzania wanaenda kusoma ,naomba niishuri serikali ione namna ya kuwapatia Mikopo vijana wanaoenda kusoma vyuo vikuu vya nje.” Amesema Kibetha

Nakuongeza kuwa sisi kama UAR tumekua tukiyashiriki Maonyesho haya kwa muda wa miaka zaidi ya 10 kutokana na ndoto au matarajio au mahitaji,hivyo imekua sehemu ya vijana wengi yakuweza kujua kujua wapi waende wakasome.

Amesema kuwa changamoto kubwa iliyopo watu hawakujua nini cha kusoma hivyo walisoma vitu ambavyo leo havina soko nakwamba wamekuwa wakiwashauri vijana yale waliyoyasoma kwa kuzingatia matakwa au sheria ya TCU kwamba yanakubalika katika nakwamba Tanzania imefanikiwa.

Aidha ameendelea kusema kuwa Changamoto nyingine ni gharama ya kulipia ada kwenye vyuo vya nje lakini UAR imefanikiwa kuleta vyuo ambavyo vinatoa ufadhili ( scholarship) ambapo ukienda kulipa ada ni sawasawa na vyuo vikuu vya hapa Tanzania

“ Kikubwa ambacho tupo nacho sisi kwa awamu hii ya tatu ni kwamba nikuhakikisha wanafunzi wanaenda kusoma kwenye vyuo ambavyo wanaweza kufanya kazi na kupata kipato ambacho wanaweza kujisaidia hata kwa ada, Nchi hizo ni Marekani,Ujerumani ,Poland pamoja na Hisapania.

Ameongeza kuwa mbali na hilo pia vijana wengi wana vipaji mbalimbali kulingana na uwezo wao, hivyo taasisi hiyo imepata nafasi katika nchi za Ujerumani na Hispania kuwapeleka vijana wenye vipaji ili kuendeleza vipaji vyao.

Amesema kuwa UAR ni taasisi ya kwanza kutoka hapa Tanzania kwa kuweza kusaidia vijana kusoma na kupata ajira nje ya nchi, kitu ambacho kama Taasisi tunajivunia.

“Malaysia na China zilikua pamoja nasi katika miaka ya sabini lakini walifanya upendeleo kwa watu wao kwenda kusoma nje ya nchi ili waweze kufanya kazi kutokana na ile tknoloji waliyopata kutoka nje” amesema.
 
Back
Top Bottom