Ghana: Wafanyabiashara 5 mbaroni kwa Kuvunja Sheria ya Ulinzi wa Data

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Wafanyabiashara watano huko Accra wamekamatwa na polisi kwa kushindwa kujiandikisha kwenye Tume ya Ulinzi wa Data (DPC) na kuvunja Sheria ya Ulinzi wa Data.

Wafanyabiashara hao ni wawakilishi wa CareFlight Ghana, kampuni inayotoa huduma za kliniki na ambulensi, Embassy Gardens, kituo cha makazi, Shule ya Morning Star, KABFAM Ghana Limited, wafanyabiashara wa vifaa vya umeme, na Kliniki ya Grace Homeopathic.

Wafanyabiashara hao watano walikamatwa wakati wa zoezi la utekelezaji jana na kupelekwa kwenye makao makuu ya polisi kwaajili ya kutoa maelezo ili kuruhusu polisi kuanzisha uchunguzi.

Kulingana na Quintin Akrobotu, Mkurugenzi wa Udhibiti na Ufuatiliaji (Director of Regulatory and Compliance), DPC, wafanyabiashara hao watapandishwa kizimbani.

Kuhusu Careflight, alisema kwamba kampuni ilishindwa kumteua msimamizi wa ulinzi wa data kama ilivyotajwa katika kifungu cha 58 cha Sheria na hawana leseni ya ulinzi wa data, jambo lililokiuka kifungu cha 17.

Alisema kwamba Embassy Gardens na Morning Star School pia walikuwa wakifanya kazi bila leseni ya ulinzi wa data na walipuuza agizo rasmi ya kuwasajili.

Ingawa ilikuwa imesajiliwa na DPC, Bwana Akrobotu alibaini kuwa KABFAM ilikiuka kifungu cha 58 na ilikuwa inavunja kifungu cha 82.

Alisema kwamba Grace Homeopathic Clinic pia haikuwa imesajiliwa na haikuonesha kuwajibika, jambo lililovunja kifungu cha 17.

Bwana Akrobotu alieleza kwamba ilitarajiwa wafanyabiashara wangehakikisha uchakataji wa data ulikuwa chini ya usimamizi na uangalizi wa Tume.

Uvunjaji wa sheria uliojitokeza zaidi, ulikuwa kushindwa kumteua msimamizi wa taarifa, ambaye alipaswa kufundishwa na kupata ithibati.

Bwana Akrobotu alisema kwamba zoezi hilo lingefanyika kila mwezi na kuwahimiza wafanyabiashara wote wanaokusanya na kuchakata data kufata Sheria.

"Tumieni fursa hii kusasisha usajili wenu ikiwa umekwisha muda wake. Kushindwa kuzingatia matakwa ya Sheria ni kosa la jinai, ambalo linawafanya muwe na hatia ya kufunguliwa mashtaka. Basi mfanikishe jambo hilo sasa kabla ya sheria kuwafikia," alisema.

Bwana Akrobotu alibainisha kuwa tume ilikuwa imeanzisha njia za kuelimisha umma kuhusu ulinzi wa data na majukumu yao chini ya Sheria ili kuboresha kuboresha ufatwaji wa sheria.

====

Five more institutions have been picked up for non-compliance with the country’s data protection laws in the latest round of an enforcement action by the Data Protection Commission.

The enforcement exercise is aimed at clamping down on businesses that have failed to register with the Data Protection Commission as data controllers but are processing personal data.

The enforcement exercise was supported by the Ghana Police Service.
The companies accosted were Care Flight Ghana, Embassy Court, Morning Star School, KABFAM and Grace Homeopathic Clinic.

On the breach of section 17 of the Data Protection Act 2012 (Act 843) which requires all companies that manages personal data to acquire a license from the data Protection Commission, Morning Star School, Embassy Gardens, CareFlight Ghana and Grace Homeopathy were cited for breach.

Embassy Gardens and Morning Star School were also cited for non-registration with the commission.

Though Kabfam, one of the companies visited during the swoop had registered with the commission, it was cited for failure to appoint a certified data protection supervisor.

Speaking to Joy Business after the exercise, Director of Regulatory and Compliance at the Data Protection Commission, Quintin Akrobeto, urged businesses to abide by the laws to avoid arrest

“Registration is just one of the aspect of compliance. What we expect from institutions is to bring their activities under the radar of the commission for supervision.”

“For some of the companies, they haven’t registered at all. Even after several follow ups, they have failed to register with the commission. For those of them that have registered, they are still not compliant. You need to appoint a certified supervisor to help guide companies to compliance. “

The exercise is expected to be held monthly to ensure the utmost enforcement of the data protection laws.

All Africa
 
Back
Top Bottom