Gharama za kujenga reli SGR zitarudi baada ya muda gani kabla ya faida?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,313
12,613
Kuwa na reli ya kisasa inayokwenda kasi ni jambo la kiunchumi na kijamii/huduma. Lakini kutokana na hali yetu ya kiuchumi kuwa sio nzuri linafaa liwe la kiuchumi zaidi kuliko kihuduma. Yaani reli ya SGR lazima ituongezee mapato kuliko tutoa huduma, maana tanzania hatujaifikia luxury hiyo.

MaSwali ninalowauliza wachumi wetu juu ya mradi huu mkubwa ni:

1. Je, reli ya SGR itaanza inakadiriwa kuanza kutupatia faida baada ya muda gani punde itakapoanza kazi? yaani baada ya kuondoa/kurejesha gharama za ujenzi wake?

2. Je, mipango ya kuwaelimisha mwenye Malori na mabasi yaliyokuwa yanabeba mizigo na abiria kupitia njia hiyo ikoje?

3. Serikali tutakosa kodi kiasi gani kutoka kwenye mabasi na malori yatakayokosa abiria na mizigo kutokana na uwepo wa reli ya SGR?
 
Kwa akili kama hizi sidhan kama tutaendelea

Kwa io gharama za kujenga hostel nzur za kisasa za udom zitarud lini maana watanzania hatujazoea kuish quality places like that na vipi kuhusu watu wanaokosa wateja kwenye nyumba za kupanga na hivyo kuikosesha serikali mapato?

Baadhi ya vitu huwa tunaangalia tu faida kwa sabab hasara tunaweza ishi nazo.
 
Miradi hyo ndo imewapa tabu watanzania. Piga chini haraka Sana, iishie Dodoma
 
Kama Rais Samia atang'ang'ana na mirada yote ya Mh. Magufuli rip kama ilivyo anakumbana na lawama nyingi sana kutoka kwa wananchi. Maana hata Mh. Magufuli aliachana na baadhi ya miradi ya watangulizi wake kama vile BRN, Kilimo kwanza, bandari ya bagamoyo, nk ili isimchelewesha kwenye miradi yake.

Hivyo hata rais Suluhu asione aibu kuiacha baadhi ya miradi hiyo kwa sasa kama vile ile ya ujenzi wa hospitali kubwa chato, kujenga viwanja vikubwa na Ikulu dodoma ili isije kumchelewesha kwenye mipango yake. Aangalie zaidi mambo yaliyoko kwenye ilani ya CCM ya uchaguzi.

Ahakikishe kuwa vjiji vyote vinapata umeme na maji na amalizie mchakato wa uandikaji wa katiba mpya ambayo ilikwamia mikononi mwake akiwa naibu mwenyekiti wa tume ya katiba
 
Sidhani kama utapata taarifa kamili ya gharama za SGR, maana ni moja ya miradi amabyo ilifanyika kwa nguvu ya mtu mmoja tu. Hakukua na common ground kwenye majadiliano ya kuanzisha miradi hii.

Naamini miradi mingi aliyoanzisha JPM itakufa kibudu maana siri na gharama zote za miradi hiyo ameondoka nazo na bahati mbaya hakutaka taarifa hIzo zijulikane na kila Mtanzania.
 
Kuwa na reli ya kisasa inayokwenda kasi ni jambo la kiunchumi na kijamii/huduma. Lakini kutokana na hali yetu ya kiuchumi kuwa sio nzuri linafaa liwe la kiuchumi zaidi kuliko kihuduma. Yaani reli ya SGR lazima ituongezee mapato kuliko tutoa huduma, maana tanzania hatujaifikia luxury hiyo.

MaSwali ninalowauliza wachumi wetu juu ya mradi huu mkubwa ni,

1. Je, reli ya SGR itaanza inakadiriwa kuanza kutupatia faida baada ya muda gani punde itakapoanza kazi? yaani baada ya kuondoa/kurejesha gharama za ujenzi wake?

2. Je, mipango ya kuwaelimisha mwenye Malori na mabasi yaliyokuwa yanabeba mizigo na abiria kupitia njia hiyo ikoje?

3. Serikali tutakosa kodi kiasi gani kutoka kwenye mabasi na malori yatakayokosa abiria na mizigo kutokana na uwepo wa reli ya SGR?
Serikali huwa haiwekezi kwa minajili ya kupata faida bali kuwaletea wananchi wake faida na huduma karibu. Haya hebu niambie wewe na familia yako uko bize kuwalisha, kuwasomesha unategemea kupata faida gani na kwa muda gani maana by the time wanaanza kujitegemea wewe utakuwa na miaka sio chini ya 10 kuishi
 
Kwa akiili kama hiz sidhan kama tutaendelea
Kwa io gharama za kujenga hostel nzur za kisasa za udom zitarud lini maana watanzania hatujazoea kuish quality places like that na vipi kuhusu watu wanaokosa wateja kwenye nyumba za kupanga na hivyo kuikosesha serikali mapato ?

Baadhi ya vitu huwa tunaangalia tu faida kwa sabab hasara tunaweza ishi nazo
Watanzania wengi bado wanahangaikia wingi (quantity) sio ubora (quality) Shule/chuo ni uwekezaji usio na j
Sidhani kama utapata taarifa kamili ya gharama za Sgr ,maana ni moja ya miradi amabyo ilifanyika kwa nguvu ya mtu mmoja tu. Hakukua na common ground kwenye majadiliano ya kuanzisha miradi hii
Naamini miradi mingi aliyoanzisha Jpm itakufa kibudu maana siri na gharama zote za miradi hiyo ameondoka nazo na bahati mbaya hakutaka taarifa hIzo zijulikane na kila mtanzania.
Lakini waziri na wahasibu si wamebaki? Tutafanya uhakiki wa miradi kwanza kabla ya kuendelea nayo. Hata yeye alianza kwa kufanya uhakiki wa miradi ya JK kabla ya kuendelea nayo na iko mingine iliyosmell rat aliiacha.
 
Serikali huwa haiwekezi kwa minajili ya kupata faida bali kuwaletea wananchi wake faida na huduma karibu. Haya hebu niambie wewe na familia yako uko bize kuwalisha, kuwasomesha unategemea kupata faida gani na kwa muda gani maana by the time wanaanza kujitegemea wewe utakuwa na miaka sio chini ya 10 kuishi
Madhumuni ya SGR ni biashara zaidi, yaani tusafirishe bidhaa kwa wingi kwenda na kutoka ziliko huku TRA ikikusanya kodi. Hivyohivyo kwa ununuzi wa ndege lengo lake kuu sio kiwapa raha watanzania bali kupata fedha kupitia nauli na utatilii. Wewe unataka kuwapotosha watu juu ya malengo ya miradi hii mikubwa. Hata mradi wa umeme malemgo yake zaidi ni ya kibiashara kwenye viwanda na kuuza nje ili tupate fedha za kuwahudumia wananchi.

Mambo ya uongouongo kwenye taifa sio mazuri. Iko miradi ambayo ni hasara kwa taifa kama TAZARA, machinga complex, ndege, na sasa nina mashaka na SGR
 
Kama unataka ujenge nipm mkuu nikupe muongozo...

Siasa mbaya Sana
Kila mradi lasima ufanyiwe cost benefit analysis kabla ya kutekelezwa wala sio maswala ya siasa. Ni Wewe tu inawezekana hujui gharama na faida za mradi wacha wenye majibu wanipe, wewe kila mtu anaehoji basi ni siasa anastahili kupotezwa ikibidi.
 
Madhumuni ya SGR ni biashara zaidi, yaani tusafirishe bidhaa kwa wingi kwenda na kutoka ziliko huku TRA ikikusanya kodi. Hivyohivyo kwa ununuzi wa ndege lengo lake kuu sio kiwapa raha watanzania bali kupata fedha kupitia nauli na utatilii. Wewe unataka kuwapotosha watu juu ya malengo ya miradi hii mikubwa. Hata mradi wa umeme malemgo yake zaidi ni ya kibiashara kwenye viwanda na kuuza nje ili tupate fedha za kuwahudumia wananchi.

Mambo ya uongouongo kwenye taifa sio mazuri. Iko miradi ambayo ni hasara kwa taifa kama TAZARA, machinga complex, ndege, na sasa nina mashaka na SGR
Kwa hiyo mkuu unaona kwa vile sgr haina faida basi imekosewa kujengwa. Narudia tena serikali haijengi miundombinu kwa ajili ya kupata faida. Niambie hospitali, barabara, shule, serikali inapata faida gani. Sawa rwli imejengwa kwa ajili ya kufanya biashara na mataifa ya landlocked lakini imejengwa kwa asababu ya kurahisisha watu kufanya biashara kati ya dar na kwingineko
 
Kuna miradi mingi tundege zimenunuliwa kwa gharama kubwa sana na wengi wakawa wanahesabu ni abiria wangapi wanasafiri na ndege ndo hela zirudi. Ila wanasahau ndege zinaleta watalii, zinapeleka wafanya biashara nje serikali inafaidika na kodi, na hiyo movement inasaidia wanufaika indirect mf watalii watanunua vinyago nk
 
Kwani ndege zetu zinafika huko watalii wanakotoka?
 
Kwa hiyo mkuu unaona kwa vile sgr haina faida basi imekosewa kujengwa. Narudia tena serikali haijengi miundombinu kwa ajili ya kupata faida. Niambie hospitali, barabara, shule, serikali inapata faida gani. Sawa rwli imejengwa kwa ajili ya kufanya biashara na mataifa ya landlocked lakini imejengwa kwa asababu ya kurahisisha watu kufanya biashara kati ya dar na kwingineko
Ili uone sgr imekosewa au haijakosewa kujenhwa lazima upembuzi wa faida na hasara zake ufanywe kitaalamu. Mfano, machinga complex imejengwa kwa faifa au hasara? Je, fedha za kujenga lile jengo zilikosa mradi mwingine wenye manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi? Viko vijiji ambavyo hata maji ya kunywa havina kwani vipaumbele vinawatambuka kila mwaka kwa miaka 60 ya uhuru?

Reli ya tazara ililenga ukombozi wa afrika zaidi kuliko huduma kwa watanzania, reli inapita maporini tu kwenda Zambia
 
Kila kitu litakua sawa...
Tuwe na imani, lakini tuwe na tahadhari pia. Sio dhambi tukafanya uhakiki ili tujielekeze kwenye vipaumbele vile vyenye tija kwa taifa badala ya utashi binafsi, ukanda au ukabila.
 
Back
Top Bottom