Kahama: Rais Magufuli amsamehe Mkurugenzi wa Halmashauri aliyenunua gari kinyume na utaratibu. Kahama yapandishwa hadhi kuwa Manispaa

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
916
1,000
Baada ya salamu kutoka kwa viongozi mbalimbali, Rais Magufuli anategemea kuhutubu punde.. Kwasasa kinachoendelea ni burudani kutoka kikundi cha asili.
======

WAZIRI JAFFO: Toka tunapita barabarani watu wamejaa sana, hi ni ishara kwamba, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ni Rais wa watu lakini watani zangu naona mko vizuri sana katika mambo flani maana katika mikoa mingine ukipita watoto huwaoni barabarani lakini Shinyanga hapa hata mheshimiwa mbunge wa Jimbo amesema, idadi ya watoto idadi ya watoto wanaozaliwa.

Hii ikionesha kwamba watani wangu wa Shinyanga mko vizuri sana, kwa hiyo hongereni sana watani zangu wa Shinyanga.

RAIS MAGUFULI: Lakini pia nikapata heshima ya kwenda kuweka jiwe la msingi la Jengo la hospitali, nilipoambiwa OPD mimi nilijua labda ni jengo moja pale mbele ya kupokelea wagonjwa, nimeingia pale nimekuta kumbe ni jengo kubwa, jengo zuri lenye plan nzuri linalojengwa na vijana wetu wa JKT, nalo nikaambiwa fedha zote ni mapato ya ndani ya halmashauri hii.

Nikawa namuangalia mkurugenzi, alikuwa na katuhuma tuhuma kidogo ka kujinunulia gari, nikasema lakini kama fedha na kupitia madiwani wamejenga hili jengo la bilioni 1.8, wanajenga jengo la hospitali kubwa tu kwa bilioni 3, ngoja nione mpaka mwisho, nikapelekwa kwenye mradi wa tatu nikakuta likiwanda likubwa, ni kama yaleyale maviwanda nilikuwa nikiyaona Ulaya.

Nilipokuwa nikipewa taarifa pale, nikaambiwa ardhi hii yote ilitolewa na halmashauri na ni heka 90, ilitolewa bure. Nikajiuliza sana huyu mkurugenzi na madiwani wana akili sana, wametoa eneo bure, lengo lao wameangalia mbele zaidi kwamba wakishajenga kiwanda, kwanza kitatengeneza ajira za wananchi wa hapa, watakusanya pia kodi.

Kwa hiyo nimemamua kumsamehe mkurugenzi huyu na hili gari namurushia aendelee kuliendesha lakini asirudie tena kununua magari nje ya utaratibu wa sheria.

Ninajua unapigwa vita, wanaokupiga vita sasa wakuogope kwamba unafanya kazi nzuri, ninahitaji watu wa namna hii, kakosa kale kadogo kamefuta dhambi zake. Nimeshangaa kweli wilaya hii ya Kahama ina mipango mikubwa ninayoipenda.

Na mimi nasema kwa sababu mmenipa kura alafu ndio Rais na kazi ya kupandisha mimi mmenipa, ninaipandisha iwe Manispaa.

==========

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ameipandisha hadhi halmashauri ya Kahama Mji kuwa Manispaa ambapo sasa Kahama Mji itajulikana kama Manispaa ya Kahama.

Rais Magufuli amesema hayo leo Alhamis Januari 28,2021 wakati akizungumza na wananchi katika uwanja wa taifa wilayani Kahama.

"Kutokana na mahitaji yaliyopo hapa Kahama naipandisha halmashauri ya Kahama Mji kuwa Manispaa na hiyo hospitali ya Kahama iwe na hadhi ya Manispaa",amesema Rais Magufuli.

Mkoa wa Shinyanga sasa utakuwa na Manispaa mbili (Manispaa ya Shinyanga na Manispaa ya Kahama), lakini pia kuwa na halmashauri za wilaya nne ambazo ni halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Shinyanga, Ushetu na Msalala.

Rais Magufuli pia amemsamehe Mkurugenzi wa Kahama Mji, Underson Msumba ambaye ni miongoni mwa wakurugenzi wanne waliokuwa na kashfa kwa kununua magari ya kifahari ambapo amesema amemsamehe na kumuachia gari hilo kutokana na jinsi anavyofanya kazi vizuri na kwa kujituma akishirikiana na madiwani ambapo wamekuwa wakitekeleza miradi yenye kuwaletea maendeleo wananchi.

"Mkurugenzi wa Kahama Mji unafanya kazi kubwa sana, ka kosa kale kadogo kamesamehe dhambi zako zote. Unafanya kazi sana najua unapigwa vita ila wanaokupiga vita kuanzia sasa wakuogope.

Nimemsamehe Mkurugenzi huyu, amefanya makubwa! Mkurugenzi hongera Sana. Na hilo gari nitamrudishia aendelee kuliendesha lakini asirudie kununua gari nje ya utaratibu",amesema Magufuli.

"Kahama panapendeza, nimekuta kiwanda kama vile vinavyojengwa Ulaya, Mkurugenzi wa Kahama na Madiwani wana akili sana, wametoa eneo bure hawakumuuzia Muwekezaji, wameangalia mbele kwamba watatengeneza ajira na wataongeza kodi, ni busara kubwa sana",ameongeza Rais Magufuli.

Rais Magufuli pia amemuagiza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Doroth Gwajima kuipandisha hadhi hospitali ya Mji Kahama iendane na hadhi ya Manispaa.

"Nawaongezea Sh Milioni 500 kuchangia jengo la hospitali ya mji Kahama. Na kwa vile waziri wa afya yuko hapa aipandishe hadhi hiyo hospitali ili endane na hatua ya Manispaa," amesema Rais Magufuli.
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
17,753
2,000
... akiwa kiongozi na amri jeshi mkuu ni muhimu aeleze wananchi cha kufanya kukabiliana na janga la Corona lililoikumba nchi na dunia kwa ujumla.

Sidhani kama wote wanaochukua hatua madhubuti kupambana na hili janga ni wajinga sisi ndio werevu. Wananchi wanajiendea tu kama kondoo wasio na mchungaji!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom