GITARAMA: Jehenamu duniani!

GITARAMA: Jehenamu duniani!

Izo c dola mia tatu ishirini na tano kwa maneno sawa na km laki saba apo au mwandishi umekosea kuandika?
 
Steve, maendeleo gani kama watu wako jehanamu gitarama? Ndiyo maana wanasiasa wanasema afadhali kuishi kwenye ufisadi tukiwa na democracy kuliko kupambana na ufisadi ndani ya utumwa
Rwanda labda usafi wa barabara. Lakini watu ni masikini bahati nzuri tumeoa Rwanda napajua vijijini pakoje, vizuri sana
Kwahyo mkuu unataka kusema kwamba Rwanda vijijini hali ni mbaya sana!
 
Bwana Papillon alifariki kwa kansa ya koo. Na kadiri muda unavyozidi kusonga, inavumbuka ya kwamba kitabu chake kilijazwa na simulizi ambazo si yake bali mjumuisho wa simulizi mbalimbali za wafungwa aliokuwa nao pamoja.

Lakini pia mamlaka ya Ufaransa imekanusha mara kadhaa kwamba Papillon alifungwa humo - Devil's island.

Ila yote ya yote, bwana huyu anatuachia ujumbe mkubwa sana kuwa chochote kinawezekana ukidhamiria.
Asante sana kwa hii story ya papillon.

Hichi kisiwa cha hili gereza kiko wapi haswa?
US, France au ......
 
Asante sana kwa hii story ya papillon.

Hichi kisiwa cha hili gereza kiko wapi haswa?
US, France au ......
Kisiwa hiki kipo kwenye koloni la nje la ufaransa linaloitwa French Guiana. Nchii hii ipo huko Amerika ya kusini ikipakana na Brazil upande wa kaskazini.

Sent from my SM-J110F using JamiiForums mobile app
 
Kwa wengi ukisema Jehanamu basi picha inayowajia ni sehemu ya mateso ambamo wenye dhambi wote watatupwa baada ya hukumu, lakini ukweli ni tofauti kabisa. Neno Jehanamu lina tafsiriwa kwenye biblia ya kiswahili kutoka nen0 la ki-ebrania "Gehinnom", neno gehinnom lina maana "bonde la Hinnom" yaani "the valley of Hinnom".

Sasa ni kwanini jehanamu (bonde la Hinnom) imekua ikidhaniwa kua ni sehemu ya mateso baada ya kifo? Katika historia bonde hili lipo upande wa kusini magharibi nje ya ukuta wa jiji la kale la Jerusalem, waflme wa Yudea baada ya kuasi kutoka kwa Mungu wa Israeli na kuanza kuabudu Mungu baal (baali) waliwatoa sadaka watoto wao kwa kuwachoma moto wakiwa hai katika bonde hilo, hivyo Mungu wa Israeli akatangaza kulilaani bonde hilo na kuliita bonde la mauti (Yeremia 19:3-9)

NOTE: wana akiolagia (archaeologists) waliweza kugundua mabaki (kuanzia 1907) ya watoto waliokufa kwa kuchomwa moto eneo hilo, hivyo sio hadithi bali ni historia. Baada ya wa Israeli kurudi kutoka utumwani Babeli (Babilon, mabaki yake yapo Iraq ya leo) waliendelea kuliona bonde hilo kama sehemu yenye laana, hivyo uchafu wote wa jiji la Jerusalem ulikua ukitupwa hapo.

Pia bonde hilo lilikua likiwaka moto mchana na usiku ili kuteketeza uchafu uliotupwa, mizoga ya wanyama (vibudu) na wahalifu waliouawa kwa hukumu ya kifo jijini ambao hawakua na wa mtu wa kuwazika ilitupwa bondeni pia, na baadhi ya miili hiyo haikuporomoka mpaka bodeni chini bali ilikwama kwenye miamba ya mteremko wa kuelekea bondeni na kuoza taratibu huku tai na funza wakiila taratibu ili moto usuzime wakati huo waliku wanatumia unga wa sulphur kuukoleza huo moto.

Katika biblia watumishi wa Mungu na hata Yesu walikua wanatumia mfano wa bonde hilo (Jehanamu) kufananisha na uharibifu wataokumbana nao waovu wote baada ya hukumu ya Mungu.

Ge-Hinnom.jpg

Jehanamu, kama inavyo onekana mwaka 1900

Valley_of_Hinnom.jpg

Jehanamu, kama inavyo onekana mwaka 1948

Valley_of_Hinom_PA180090.JPG

Jehanamu, kama inavyo onekana mwaka 2007
 
Mashahidi wa YEHOVA wamejitahidi sana kuelezea ukweli huo lkn ukinzani ni mkubwa mno kutoka kwa baadhi ya madhehebu.
Ukweli ni kama alivyo Eleza mtoa post jehanamu ipo toka zamani hapa duniani.
 
Back
Top Bottom