Global Alliance inauharibu mji wa Kahama

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,642
9,222
Wakuu habari

Global alliance wamepanga ktk jengo la NSSF umbali wa mita 100 kutoka yalipo makao makuu ya manispaa

Vijana wengi kutoka Wilaya zinazopakana na Kahama wenye umri kati ya miaka 16 hadi 29 wamekuwa wakitolewa maeneo mbali mbali na kupelekwa kahama kisha kupangishiwa chumba, chumba wanakaa wanne wanne, kisha kutozwa ada ya laki sita kila mmoja

Mwisho wa siku wanaacha baada ya kupigwa kilo 6 wanabaki mtaani wanalanda landa wengine wanaishia kupigwa mimba wengine wanageuka kuwa vibaka

Vijana wanaoletwa kwa wingi ni kutoka Tabora, Nzega, Kaliua, Masumbwe, Runzewe, Ushetu n.k wanaletwa kwa gia ya kushawishiwa kuwa matajiri

Ukikutana nao asubuhi utasema ni wanachuo au wafanyakazi, ukiwauliza wanafanya kazi gani wanakujibu ni wafanya biashara wa alliance

Hii ALLIANCE inaharibu mji wa KAHAMA serikali iingilie kati vijana wengi wanaharibiwa mwisho wa siku wanajikuta hawana msaada wowote

Nawasilisha
 
Wakuu habari

Global alliance wamepanga ktk jengo la NSSF umbali wa mita 100 kutoka yalipo makao makuu ya manispaa

Vijana wengi kutoka wilaya zinazopakana na Kahama wenye umri kati ya miaka 16 hadi 29 wamekuwa wakitolewa maeneo mbali mbali na kupelekwa kahama kisha kupangishiwa chumba, chumba wanakaa wanne wanne, kisha kutozwa ada ya laki sita kila mmoja

Mwisho wa siku wanaacha baada ya kupigwa kilo 6 wanabaki mtaani wanalanda landa wengine wanaishia kupigwa mimba wengine wanageuka kuwa vibaka

Vijana wanaoletwa kwa wingi ni kutoka Tabora, Nzega, Kaliua, Masumbwe, Runzewe, Ushetu n.k wanaletwa kwa gia ya kushawishiwa kuwa matajiri

Ukikutana nao asubuhi utasema ni wanachuo au wafanyakazi, ukiwauliza wanafanya kazi gani wanakujibu ni wafanya biashara wa alliance

Hii ALLIANCE inaharibu mji wa KAHAMA serikali iingilie kati vijana wengi wanaharibiwa mwisho wa siku wanajikuta hawana msaada wowote

Nawasilisha
Wasukuma na wanyamwezi wamefikiwa

Sent from my VTR-L29 using JamiiForums mobile app
 
Hahah hahaha hahaha

''Ukiona unaitwa katika fursa jua wewe ndo fursa kwa wakuitao"
 
Kauli mbiu yao ni AFYA NA MALI .Hata hapa mwanza wameenda wengi na Cha kushangaza ni vijana wengi wao ni wahitimu wa vyuo.
 
Hata Mwanza kuna binti ninayemfahamu ametolewa Tabora na amejiingiza kwenye biashara ya kudanga baada ya kutapeliwa pesa ya ada
 
Yaani jamaa wa Alliance kindaki ndaki hata ukikutana nae usiku na zile suti zao salamu zao utasikia "Good morning Champ" 😁😁😁😁😁
 
ndugu yangu kaingia hko,siku nmeenda ofisini kwao nilibakia nacheka tu nakuondoka zangu
 
Back
Top Bottom