Reli ya TAZARA taabani

wakikosi

JF-Expert Member
Feb 28, 2015
1,354
1,483
Usafirishaji wa mizigo, abiria pamoja na utoaji wa huduma kwenye reli ya TAZARA ni kama umekufa au upo kwa kiwango cha chini sana.

Lengo la Mwl Nyerere kujenga reli ya TAZARA ilikuwa kurahisisha utoaji wa huduma za Usafiri wa binadamu na mizigo baina ya Tanzania na nchi ya Zambia lakini hadi mwaka huu wa 2023 huduma hiyo ipo taabani.

Mizigo ndio kama haisafirishwi kabisa kwenye reli hiyo na sasa malori ya wafanyabiashara ndiyo husafirisha mizigo kwenda Zambia.

Hii inanipa wasiwasi mkubwa hata hii treni SGR inayojengwa baina ya Dar-Moro,kisha Dodoma-Tabora hadi mwanza na kigoma haitakuwa na mwisho mzuri maana serikali yetu inaendeshwa na wafanyabiashara wakubwa ndio hao wa malori ya mizigo,hawapo tayari kuona reli inafanyakazi na malori yao pamoja na mabasi yao ya kusafirisha abiria yakikosa kazi.

Wabongo watafanya lolote ile reli hiyo ya standard gauge kukosa ufanisi na hatimae itakufa kama reli ya TAZARA.

KAMA NCHI NI KAMA TUNALAANA FULANI HIVI TUSIPATE MAENDELEO.

Ukiwa unafikiria vizuri kuwa mtanzania ni maumivu sana
 
Kusafirisha mizigo kwa njia ya Reli ni gharama ndogo sana harafu usalama wa mzigo kufika ni mkubwa sema Watanzania wengi hawapendi kusafirisha kwa njia ya Reli kutokana na kutokua na uhakika wa mzigo kufika kwa wakati hawachelewi kutoa taarifa diesel imekata Makambako wanasubiri itoke daslm ndio treni ya mzigo ianze safari kwa Wafanyabiashara hiyo ni ngumu hakuna anahujumu treni wasimamizi wanafanya kazi chini ya kiwango na kusingizia wasiohusika...
 
Sijawahi kuelewa jinsi mipango ya nchi hii inavyotekelezwa. Kuna kipindi reli ya Dar to Arusha iliachwa ikafa kifo cha mende.

Reli ya Tazara, reli ya kati na reli ya kwenda MPANDA zote ziko hoi. Badala ya kuja na mpango kabambe wa kuzifufua na kuzijenga upya hizi reli na baadae kununua vichwa na mabehewa (ya abiria na mizigo) mapya na mengi wao eti wamekimbilia Reli mpya ya umeme!!

Reli imara hata kama ni treni za diesel unakuta zina uwezo wa kuvuta mpaka wagons 50 kwa mpigo, je kwa uwezo huo wangebeba abiria na mizigo mingapi??L

eo nimeona Azam Tv TRC kubeba tuu abiria kwa kutumia mabehewa hata ya zamani hawawezi, yaani wameshindwa kukarabati behewa za zamani walau 30 zibebe abiria kuanzia saa 10 alfajiri kutoka Pugu kuja Dar kweli?
 
Nchi zetu za kiafrika huwa zinatakiwa kupata viongozi wababe na wabishi ili kufikia pale panapotakiwa.

Alikuwepo mwamba hapa, leo Moro - Dar mngekuwa mnatereza tu ila sasa mkampiga mawe na kila aina ya maneno ili aonekane fedhuri na mkafanya yenu dhidi yake.

Ila jana na leo kila mtu analia vile wanaona haibu kusema ukweli ila nafsi zinawasuta!.
 
Watu wanaihijumu reli hiyo tena wengine wana biashara ya kusafirisha mizigo wapo bungeni. Bi mkubwa hasipo kaza hii SGR haitoisha, zitakuwa stori na haita ikiisha still haita fanya kazi kama ilivyo kusudiwa.
 
Back
Top Bottom