Kwa wengi ukisema Jehanamu basi picha inayowajia ni sehemu ya mateso ambamo wenye dhambi wote watatupwa baada ya hukumu, lakini ukweli ni tofauti kabisa. Neno Jehanamu lina tafsiriwa kwenye biblia ya kiswahili kutoka nen0 la ki-ebrania "Gehinnom", neno gehinnom lina maana "bonde la Hinnom" yaani "the valley of Hinnom".
Sasa ni kwanini jehanamu (bonde la Hinnom) imekua ikidhaniwa kua ni sehemu ya mateso baada ya kifo? Katika historia bonde hili lipo upande wa kusini magharibi nje ya ukuta wa jiji la kale la Jerusalem, waflme wa Yudea baada ya kuasi kutoka kwa Mungu wa Israeli na kuanza kuabudu Mungu baal (baali) waliwatoa sadaka watoto wao kwa kuwachoma moto wakiwa hai katika bonde hilo, hivyo Mungu wa Israeli akatangaza kulilaani bonde hilo na kuliita bonde la mauti (Yeremia 19:3-9)
NOTE: wana akiolagia (archaeologists) waliweza kugundua mabaki (kuanzia 1907) ya watoto waliokufa kwa kuchomwa moto eneo hilo, hivyo sio hadithi bali ni historia. Baada ya wa Israeli kurudi kutoka utumwani Babeli (Babilon, mabaki yake yapo Iraq ya leo) waliendelea kuliona bonde hilo kama sehemu yenye laana, hivyo uchafu wote wa jiji la Jerusalem ulikua ukitupwa hapo.
Pia bonde hilo lilikua likiwaka moto mchana na usiku ili kuteketeza uchafu uliotupwa, mizoga ya wanyama (vibudu) na wahalifu waliouawa kwa hukumu ya kifo jijini ambao hawakua na wa mtu wa kuwazika ilitupwa bondeni pia, na baadhi ya miili hiyo haikuporomoka mpaka bodeni chini bali ilikwama kwenye miamba ya mteremko wa kuelekea bondeni na kuoza taratibu huku tai na funza wakiila taratibu ili moto usuzime wakati huo waliku wanatumia unga wa sulphur kuukoleza huo moto.
Katika biblia watumishi wa Mungu na hata Yesu walikua wanatumia mfano wa bonde hilo (Jehanamu) kufananisha na uharibifu wataokumbana nao waovu wote baada ya hukumu ya Mungu.
View attachment 608497
Jehanamu, kama inavyo onekana mwaka 1900
View attachment 608498
Jehanamu, kama inavyo onekana mwaka 1948
View attachment 608499
Jehanamu, kama inavyo onekana mwaka 2007