Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

Hivi wanajeshi wa bongo, mnarundika mibomu kwenye maghala ili iweje???... Na kwanini kwenye maeneo ya makazi ya watu?? Mapori yooote Tanzania mmeyaacha mnaenda kwenye makazi ya watu??? duh!!

Yaani asipostep down mtu, tutaondoka na roho ya mmoja wao we waacha... Kwanza inaonekana walinunua mabomu yaliyoexpire, ili wapate dili la kuchakachua, ona sasa wanavyoingia aibu!!!!! Sé&nzi taip!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!:angry:
 
Hatimae Mabasi yameanza kufanya kazi na watu wanarudi baada ya hali kuwa tulivu kidogo
 
Kwa hiyo watu wanaenda kulala uwanja wa taifa!
Ndio serikali ya JK imewatangazia wafanye hivyo!
Nasikia wanaotoka GmBOTO kwenda u/taifa wanapishana na vibaka wanaokwenda majumbani kulikoachwa bila watu!
 
Hivi Kamanda Kova alipowataka wananchi warejee majumbani kwao alimaanisha nini hasa? Manake nimeshindwa kabisa kumuelewa kusudio lake..

Huyo Jamaa yaani we muache tu maana hata sijui nani huwa anamshauri ktk statement zake
 
Kesho ni PM Time Bungeni na CDM wanamtafutia helicopter Mbowe ambaye yuko jimboni kwake arudi Dom haraka ili ambane huyu PM wa kuchakachua.
 
Usingizi umerudi, Nisubiri utumbo wa kesho:angry::angry::angry:
 
There are currently 1684 users browsing this thread. (320 members and 1364 guests)


Hii rekodi kwa usiku mwingi namna hii ni mara chache kufikiwa!...BTW, waombolezaji na waathirika wengineo, tuko pamoja na nyinyi...hatulali, hadi mrudi majumbani kwenu salama!
 
tuko pamoja na wahanga wa mabomu lakini wakati umefika jeshi lihakiki silaha zake kama zimepitwa na wakati ziharibiwe ili kuepuka madhara makubwa.
 
nasikitika kusikia na ninayoendelea kusikia juu ya mabomu yanayoendelea kulipuka nchini kwetu! sijui kama tunaweza kuamini kama kuna kitengo cha jeshi ambacho kina pokea mshahara kila mwisho wa mwezi na bado wameshindwa kufanya kazi yao. kuna swali bado najiuliza, intelijensia iko wapi?
 
Viongozi inabidi wawajibike hapa.(hasahasa TPDF)

ni kweli sababu sioni sababu za mambo yaliyotokea kurudia. hatujawahi kua na kazi ambayo imewafanya wawe bize namna hiyo..
 
Unajua Jeshi letu sasa hivi linatakiwa kufanya kazi kisomi zaidi. Safety should be a priority.

Baada ya milipuko wa Mbagala wakaamua kukusanya mabomu yote chakavu nchi nzima na kuyaweka pale gongo la mboto kwenye madhala 15 wakisubiri kuyaharibu sijui lini. Hebu fikiria kama yangelipuka maghala yote 15 ingekuwaje? Maana hili lililolipuka ni ghala la tano kimahesabu ambayo huwekwa kutokana na muda wa mabomu tokea yatengenezwe, yaani kuna mabomu mbaka yaliyotekwa kwa Idd Amin.

Kwa kawaida huwa wanamonitor likelihood ya kulipuka kwa ku-test pini za mabomu hayo. Hufanya hivyo kwa kutumia panya maalum, ambao huwekwa kwenye ghala na wakiona panya wamekufa basi ni kuwa kuna pini zimelegea na huenda mabomu yakalipuka muda wowote na kuanza kukagua na kuzi-fix, maada huanza ku- release toxic gas ambayo ndiyo humuua panya. Sasa sisi wabongo kwa mazoea yetu jana na leo waliokuwa zamu hawakufanya hivyo ndiyo haya sasa yametokea. Mpaka sasa watu watano wamethibitika kupoteza maisha na 40 wameumia.

Mimi kinachonisikitisha ni kwa nini mabomu yalundikwe Dar badala ya kujenga emergence amour maporini?. This time ni lazima Mwinyi awajibe hakuna siasa hapo. Hata kama watawafukuza kazi waliokuwa responsible lakini huu ni uzembe wa system nzima.
 
Back
Top Bottom