Gharama ya ziara ya Prof Muhongo Mkoani Mara ni kufuru

Kwa mujibu wa taarifa za kiuchunguzi katika ziara ya dalali wa wezi nchini Prof Muhongo kumebainika ufujaji mkubwa katika wizara hiyo kwa ziara ya waziri huyu katika sherehe za krismasi na mwaka mpya.

Kwa upande wa taarifa zilizonaswa ndani ya jeshi la Polisi mkoani Mara nikuwa katika kibali cha tarehe 24 Dec gate pass number 1776857, Muhongo aliomba ulinzi toka jeshi la polisi kisha akaambiwa jeshi halina mafuta ya mchezo mchafu, kuona hivyo Muhongo akaamua kugharimia mafuta na matengenezo ya magari ya polisi na kuwalipa polisi wote atakaoambatana nao katika ziara yake.

Nyaraka zinaonyesha jeshi la polisi lilikabidiwa mafuta ya dizeli lita mia tisa (900) kwaajili ya magari mawili yaliyokuwa yakiongoza msafara huo, Matairi manne mapya kwa ajili ya gari aina ya Toyota Land cruiser, T 381 BQP, Blue ya Polisi.

Malipo hayo yamefanyoka Central store ya Musoma power station, Gate keeper anaitwa Musa anakiri kupitisha, maana ni order ya wizara, Escort ya magari mawili na askari kumi walilipwa posho zao laki tano kwa siku kila mmoja. Pia Waandishi wa habari Kasoro wa IPP media, walilipwa laki Tatu kwa kila Mwandishi wa siku kwa kila story nzuri iliyotoka, Blogger pia walialikwa.

Kula na kulala kwa wote ilikuwa juu ya wizara(Muhongo.

Musoma walikaa Penisula hotel, Tarime walikaa Goldland Hotel, Serengeti walikaa Giraffe hotel, Butiama na Bunda walienda na kurudi.

Hoja ya msingi nikuwa gharama hizi zinatoka katika bajeti ipi pale wizarani??

Alafu mkuu wa nchi ana baki kuchekacheka tu eti nambakiza kiporo,mtu kama huyu hata geti la wizara asingeruhusiwa kuligusa enzi za Nyerere
 
nikweli mkuu nilimsikia konda wa hiace kutoka tarime kuja msma akilalamika eti eeee mungu huyu nimemtazama yule baba hadi nikachoka eti wamekula hela zote zile its true alikua huku musoma
 
hii nchi kila mtu akipata chance apige tu bwana....wakuu wenyewe wanapiga...ikulu nayo inapiga.. acha pige tu..maana walipakodi ni wendawazimu......
 
Prof Muongo pumzika Usilazimishe Watanzania waakupende.....hawakukuchagua kwenye nafasi yoyote ile,
 
Nonsense! soma thread. Angeenda ziara akafanya kazi zake bila hivyo vituko vilivyoelezwa nani angepiga kelele?

Hapo kuna vituko gani? Sijaona kituko chochote as long as anatimiza wajibu wake
 
Prof ana maswahiba wake hizi Pesa zaweza tolewa na chifu kiumbe tu vitu vingine tuwe tunapata hbr za kina.
 
Kwa mujibu wa taarifa za kiuchunguzi katika ziara ya dalali wa wezi nchini Prof Muhongo kumebainika ufujaji mkubwa katika wizara hiyo kwa ziara ya waziri huyu katika sherehe za krismasi na mwaka mpya.

Kwa upande wa taarifa zilizonaswa ndani ya jeshi la Polisi mkoani Mara nikuwa katika kibali cha tarehe 24 Dec gate pass number 1776857, Muhongo aliomba ulinzi toka jeshi la polisi kisha akaambiwa jeshi halina mafuta ya mchezo mchafu, kuona hivyo Muhongo akaamua kugharimia mafuta na matengenezo ya magari ya polisi na kuwalipa polisi wote atakaoambatana nao katika ziara yake.

Nyaraka zinaonyesha jeshi la polisi lilikabidiwa mafuta ya dizeli lita mia tisa (900) kwaajili ya magari mawili yaliyokuwa yakiongoza msafara huo, Matairi manne mapya kwa ajili ya gari aina ya Toyota Land cruiser, T 381 BQP, Blue ya Polisi.

Malipo hayo yamefanyoka Central store ya Musoma power station, Gate keeper anaitwa Musa anakiri kupitisha, maana ni order ya wizara, Escort ya magari mawili na askari kumi walilipwa posho zao laki tano kwa siku kila mmoja. Pia Waandishi wa habari Kasoro wa IPP media, walilipwa laki Tatu kwa kila Mwandishi wa siku kwa kila story nzuri iliyotoka, Blogger pia walialikwa.

Kula na kulala kwa wote ilikuwa juu ya wizara(Muhongo.

Musoma walikaa Penisula hotel, Tarime walikaa Goldland Hotel, Serengeti walikaa Giraffe hotel, Butiama na Bunda walienda na kurudi.

Hoja ya msingi nikuwa gharama hizi zinatoka katika bajeti ipi pale wizarani??

Asilimia kubwa ni UONGO UMEANDIKA.

HAIWEZEKANI ASKARI AKAPEWA posho ya 500000( laki tano kwa siku) labda umeandika kwa hasira maana mwandishi wa IPP hakuruhusiwa katika msafara huo kuandika habari
 
Mara nyingi ukiona mtu anatoa story kama hizi ujue na yeye kuna dili alikuwa amelilenga la kumpa ulaji kwenye hiyo ziara likampita pembeni, kama siyo yeye basi anatumiwa na mtu aliyelenga kunufaika na yeye kapigwa chini. Na inaonekana kuna watu walikuwa wanagombania ulaji kwenye hiyo ziara wakazidiana kete sasa waliokosa wanaamua kuharibu.

Hebu, tusaidie pia ndugu yangu Yericko, lengo la hiyo ziara ilikuwa ni nini? Alilenga kwenda/ alienda wapi na wapi? ni yapi matokeo ya hiyo ziara (matokeo yaliyopatikana au yanayotarajiwa) kwa maendeleo ya taifa letu?

Kwani wewe umekosa dili gani kwa Yeriko hadi unataka kumharibia?
 
Asilimia kubwa ni UONGO UMEANDIKA.

HAIWEZEKANI ASKARI AKAPEWA posho ya 500000( laki tano kwa siku) labda umeandika kwa hasira maana mwandishi wa IPP hakuruhusiwa katika msafara huo kuandika habari

Mwandishi wa IPP hakuruhusiwa kuandika lakini aliambatana naye kwenye ziara hiyo
 
Anakula kwa kukomba mboga akijua muda unahesabika...
 
poleni watanzania mnaotuika hamjui kuwa huo ni utumwa?

mtumikie bwana ili afurahi nafsi yake
 
Back
Top Bottom