Gharama ya ziara ya Prof Muhongo Mkoani Mara ni kufuru

Gharama ya ziara ya Prof Muhongo Mkoani Mara ni kufuru

Ndo maana anaomba alindwe na polisi kila anapoenda anajua atachezea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali

Weka picha.akilindwa na polisi. Na.kale kavideo kenu feki.ka kutengeneza pelekeeni watoto
 
kwangu mimi napata shida kidogo kwa nini kaka mkubwa anaendelea kumshikilia huyu prof. kwenye comment yangu ya kwanza nilisema ya kuwa kuna siri gani hasa kwenye suala la hili la escrow? kiukweli tunaomba mkuu wa kaya atende haki kama alivyofanya kwa wengine wote kwani kutofanya maamuzi katika suala la huyu jamaa kunatupa picha ambayo yeye mwenyewe anaweza kuwa ni sehemu ya sakata hilo
........inasemekana ndio ameshatenda haki tayari..prof Muhongo hana kosa ndio maana kaachwa aendelee na kazi
 
hapana Mkuu. Muhongo yupo sahihi kwa vile adui wake Reginald Mengi ametoa fedha nyingi kwa ajili ya watu watakaofanikisha kukatwa kichwa cha profesa muhongo. Taarifa zipo

Kwanini msiende kumkamata Mengi au mnamuogopa inabidi mumlinde Muongo?
Tanzania bana
 
JK alisema pesa za escrow siyo za umma ni za IPPTL ndo maana Muhongo anatumia gharama za kufuru kwa sababu anajua hakuna mwenye uwezo wa kumgusa kama raisi mwenyewe ameogopa kumfukuza nani atamuweza tena .utawala wa shetani unakaribia kuisha.
 
Kwa mujibu wa taarifa za kiuchunguzi katika ziara ya dalali wa wezi nchini Prof Muhongo kumebainika ufujaji mkubwa katika wizara hiyo kwa ziara ya waziri huyu katika sherehe za krismasi na mwaka mpya.

Kwa upande wa taarifa zilizonaswa ndani ya jeshi la Polisi mkoani Mara nikuwa katika kibali cha tarehe 24 Dec gate pass number 1776857, Muhongo aliomba ulinzi toka jeshi la polisi kisha akaambiwa jeshi halina mafuta ya mchezo mchafu, kuona hivyo Muhongo akaamua kugharimia mafuta na matengenezo ya magari ya polisi na kuwalipa polisi wote atakaoambatana nao katika ziara yake.

Nyaraka zinaonyesha jeshi la polisi lilikabidiwa mafuta ya dizeli lita mia tisa (900) kwaajili ya magari mawili yaliyokuwa yakiongoza msafara huo, Matairi manne mapya kwa ajili ya gari aina ya Toyota Land cruiser, T 381 BQP, Blue ya Polisi.

Malipo hayo yamefanyoka Central store ya Musoma power station, Gate keeper anaitwa Musa anakiri kupitisha, maana ni order ya wizara, Escort ya magari mawili na askari kumi walilipwa posho zao laki tano kwa siku kila mmoja. Pia Waandishi wa habari Kasoro wa IPP media, walilipwa laki Tatu kwa kila Mwandishi wa siku kwa kila story nzuri iliyotoka, Blogger pia walialikwa.

Kula na kulala kwa wote ilikuwa juu ya wizara(Muhongo.

Musoma walikaa Penisula hotel, Tarime walikaa Goldland Hotel, Serengeti walikaa Giraffe hotel, Butiama na Bunda walienda na kurudi.

Hoja ya msingi nikuwa gharama hizi zinatoka katika bajeti ipi pale wizarani??


Mtahangaika sana mwaka huu.MWAMBIENI MKURUGENZI WA IPP MWAKA HUU ATAKONDA SANA ukweli ndio huo ingawa ni NGUMU KUMEZA.
 
Watu kama akina yericko nyerere wanapaswa kuangaliwa kwa makini sana kwani ni wazushi wakubwa sana na wanatunga uongo usio na mashiko. Kwanza posho ya laki tatu au laki tano kwa siku haipo, pili hoteli wanazolala ni za hadhi ya nyota tatu au nne kwa hiyo ni sawa wakilala huko, lakini uongo wa fungua mwaka ni huu wa kwamba profesa alitoa dizeli na matairi ya magari wakati kuna taratibu za manunuzi ya umma ambayo yanafuatwa kwa kupokea vifaa. sasa yericko angekuwa mkweli angetupia dokezo sabili la kuomba ulinzi, majibu ya polisi, vocha ya malipo iliyotoa hizo hela za dizeli na pia vocha walizosaini hao waandishi ...
 
Pia Waandishi wa habari Kasoro wa IPP media, walilipwa laki Tatu kwa kila Mwandishi wa siku kwa kila story nzuri iliyotoka, Blogger pia walialikwa.

Mtahangaika sana mwaka huu.MWAMBIENI MKURUGENZI WA IPP MWAKA HUU ATAKONDA SANA ukweli ndio huo ingawa ni NGUMU KUMEZA.

Naona shida iko hapa kwenye posho! Huyo wa IPPMedia si amevuta za kutosha kuto kwa Mzee Mengi?
 
Watu kama akina yericko nyerere wanapaswa kuangaliwa kwa makini sana kwani ni wazushi wakubwa sana na wanatunga uongo usio na mashiko. Kwanza posho ya laki tatu au laki tano kwa siku haipo, pili hoteli wanazolala ni za hadhi ya nyota tatu au nne kwa hiyo ni sawa wakilala huko, lakini uongo wa fungua mwaka ni huu wa kwamba profesa alitoa dizeli na matairi ya magari wakati kuna taratibu za manunuzi ya umma ambayo yanafuatwa kwa kupokea vifaa. sasa yericko angekuwa mkweli angetupia dokezo sabili la kuomba ulinzi, majibu ya polisi, vocha ya malipo iliyotoa hizo hela za dizeli na pia vocha walizosaini hao waandishi ...

... Mkuu, Wewe Ni Msemaji Wa Muhongo?
 
yericko nyerere umesema ni taarifa za kiuchunguzi lakini hukumalizia kuwa ni taarifa za kiuzushi. Profesa haombi gari kwa mdomo bali barua inaandikwa na polisi hawajibu kwa mdomo bali wanajibu kwa maandishi. Pesa za umma zinatolewa kupitia maombi katika dokezo sabili na kisha vocha ya malipo huandaliwa . na posho ya serikali ina viwango kwa ngazi za maafisa. ambazo ni kati ya sh 65,000 na 80,000. sasa unataka kutufanya sisi watoto tuamini upuuzi wako bila aibu unasema uongo usio na mashiko.na wanaoandaa ziara ni maafisa wa wizara kwa hiyo kama wao wamedai kulipa posho ya shilingi laki 5 kwa siku bila shaka wanayo orodha ya waliosaini kupokea posho hiyo..tupia nyaraka zoote hizo ili tukuamini. Muongo mkubwa wewe

Acha kukariri wewe, huo ni utaratibu unavyotakiwa kuwa. Lakini serikali yako hii haifuati huo utaratibu mrefu na mgumu. Fisadi hana muda huo, anapiga shortcut tu. Nyie wa vijiofisi vya chini huku ndo mmewekewa huo mlolongo ili msiibe kama wao!
 
uongo mwingine huo
Acha kukariri wewe, huo ni utaratibu unavyotakiwa kuwa. Lakini serikali yako hii haifuati huo utaratibu mrefu na mgumu. Fisadi hana muda huo, anapiga shortcut tu. Nyie wa vijiofisi vya chini huku ndo mmewekewa huo mlolongo ili msiibe kama wao!
 
Nafikiri jibu muafaka linapatikana hapa;

  • Waziri Mkuu Pinda: Wezi wana nguvu, serikali ikiwachukulia hatua nchi itayumba!
  • Waziri Prof. Muhongo: Sijiuzulu, nikilazimishwa kung'oka, nchi itatikisika!
Matokeo yake mwizi anazidi kutanua...naam, taifa liko mikononi mwa wezi! Nani arushe jiwe?
 
sasa yericko angekuwa mkweli angetupia dokezo sabili la kuomba ulinzi, majibu ya polisi, vocha ya malipo iliyotoa hizo hela za dizeli na pia vocha walizosaini hao waandishi ...
unajifanya mjuaji kumbe giza mpaka ubongo,toka lini mchukua pesa akasaini kwenye vocha,unadhani ni lazima vocha iwe ya mafuta?hasa kwa mtu anayetaka kukiuka taratibu!
 
Hbari hii naweza itizama kwa mitazamo miwili. Kwanza, iweje jeshi la polisi liombwe ulinzi na lidai halina mafuta ya mchezo mchafu. Kama waziri anajibiwa hivi basi raia tuna kazi , kwani ili upate ulinzi lazima utoe gharama za ulinzi na ndio maana polisi hutumika vibaya kwani hulazimika kucheza ngoma za watu hao bila kujali taaluma yao.

Pili sasa inaonekana Muhongo hakuna wa kumuambia chochote baada ya Kikwete kumshindwa, hivyo hela ya umma anatumia atakavyo kwani hakuna wa kumuuliza. Na Kikwete akithubutu tu ataumbuka vibaya. Halafu lita mia tisa za mafuta(Dizeli) hawa nadhani walikuwa wanatoka Mara kwenda South Afirca kwani hayo ni mafuta mengi sana
 
... Yeriko Nyerere Nimekukubali, We Uko Njema Sana.
 
Angeenda kikazi ndo gari ingevalishwa matairi?.tuseme hiyo gari ina matairi mabovu kwa ajili ya parking na huvishwa mengine kwa kazi,kama ndivyo mtatuvunjia migongo mafundi makanika kwa kuvisha na kuvulisha matairi.
ishu hapa gari ilikua na matairi kipara na wameweka mapya ambayo baada ya ziara yataendelea kutumika kwa faida ya wananchi.



yaani bado hainingii akilini kuwa gari lilikuwa na tairi kipara. inamaana wananchi wangevamiwa polisi wasingekuja kwa kisingizio hicho? shame on you ccm.
 
katika kitu ambaco polisi tanzania wamechemsha ni siri,hawana siri kabisa
 
yaani bado hainingii akilini kuwa gari lilikuwa na tairi kipara. inamaana wananchi wangevamiwa polisi wasingekuja kwa kisingizio hicho? shame on you ccm.
Wangeazima gari kwa mtu yeyote.
gari kuwa na tairi kipara si ajabu sana kwani si matairi huisha bana?
 
Back
Top Bottom