Getrude Lwakatare ni Mchungaji, Mwanasiasa

Sio nia yangu kumchafua au kumkashifu Mch Kwakatare. Lakini nimekuwa na maswali mengi sana juu ya Ubunge na Uchungaji wake ukizingatia kwamba Kiongozi yeyote ktk jamii awe anatokana na Dini au Siasa kazi yake kubwa ni kukemea Uovu!

Ni takriban miaka 6 kama sio 7 sasa tangia Mama yangu huyu kuingia ktk ulingo wa Siasa. Binafsi ni mfuatiliaji mzuri sana wa Vipindi vya bunge lakini sikumbuki na sijui km kuna siku niliwahi kumuona Mama Lwakatare akipinga Ufisadi Bungeni. Zaidi sana niliwahi kumsikia akimuomba waziri husika kuifungia Jamii Forum.

Kuna usemi umeenea sana Mijini kuwa CCM ni Ukoo wa Panya,kwa kuwa Baba,Mama,Babu,Bibi,Dada,Kaka,Shangazi na Mjomba wote ni Wezi! Siamini hakika km ni kweli kwa 100% lakini yawezekana kwa 99%.

Kuna wengine wameenda mbali zaidi na kusema kuwa CCM ni Janga hata ukamchukuwa MALAIKA ukamuweka humo bado tu atakuwa Fisadi.

Wiki iliyopita Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dk Tereza Huvisa akizungumza na wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira, iliyokwenda kumtembelea Ofisi za Baraza la Mazingira (NEMC) aliwataja Vigogo watatu jijini Dar es salaam kuwa ni "WAVAMIZI" Sugu wa Ardhi.

Huviza alikuwa akiogopa kuwataja kwa majina vigogo hao lakini mwenyekiti wa kamati hiyo James Lembeli alimkasirikia na kumhoji ni nani huyo alieko juu ya sheria kiasi cha kumfanya aogope kumtaja licha ya kuwa kavunja sheria.
Kufuatia shinikizo hilo, Waziri aliwataja wavamizi hao sugu wa Ardhi kuwa ni, Mbunge wa Singida Mjini Mohamed Dewji, Mbunge na Mch Getrude Lwakatare na Patrick Lutabanzibwa.

Getrude Lwakatare Mchungaji na Mbunge wa viti maalum(CCM) alishatajwa pia hapo nyuma ktk Orodha ya wanaodhaniwa kuwa ni "WEZI SUGU" wa umeme,ingawa hadi sasa hatukusikia alichukuliwa hatua gani.

Kama nilivyosema hapo mwanzo kuwa Sio nia yangu kumchafua Mama Lwakatare ila ukweli nimeshindwa kujua kuwa yupo kundi lipi, kwa kuwa Kanisani kwa cheo cha Uchungaji yupo, Bungeni kwa Cheo cha Ubunge akiitwa yupo,na Kwa WAHUJUMU na Wavamizi wa mali za Umma yupo!

Ndio maana nauliza Getrude Lwakatare ni MCHUNGAJI, MBUNGE, au ni MUHUJUMU UCHUMI? Nashindwa kidogo kumfananisha Getrude Lwakatare na Mbunge Peter Msigwa wa Iringa mjini au Mbunge na Mch Israel Natse wa Karatu ambao wamekuwa mstari wa mbele kukemea Maovu ndani na nje ya Bunge.

Samahani kwa yeyote nitakae kuwa nimemkwaza.

Penye red hapo, ni Mchungaji na pia Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
IMG_1153.JPG

Its amazing
 
unasungukasunguka tu, au ulitaka kusema huyu mama alilala mbele pale china na kumuacha mtoto wa mfalme aingie matatani na zile kilo za ngano laini?
 
Kuna mtu mmoja alisema kuwa yeye tangia amjue Reinhad Bonke hakuwahi kusikia akijiongeza majina zaidi ya Mwinjilist!
Ila hapa Tanzania utamsikia mtu mwaka huu akijiita Mtumishi,mwakani Mwinjilist,mwaka unaofuatia Mchungaji,Mwaka mwingine Askofu,Mwaka mwingine Mtume,mwaka mwingine NABII! Ndani ya miaka 7 anakuwa na vyeo vyote hivi. Je hapo kweli kuna Mungu anaetumikiwa au ni shetani tu?
 
Duh! Ninakushauri usiende kwani utarudi na pepo. Mchunguze kwanza mchungaji wako kuhusu wale watoto inaosemekana aliowatafutia wabakaji halafu akataka eti kesi iishe kimya kimya. Kha!
Vipi kuhusu wale wachawi waliosemekana wamenguka hapo kanisani miaka ya nyuma. Huenda nao ulikua usanii.
 
Kuna mtu mmoja alisema kuwa yeye tangia amjue Reinhad Bonke hakuwahi kusikia akijiongeza majina zaidi ya Mwinjilist!
Ila hapa Tanzania utamsikia mtu mwaka huu akijiita Mtumishi,mwakani Mwinjilist,mwaka unaofuatia Mchungaji,Mwaka mwingine Askofu,Mwaka mwingine Mtume,mwaka mwingine NABII! Ndani ya miaka 7 anakuwa na vyeo vyote hivi. Je hapo kweli kuna Mungu anaetumikiwa au ni shetani tu?
Muumini yeyote anapaswa kumwabudu Mungu kwa uangalifu sana ikiwa anasali ktk makanisa ya aina hii uliyoitaja. Zamani iikua unahamasishwa kumtolea Bwana ili kazi yake isonge mbele siku hizi imekua tofauti kabisa kila mtu ana definition yake ya utoaji lol waumini tuwe macho.
 
Inabidi wanaojua skendali za Mama huyu, Mh. Mch. Director Rwakatare (Dr) atuelezee vizuri!
 
Penye red hapo, ni Mchungaji na pia Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kidogo ungepata jibu ila umekosea!! Nipe mji nikupe jibu sahihi!
Swali langu liliuliza je Getrude Rwakatare ni Mchungaji,Mbunge au Muhujumu uchumi?

Swali hili linahitaji jibu moja tu,kwani ukisema ni Mchungaji na Mbunge mbona basi hafanyi kazi za mbunge km ambavyo tunawaona baadhi ya wabunge wakifanya?

Ukisema ni Mchungaji,mbona hatuoni kwa sasa akifanya kazi za kichungaji(yaani kukemea maovu ktk jamii)!? Zaidi sana tunamuona na kumsikia akihusishwa ktk Kashfa mbalimbali, km Kuvamia Ardhi na kutajwa kuwa miongoni mwa Wezi Sugu wa umeme hapa Tanzania? Je hiyo ndio kazi za Mchungaji na Mbunge?

Kama utanipa Mji basi jibu ni kuwa Getrude Rwakatare sio Mbunge wala Mchungaji bali ni MPIGA DILI!! Hizo sifa zingine ulizompa za Uchungaji na Ubunge ni njia tu ya kumrahisiahia yeye kupiga DILI bila kusanukiwa na wajinga!!
Jibu nimeshakupa nipe basi Mji!
 
Vipi kuhusu wale wachawi waliosemekana wamenguka hapo kanisani miaka ya nyuma. Huenda nao ulikua usanii.

Mzee hakuna cha Wachawi wala Wanga kuanguka Kanisani. Yote ni Mazingaumbwe ya kuwanasa Wajinga. Dili linapangwa na watu wanalipwa kujidai wameanguka kanisani kumbe ni uwongo tu!

Kuna mtu mmoja aliwahi kusema kwamba shetani nae anaenda na wakati. Kwa hiyo anajuwa kwamba ili kuwavuta watu ni lazima atumie njia ya Dini au wanaojiita Watumishi.

Maana siku hizi utasikia sijui Gongo la mboto kuna mtu anaombea huyo mara kule Masaki,ili mradi tu watu wapige Dili!

Washindwe ktk Jina la Yesu!!
 
haya makanisa ya majina ya watu auu mtu mmoja mmoja sijui mchungaji nabii mwingira, kabobe,mzee wa upako,nk ni ya kuyaogopa sana maana huwezi kujia anamtumikia mungu gani na dhamira yake ya kweli anayoendeshe utumishi ni ipi.

mimi nitabaki kusali katika makanisa niliyozaliwa na kuyakuta, katoliki angikana, sabatho, luteli nk

Yesu, Paulo, Petro, Yohana etc. hawakuwa Katoliki, lutherani, etc wala hakuna panapotajwa makanisa yao. Cha msingi fuata maagizo ya Biblia ambayo ni Utakatifu (WAEBRANIA 12:14) na siyo maagizo ya dhehebu kwa kuwa hayatakusaidia siku ile.
 
huyu maza anauza watoto mbele, human trafickn, alivyoona wazungu wanaoleta msaada kwnye skul yake kule tabata cjui wamemshtukia akaifunga eti amekosa hela ya kuendeshea, ndo akaanza kuwatumia wachungaji wake kuwabaka na kuwauza watoto kama yule mwenye kesi ya kutorosha watoto wa kichaga toka huko moshy, hotel walizofikishwa hao watoto aliyekuwa analipia vyumba ni huyo bibi, anayejifanya anaweza kutoa elimu ya ndoa ilihali yuko single,
 
Ukiona mchungaji anang'ang'ania siasa na uchungaji, muombe Mungu sana afunguliwe. haswa kwa CCM, hainipi sana akilini. Tena fuatia kwa undani, alipataje ubunge? utajiju.
 
Yesu, Paulo, Petro, Yohana etc. hawakuwa Katoliki, lutherani, etc wala hakuna panapotajwa makanisa yao. Cha msingi fuata maagizo ya Biblia ambayo ni Utakatifu (WAEBRANIA 12:14) na siyo maagizo ya dhehebu kwa kuwa hayatakusaidia siku ile.
Church of Corinthian, Ephesian ect? those were apostles.. ni kweli there was no church of paulo.
 
Methali mshika mawili moja humponyoka nadhani hili la Uchungaji litamponyoka kwani kupora viwanja na kuwazurumu wazee kama akina Ngonyani wa huko kawe ni dalili tosha kuwa ibirisi amemjaa pia anapaswa ajitambue kuwa tiba ya uovu si kumwomba Waziri aifungie JF bali ni kuhakikisha anawalipa wale wote wanaomdai na aache kutumia pesa nyingi kuzui haki za watu kwani kuna Wajanja wamejipenyeza kwake wanajinufaisha na Udhaifu wake Wa kukwepa kumlipa Ngonyani na wanavuta pesa kiulaini kwa ahadi ya kumsaidia kukwepa kumlipa huyo mzee masikini asiye na uwezo wowote
 
Huyu mama ni mmoja kati ya watu ambao wanaogopwa kutajwa kwenye list ya wahujumu uchumi na nguvu kazi Tanzania.

Siasa na uchungaji ni maficho yake tu.
 
Back
Top Bottom