Gharama ya ziara ya Prof Muhongo Mkoani Mara ni kufuru

Gharama ya ziara ya Prof Muhongo Mkoani Mara ni kufuru

Huyu fisadi wa escrow Sospeter Muhongo hadi atakapofukuzwa kwenye hiyo wizara atakuwa amemaliza kila kitu. JK amekuwa BLACKMAILED hawezi kufanya kitu kwa vile wameiba wote. Ila huyu mzee mwongo asipojiangalia atapigwa mawe kama wezi wa kuku...
 
jk anatufanyia uhuni wa tz. mtu anatuhumiwa afu anapiga job na kuendelea kutumia fedha za uma.
 
Gari ya polisi kuvishwa matairi 4 nao ufisadi.
kujazwa mafuta ya kucover km zote alikopita ni ufisadi.
watu kulipwa posho kwa ziara yote sh laki tano ufisadi,hiyo laki tano ukiigawa kwa siku za ziara unakuta perday wamepewa labda elfu tano tano.

sasa mwandishi unamtoaje dar mpaka huko vijijini na usimpe pesa ya kujikimu?.
hii habari ni pointless.
Haya ni matumizi mabaya ya resources, polisi kumi wote wanamlinda Sospeter kwa lipi hasa!?
 
Fisadi mkubwa huyu Muongo na cha ajabu kateua mpaka wajumbe Wa bodi Tanesco
 
Muhongo kesha juwa ulaji wa bongo, sasa anajipanga kuchukua jimbo. Anataka aingie mjengoni kupitia jimbo siyo "viti maalumu" tena.
 
Gari ya polisi kuvishwa matairi 4 nao ufisadi.
kujazwa mafuta ya kucover km zote alikopita ni ufisadi.
watu kulipwa posho kwa ziara yote sh laki tano ufisadi,hiyo laki tano ukiigawa kwa siku za ziara unakuta perday wamepewa labda elfu tano tano.
sasa mwandishi unamtoaje dar mpaka huko vijijini na usimpe pesa ya kujikimu?.
hii habari ni pointless.

fedha za faini barabarani zinaenda wapi?
wizara ya mambo ya ndani inapowakilisha bajeti huwa wanaweka mafuta,matairi, service na mengineyo. hapo ndipo ilipoonyesha kuwa hakwenda kikazi. maana kama ingekuwa hivyo angepata ulinzi bila hivyo vikwazo. na pia kama wewe ni waziri na unajiamini kwa nini uchukue polisi?
 
Musumwonee wivu Prof. Muhongo. Hizo hela huwa zinawekwa kwenye bajeti na kupitishwa na Wahe. Wabunge wetu. Prof. Ni Jembe. Chapa kazi Prof. achana na wenye chuki binafsi.
 
fedha za faini barabarani zinaenda wapi?
wizara ya mambo ya ndani inapowakilisha bajeti huwa wanaweka mafuta,matairi, service na mengineyo. hapo ndipo ilipoonyesha kuwa hakwenda kikazi. maana kama ingekuwa hivyo angepata ulinzi bila hivyo vikwazo. na pia kama wewe ni waziri na unajiamini kwa nini uchukue polisi?
Angeenda kikazi ndo gari ingevalishwa matairi?.tuseme hiyo gari ina matairi mabovu kwa ajili ya parking na huvishwa mengine kwa kazi,kama ndivyo mtatuvunjia migongo mafundi makanika kwa kuvisha na kuvulisha matairi.
ishu hapa gari ilikua na matairi kipara na wameweka mapya ambayo baada ya ziara yataendelea kutumika kwa faida ya wananchi.
 
hapana Mkuu. Muhongo yupo sahihi kwa vile adui wake Reginald Mengi ametoa fedha nyingi kwa ajili ya watu watakaofanikisha kukatwa kichwa cha profesa muhongo. Taarifa zipo

Tulichosikia wenyewe ni Kundi la Muhongo wakiongozwa na werema kutaka kukata kichwa cha Kafulila na si vinginevyo. Haya mengine majungu ya kawaida tu ya watumwa wa nape
 
Hana wa kumunini? Ikifika tarehe 15 bado ni waziri utanipa namba niitumia 50000. Ni anamalizia muda wake wa uwaziri.
Mamdenyi deal hiloo,umepata utaongeza kwenye mtaji wa kuku wa vifaranga.
 
yericko nyerere umesema ni taarifa za kiuchunguzi lakini hukumalizia kuwa ni taarifa za kiuzushi. Profesa haombi gari kwa mdomo bali barua inaandikwa na polisi hawajibu kwa mdomo bali wanajibu kwa maandishi. Pesa za umma zinatolewa kupitia maombi katika dokezo sabili na kisha vocha ya malipo huandaliwa . na posho ya serikali ina viwango kwa ngazi za maafisa. ambazo ni kati ya sh 65,000 na 80,000. sasa unataka kutufanya sisi watoto tuamini upuuzi wako bila aibu unasema uongo usio na mashiko.na wanaoandaa ziara ni maafisa wa wizara kwa hiyo kama wao wamedai kulipa posho ya shilingi laki 5 kwa siku bila shaka wanayo orodha ya waliosaini kupokea posho hiyo..tupia nyaraka zoote hizo ili tukuamini. Muongo mkubwa wewe
Kwa mujibu wa taarifa za kiuchunguzi katika ziara ya dalali wa wezi nchini Prof Muhongo kumebainika ufujaji mkubwa katika wizara hiyo kwa ziara ya waziri huyu katika sherehe za krismasi na mwaka mpya.

Kwa upande wa taarifa zilizonaswa ndani ya jeshi la Polisi mkoani Mara nikuwa katika kibali cha tarehe 24 Dec gate pass number 1776857, Muhongo aliomba ulinzi toka jeshi la polisi kisha akaambiwa jeshi halina mafuta ya mchezo mchafu, kuona hivyo Muhongo akaamua kugharimia mafuta na matengenezo ya magari ya polisi na kuwalipa polisi wote atakaoambatana nao katika ziara yake.

Nyaraka zinaonyesha jeshi la polisi lilikabidiwa mafuta ya dizeli lita mia tisa (900) kwaajili ya magari mawili yaliyokuwa yakiongoza msafara huo, Matairi manne mapya kwa ajili ya gari aina ya Toyota Land cruiser, T 381 BQP, Blue ya Polisi.

Malipo hayo yamefanyoka Central store ya Musoma power station, Gate keeper anaitwa Musa anakiri kupitisha, maana ni order ya wizara, Escort ya magari mawili na askari kumi walilipwa posho zao laki tano kwa siku kila mmoja. Pia Waandishi wa habari Kasoro wa IPP media, walilipwa laki Tatu kwa kila Mwandishi wa siku kwa kila story nzuri iliyotoka, Blogger pia walialikwa.

Kula na kulala kwa wote ilikuwa juu ya wizara(Muhongo.

Musoma walikaa Penisula hotel, Tarime walikaa Goldland Hotel, Serengeti walikaa Giraffe hotel, Butiama na Bunda walienda na kurudi.

Hoja ya msingi nikuwa gharama hizi zinatoka katika bajeti ipi pale wizarani??
 
Prof Muhongo alisema " Siku nikifukuzwa kazi, ardhi ya Tanzania itapasuka".

Anajiamini nini huyu Prof?
 
Hiv watanzania kama tuweza kuamini tarifa ambazo hazina chanzo kwa sababu zinamhusu mtu labda ambaye umtaki, Hivi tunajenga Tanzania au tujenga vyama vya siasa?
 
Mtamchafua sana ila.jembe linaendelea kupiga kazi. Tupo watanzania tunaoelewa kuwa mnafanya.siasa za.majitaka zisizo na.mashiko.
 
Sheikh Yahya upo kazini unztabiri! Mshukuru mtoa taarifa kwa taarifa aliyokujulisha na siyo kumtaka akafanye kazi ya kufuatilia hayo maswali yako! Kama unataka iamini taarifa yake, kama hutaki baki hivyo hivyo! Na ukitaka taarifa zaidi idai serikali yako sikivu ikupe wakwambie lengo na mrejesho wa hiyo ziara ya propesa muongo dalali
Mkuu unaonekana kuwa na jazba, siyo sahihi hata kidogo, hili ni jukwaa la kubadilishana mawazo na kupeana taarifa. Sina ugomvi na mtu anayetoa taarifa za ubadhilifu wa kodi za watanzania hata kidogo. Nina ugomvi na mtu anayeleta taarifa kwa sababu tu kakosa dili. Uzoefu unaonyesha watu wengi wanatibua baada ya madili yao kuharibika. Kama ameleta kwa nia njema kabisa (siyo kwa vile yeye au mtu wake kakosa) tunampongeza na tunamshukuru ila kama limegoma ndo akalitibua si sawa hata kidogo.

Lakini kama amepata uwezo wa kupata habari kama hizo (ambazo mimi naona ni ngumu kuzipata), hawezi kupata majibu ya maswali yangu? Ni vizuri tuangalie pia ziara yake imekuwa na manufaa gani pia siyo kuangalia tu kwamba kafuja pesa, tuangalie pande zote. Kama hawezi kujua alikwenda wapi, kufanya nini na matokeo ya ziara yake, jibu ni rahisi tu kwamba sikufanikiwa kujua au nafuatilia, nikifanikiwa nitawaletea. Punguza jazba ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom