Getrude Lwakatare ni Mchungaji, Mwanasiasa

Getrude Lwakatare ni Mchungaji, Mwanasiasa

Kidogo ungepata jibu ila umekosea!! Nipe mji nikupe jibu sahihi!
Swali langu liliuliza je Getrude Rwakatare ni Mchungaji,Mbunge au Muhujumu uchumi?

Swali hili linahitaji jibu moja tu,kwani ukisema ni Mchungaji na Mbunge mbona basi hafanyi kazi za mbunge km ambavyo tunawaona baadhi ya wabunge wakifanya?

Ukisema ni Mchungaji,mbona hatuoni kwa sasa akifanya kazi za kichungaji(yaani kukemea maovu ktk jamii)!? Zaidi sana tunamuona na kumsikia akihusishwa ktk Kashfa mbalimbali, km Kuvamia Ardhi na kutajwa kuwa miongoni mwa Wezi Sugu wa umeme hapa Tanzania? Je hiyo ndio kazi za Mchungaji na Mbunge?

Kama utanipa Mji basi jibu ni kuwa Getrude Rwakatare sio Mbunge wala Mchungaji bali ni MPIGA DILI!! Hizo sifa zingine ulizompa za Uchungaji na Ubunge ni njia tu ya kumrahisiahia yeye kupiga DILI bila kusanukiwa na wajinga!!
Jibu nimeshakupa nipe basi Mji!

wewe una tatizo kidogo sana ukiwahi litakwisha, wewe unataka mbunge afanye nini zaidi ya kuhudhuria vikao vya bunge, kuchangia hoja, kutetea maslahi ya wananchi wake na watanzania kwa ujumla?! Umeona Mh. Lwakatare hafanyi hayo? (weka ushahidi kama hajafanya hayo yote au kaulize Ifakara), Pili: Wewe kwa upeo wako kazi ya Uchungaji ni kukemea maovu? Mchungaji huchunga kanisa kwa kufundisha neno la Mungu kwa usahihi na kumuandaa muumini kwenda mbinguni baada ya kufa kwake hapa duniani. Muumini akishalijua neno la Mungu, ni wajibu wake kuachana sasa na tabia zote mbaya ambayo ni kazi ya shetani. Ndio maana nakwambia unatatizo, lakini dogo sana , unahitaji tiba kiasi kidogo sana.

Mwisho, kama bado unahitaji mji, nenda Kanyigo na nakutakia safari njema. Naomba tafadhali usinisababishie ban siku ingine
 
Kwa Wakristo wote awe mchungaji, nabii, mtume ama mwanasiasa. Tunapaswa kumcha, ambako ni kuchukia uovu na kupenda mema. Kukemea uovu siyo kazi ya viongozi tu, jamii yote inao wajibu wa kukemea. Huwezi kuhalalisha maovu yako kwa kuonesha ya wengine! Tanzania tujenge jamii bora yenye misingi ya kumtii Mungu, alafu jamii hiyo itazaa viongozi bora, kwa sababu viongozi wanatoka kwenye jamii. Tatizo letu wanajamii wa Tanzania siyo waaminifu kwenye imani zetu, tunajua mabaya na mema, lakini pamoja na kuishi tofauti na tunayoiita imani yetu, tunaona makosa hayo kwa wengine tu.
Mimi siujui sana ubaya ama uzuri wa Rwakatare, lakini najua tatizo kubwa la jamii, siyo waaminifu, na hatujioni, jitazame! Siasa ama kuongoza nchi iwe mwito wala siyo jambo ovu la kufanywa na waovu bali watu waadilifu wenye kumcha Mungu na kuuchukia uovu,
 
kama yesu yupo ndani ya moyo wa ko utajua mama getrude ni mchungaji, kama unashetani ndani ya moyo wako ujua mama getrude siyo mchungaji..kazi kwako

Kazi ipi?wewe unayeutetea uovu kwa kivuli cha Yesu ndie shetani mkubwa Kama wewe ni muumini wake nenda kamshauri aludishe viwanja vyote alivyopora na amlipe Mzee Ngonyani pesa zake za kiwanja asiwalipe wapambe wanaomsaidia jinsi ya kulikwepa Deni hapo utaonekana si muumini wa shetani kinyume na hapo lawama Hapa JF hazitamalizika
 
Ushauri wa Bure kwa huyo mchungaji namshauri kwanza awatizame upya washauri wake kwani inaelekea hawamshauri vizuri namna ya kuishi bila sikendo Kama walivyo wachungaji wengine wakubwa au Yawezekana kuna Wapambe wao wananufaika na Udhaifu wake kwani kila ikitokea janga inabidi wapambe wampatie Bajeti ya kupangua Majanga pasipo kujitambua Kuwa anachafuka yeye hutoa pesa kwa wapambe matokeo yake Wapambe wamemfikisha hapa alipo sasa !ebu mchungaji jaribu kuvimaliza Vimeo vyote vya Viwanja kisha uone Kama kuna mtu atakulalamikia !
 
Alafu kwa mambo yote haya machafu kujulikana bado mibaba na misuti na mimama inasema nasali kanisa la mama lwakatare hahaha ukombozi bado sana jamani kwa hii tz bado sana! Ingetakiwa huyu kesha achiwa kanisa lake
biashara ya unga
biashara ya kuuza watoto
wizi wa umeme
bado mijianaume iko pale!

Believe me, moja ya mambo yanayorudisha nyuma maendeleo ya watanzania ni mafundisho ya hizi dini za kigeni. Wanafundisha wananchi/waumini unyenyekevu il-hali rasimali ya taifa lao ikitumika vibaya. Matokeo ya mafundisho haya ni watanzania kutokuwa aggressive kwa mambo yanayowaumiza kama vile rushwa, ufisadi n.k. Hospitali zetu hazina dawa, elimu duni, umasikini uliokithiri lakini wananchi wameendelea kuwa wapole.

Wachungaji na viongozi wa kisiasa wamejiingiza kwenye biashara na kashfa kubwa kubwa lakini waumini bado wanaendelea kuwaamini. Kwa nini viongozi wa dini hawakemei ufisadi na rushwa hadharani? Kwa nini hawatengi viongozi wala rushwa na mafisadi il-hali wengi ni waumini wao? Ukombozi wa fikra must start from church now, waumini wafunguke akili kwanza! Short of that hili taifa litaendelea kupiga marktime.
 
Wiki ijayo bunge linaanza lazima atatoa hoja kuhusu JF ifungwe kwa hoja hz
 
Jamani msitake kulitia gundu ukoo wa kamanda wilfred lwakatare,huyu mama si Lwakatare ila ni Rwakatare.Lwakatare ni ukoo wa wilfred lwakatare ambao hawana undugu wowote ule na fisadi huyu.
 
Wiki ijayo bunge linaanza lazima atatoa hoja kuhusu JF ifungwe kwa hoja hz

Akitaka JF isimkosoe ajitahidi alipe madeni yake ya viwanja na awaepuke wapambe wanaotumia Udhaifu wake kujinufaisha hakika atapotea JF
 
well said mkuu "The intelligence doesnt lie on faith" kwanini ana records ya evils. wewe muumini hujiulizi tu?yule mama ni mchumia tumbo na free manson
 
Huyu mpogoro ni tapeli flani. Amewakamata wajingawajinga wanampa vihela vyao hapo mikocheni b.
 
huyu mazeri ni more than two in one... yani anapiga kata funika za kutakata e.g: huku anaimba ccm no 1 huku kanisani anapiga yu mwemaaaaa..... yu mwemaaaa...maishani mwangu...
 
1.Ni udhaifu na tabia mbaya sana kuamini kuwa jamii ya watanzania itarekebishwa na viongozi.
2.Hadi hapo wananchi waishio Tanzania watakapojitambua kuwa wao ni nani (self awareness) na kukataa katakata kupelekwa wasipopataka wao.
3.Hadi mafisadi watakapojua kuwa "HAWA JAMAA HAWAPENDI" matendo fulani fulani ndipo watakapoacha kufanya matendo hayo.

4. Wananchi ndio wanaopaswa kubadilika na sio Rwakatare au Dewji. Wengi sana wanasema wanachukia ufisadi, Lakini kila mmoja wetu yuko busy kutafuta mwanya wa kuwa Fisadi??????????????????????????????????????????
 
Huyu mpogoro ni
tapeli flani. Amewakamata wajingawajinga wanampa vihela vyao hapo
mikocheni b.

nina rafiki yangu mmoja alinialika kwenye ibada ya jumapili hapo kanisani kwao (MLIMA WA MOTO)!
Hayo mahubiri niliyoyasikia hapo ni viroja..!
 
Aliye mwema nani Silaa au nani? Aliye mwema awe wa kwanza kumrushia jiwe! wengine wana wivu na nyumba yake na mafanikio yake..mama songa mbele maana hata angeshuka paulo leo watu wangemkataa
 
Back
Top Bottom