GESTAPO yatunyemelea! Je tumerudi nyuma miaka 80?

GESTAPO yatunyemelea! Je tumerudi nyuma miaka 80?

Lazima wamsifie kwa sababu binadamu tuna tabia ya ku-take things for granted. Au kwa maneno mengine huwa hatujui thamani ya kitu hadi tukikose.
Binadamu ni wanafiki sana,kuna mambo yalitokea Enzi za JK leo tumesahau Magufuli anaitwa dikteta

1.Kifo cha Daudi Mwangosi,Dr. Mvungi
2.Kuteswa kwa Dk Ulimboka,kumwagiwa tindikali kina Kubenea
3.Kufungiwa kwa Mwanahalisi,Kufungwa familia ya Nguza Viking
4.Mabomu ya Arusha,
5.Zitto kufungiwa bungeni (Buzwagi)
6.Kukamatwa kwa Mbowe,kukamatwa kwa Lema,Kukamatwa kwa Mtikila,Kukamatwa kwa Sheikh Ponda

Na Enzi za Ben Mkapa
1.Mauaji ya Mwembechai
2.Mauaji yaliyotokea uchaguzi Zanzibar hadi watu wakakimbilia Mombasa
 
Watakubali tu. Sioni mtu yeyote mwenye ujasiri wa kuchomoa zaidi ya kulia lia humu mitandaoni. Tena hata huku mitandaoni naona watu wamepunguza baada ya kale kasheria ketu kapya kuanza kazi yake.
Ubabe wa kishamba haujawahi kushinda umma .
 
Ubabe wa kishamba haujawahi kushinda umma .
Uko sahihi kabisa ila ni hadi huo uma uamue kufanya kweli. Kulialia mitandaoni hakusaidii kitu. Hata waarabu walikandamizwa miaka kibao hadi walipoamua imetosha.
 
Mi napenda hali inavyoendelea ,nataka ibane zaidi hasa kwa wale waliolala hawajijui (jamii wana lumumba) tuumie sote labda itafika wakati tutafanya maamuzi bora!
 
Tatizo lako claytonx ni ujinga...hujui kilichokuja kuwapata viongozi wa GESTAPO. Waliokuwa na bahati walimeza sumu na kujiua ama walijipiga risasi. Ambao hawakuwa na ujasiri wa kujiua walikuja kuwindwa kama wawindwavyo nguchiro na wengi waliihama nchi wakitafuta pa kujificha. Hata hivyo pamoja na kukimbia, wao na vizazi vyao wameendelea kuwindwa hadi leo huku dunia ikizidi kuwa ndogo kwao. Miaka 80 baadaye wanaendelea kukamatwa hata kama wamezeeka kiasi gani na hata kama alikuwa ni mtumishi tu wa nyumbani anayo kesi ya kujibu kwa ukatili walioufanya dhidi ya binadamu wenzao.

Hapa sisi tunatoa onyo tu kwamba ingawa kwa sasa viongozi wetu hawagusiki kwa sababu GESTAPO ya kwetu inastawi kwa damu za raia wa nchi hii, iko siku mambo yatawageuka. Bahati mbaya kwao ni kwamba katika dunia ya leo, hata sehemu za kujificha zinazidi kuwa finyu...dunia imekuwa tambarare. Iko siku wao na vizazi wao watakumbuka haya tunayoyaandika ingawa itakuwa too late kwao. Adolf Hitler, Fuhrer wa Ujerumani na mkewe, Eva Braun, kwa kujua yatakayowapata walijifungia na kujiua. Baada ya miaka 71 GESTAPO imepiga hodi Tanzania, na mlango tuliuacha wazi.
bahaty mbaya sana sisi sio wajerumani na hatuwez kua wajerumani
 
    • Kwa mara ya kwanza tunashuhudia Bunge likianza kuhoji hukumu zinazotolewa na mahakama.
    • Kwa mara ya kwanza mbunge wa kuteuliwa na Rais ndiye analiongoza Bunge.
    • Kwa mara ya kwanza tunashuhudia polisi wakianza kutoa hukumu.
    • Kwa mara ya kwanza Kanali wa Jeshi anamtishia maisha mtuhumiwa hadharani.
    • Kwa mara ya kwanza kumkosoa Rais ni sawa na kuvunja sheria.
    • Kwa mara ya kwanza matokeo ya uchaguzi mkuu yafutwa bila kuwepo walalamikaji.
    • Pamoja na kuwa na mfumo wa vyama vingi Bunge lageuka kikao cha chama tawala
    • Pamoja na kuwa na mfumo wa vyama vingi, siasa yapigwa marufuku.
    • Kwa mara ya kwanza Katiba ni kama kipande tu cha karatasi.
    • .......
Je GESTAPO yapiga hodi Tanzania?

Gestapo kilikuwa ni kikosi rasmi cha polisi katika serikali ya NAZI Ujerumani kilichoanzishwa baada ya kuunganishwa kwa mihimili miwili ya dola na kuwa kitu kimoja. Mihimili hiyo ilikuwa ni utendaji (executive branch) na mahakama (judicial branch). Baada ya kuunganishwa kwa hii mihimili miwili ya dola, hakukuwepo tena na haja ya kuwa na mhimili wa tatu wa kutunga sheria (Legislative branch) au kwa jina lililozooleka Bunge (Parliament)

Kazi maalum ya GESTAPO ilikuwa ni kuhakikisha upinzani wowote dhidi ya chama tawala, NAZI Party, haupewi nafasi na kumkosoa Hitler kulitafsiriwa kama uhaini. Njia iliyotumika kuzima upinzani ilijulikana kama schutzhaft ambapo mtuhumiwa alilazimishwa kusaini hati kwamba ni yeye ndio kaomba kuwekwa kizuizini kwa usalama wake. Hata uhuru wa kuabudu uliminywa na viongozi wa dini wasioafiki walikamatwa na kufungwa kama wahaini wa taifa.
rubbish
 
Maendeleo yanaletwa na 1.watu 2.siasa safi 3.uongozi bora,mnaweza kuongezea hapo lakini kati ya hivyo vitatu nilivyovitaja kuna moja au viwili utawala huu unavitumia vibaya.
 
Unaandika vizuri sana. Hongera

Turudi kwenye Mada: Hoja ya Msingi ya Nkamia ni kwa nini mtuhumiwa aliruhusiwa kwenda nje kutafuta fedha ya kulipa...hiyo ndiyo hoja yake kubwa. na kwa kuwa huyo mtuhumiwa aliruhusiwa na mahakama, ni sahihi kusema bunge linahoji maamuzi ya mahakama.

Kama hoja hiyo si nzito, na tukikubaliana kwamba ni halali akatafute fedha, basi sioni tatizo lolote kama atazipata kwa harambee, kuuza nguo zake au mali zake zingine mradi tu apate hizo pesa. Cha msingi ni kwamba pesa zipatikane kwa njia halali. najua kilichomkera Nkamia na wewe ni kwa sababu kuna "watoto wa baba mdogo" walionekana wakichanga pesa...
Mwambie,hata kesi ya Kajala pesa ya faini walienda kuitafuta kwa donations
 
You are just proving my point shylock...you are after a pint of my blood and why not, you are blood thirsty!
Not necessarily your blood but a pint of post in some district, that is what the so called avid critics hope in attaining by always pretending to be on the side of the so called 'the good side'.
 
GESTAPO syndrome...! You qualify for a medal dlamini, here's one for you.

coin3a.jpg
 
Kama utekelezaji wa majukumu unaofanyika sasa na kusimamia misingi ya kiutendaji ndio kuja kwa Gestapo, nadhani ije tu maana tulichoka sana blahblah na usanii.
 
Huu ni unafiki of highest order, binafsi nawaheshimu sana wazee wa CDM ila mmezidi kuwa wanafiki na gia zenu said angani, mnajidai mnajua demokrasia kwa kuropoka ila mnashindwa kuitumia hata wenyewe kwenye chama chenu tu.
1) Spika wa bunge kutokuwa mbunge wa kuchaguliwa, kisheria na kisiasi hili si tatizo, mtu yoyote ana haki ya kuwa mbunge as long as ametimiza matakwa ya katiba, na hiyo ndiyo demokrasia. Inashangaza Mag3 unalalamikia kuwa na Naibu Spika asiye mbunge wa kuteuliwa ila unasahau Uspika 2010 CDM walimsimamisha Marando na 2015 CDM walimsamisha Ole Madeye.

Marando na Ole Medeye walikuwa si tu hawakuwa hata na huo ubunge wa kuteuliwa ila hawakuwa wabunge kabisa. Unafiki huu nyie wazee mnajifunzia wapi siku hizi, au gia za angani zinawapotezea kumbukumbu haraka hivi.
 
Inakuwaje unajidai kushangaa bunge kuhoji hukumu za mahakama ila haushangai vyama vya siasa vinavyowatishia wanachama wake kwenda mahakamani. CDM ukienda mahakamani na kushindwa kesi umefukuzwa uanachama automatically. Hivi ndivyo ndugu Zitto alivyotendwa na wapenda demokrasia wa CDM, kwako wewe hii ni sahihi ? Hii ndio demokrasia ya CDM ya kuigwa, na huu ndio uhuru wa wanachama wa chama demokrasia mbele ya mahakama?
Kwa nini tusianze kutoa boriti kwenye macho yako kabla ya kuhangaika na boriti za Magu. Nyie CDM hamna demokrasia ndani ya chama ila unaona ni sahihi, ila kwa unafiki wa wanasiasa mnafungia macho uozo wenu mnakimbilia ya CCM. Tafuta demokrasia ndani ya CDM kwanza kabla ya kuanza kuitafuta nje ya CDM.
 
Bunge limegeuka kuwa kijiwe cha CCM kwa sababu ya ujinga wa Mbowe. Wabunge wa UKAWA watarudi bungeni siku atayoamua Mbowe kwa sababu yeye ndiyo amewaamuru wasusie Bunge. Wanaoathirika na mgomo huu wa kijinga ni wapiga kura wa majimbo ya UKAWA. Wananchi wataamua 2020 kama waliwatuma wawakilisha kwenda kufanya migomo ya kuonyeshana ubabe bungeni, muda waenda kasi, jibu murua utalipata 2020 kama UKAWA wakiendelea na utoto wao.

Dk Tulia hana jimbo na wala hana pressure yoyote kisiasi, inashangaza UKAWA wanahangaika na Tulia, huyu kisiasi hadhuriki. Mbowe na uzoefu wake wote hajui tofauti ya "strike" na "protest" ?
 
Mwisho, mzee wangu Mag3, mbona hauulizii term limits kwa uenyekiti CDM au CUF, au hiyo sio sehemu ya demokrasia? Mbowe alikinyofua kipengele cha term limits 2006 kwenye katiba ya CDM, je hii ndio demokrasia tunayolilia au ni unafiki tu na gia za angani?

Inakuwaje haupigi kelele kuwa na demokrasia bora ndani ya CDM ila unalalamikia demokrasia nje ya CDM. Kama CDM ni wapenda demokrasia kwa nini wasianze kurekebisha mambo yaliyo ndani ya uwezo wao. CDM ukitangaza kuusaka uenyekiti upo hatihati ya kuitwa msaliti.
ACHA KUPIGA MAYOWE, KATAA KUWA NYUM..
 
Bunge limegeuka kuwa kijiwe cha CCM kwa sababu ya ujinga wa Mbowe. Wabunge wa UKAWA watarudi bungeni siku atayoamua Mbowe kwa sababu yeye ndiyo amewaamuru wasusie Bunge. Wanaoathirika na mgomo huu wa kijinga ni wapiga kura wa majimbo ya UKAWA. Wananchi wataamua 2020 kama waliwatuma wawakilisha kwenda kufanya migomo ya kuonyeshana ubabe bungeni, muda waenda kasi, jibu murua utalipata 2020 kama UKAWA wakiendelea na utoto wao.

Dk Tulia hana jimbo na wala hana pressure yoyote kisiasi, inashangaza UKAWA wanahangaika na Tulia, huyu kisiasi hadhuriki. Mbowe na uzoefu wake wote hajui tofauti ya "strike" na "protest" ?
Nyiye maccm tatizo hampendagi kusikia ukweli, as far as ukweli huo utakuwa wa kuwakosoa nyiye.

Huyo mdada analiendesha Bunge kwa kuibeba serikali waziwazi.

Wabunge wa upinzani wakiomba miongozo katika masuala ya msingi kabisa, huyo NS huwa anawapuuzia.

Hebu nitoe mifano michache namna gani huyo mdada anavyoliendesha Bunge kama kikao cha NEC ya chama chake.

Wakati wa suala la sakata la serikali kuwafukuza wanachuo wa Udom ndani ya masaa 24 wawe wameondoka Chuoni, huyo mdada aliombwa mwongozo wa jambo hilo na wabunge wakataka jambo hilo lijadiliwe kama jambo la dharula, huyo mdada alipuuzia. .

Wakati Mbunge wa CCM wa jimbo la Ulanga alipotoa madai ya uwongo na ya udharirishaji wa kusema wabunge wote wa Chadema wa viti maalum ni 'mabebi' kwa maana nafasi hizo wamezipata baada ya kufanya ngono na mabosi wao na huyo mdada kuombwa mwongozo, badala ya kuwa fair kwa kumtaka Mbunge huyo aljyetoa madai huyo athibitishe madai yake kama kanuni za Bunge zinavyotaka, yeye alipuuzia.

Ndiyo maana waTz wengi wanaamini kuwa huyo mdada amewekwa na Mkulu kwenye kiti hicho cha NS kwa 'special mission' ya kuibeba serikali, ambapo ni kinyume cha wajibu mkuu wa Bunge ambao ni kuisimamia serikali.....
 
Nyiye maccm tatizo hampendagi kusikia ukweli, as far ukweli huo utakuwa wa kuwakosoa nyiye.

Huyo mdada analiendesha Bunge kwa kuibeba serikali waziwazi.

Wabunge wa upinzani wakiomba miongozo katika masuala ya msingi kabisa, huyo NS huwa anawapuuzia.

Hebu nitoe mifano michache namna gani huyo mdada anavyisndesha Bunge kama NEC yao.

Wakati wa suala la sakata la serikali kuwafukuza wanachuo wa Udom nano ya masaa 24 wawe wameondoka Chuoni, huyo mdada alipuuzia.

Wakati Mbunge wa CCM wa jimbo la Ulanga alipotoa madai ya uwongo na ya udharirishaji wa kusema wabunge wote wa Chadema wa viti maalum ni 'mabebi' kwa maana nafasi hizo wamezipata baada ya kufanya ngono na mabosi wao na huyo mdada kuombwa mwongozo, badala ya kuwa fair kwa kumtaka Mbunge huyo aljyetoa madai huyo athibitishe madai yake kama kanuni za Bunge zinavyotaka, yeye alipuuzia.

Ndiyo maana waTz wengi wanaamini kuwa huyo mdada amewekwa na Mkulu kwenye kiti hicho cha NS kwa 'special mission' ya kuibeba serikali, ambapo ni kinyume cha wajibu mkuu wa Bunge ambao ni kuisimamia serikali.....
Ni lini kiti cha Spika kiliwahi kutokuwa na upendeleo? Je solution ni kugomea Bunge, Dk Tulia anaathirika nini kwa mgomo na kususa susa kwa CDM?

Kwa ufupi, Mbowe ametoa uamuzi wa ovyo kwa kuamua kuwa na mgomo usio na kikomo akitegemea CCM wataenda kuomba usuluhisho. CCM haiwaathiri sana kwa CDM au UKAWA kugoma na hawatarajii kuomba usuluhishi wowote, ni suala la muda na gia tu Mbowe atayotumia kula matapishi yake wakati anawarudisha "Nyumb.... " wake Bungeni.
 
Huu ni unafiki of highest order, binafsi nawaheshimu sana wazee wa CDM ila mmezidi kuwa wanafiki na gia zenu said angani, mnajidai mnajua demokrasia kwa kuropoka ila mnashindwa kuitumia hata wenyewe kwenye chama chenu tu.
1) Spika wa bunge kutokuwa mbunge wa kuchaguliwa, kisheria na kisiasi hili si tatizo, mtu yoyote ana haki ya kuwa mbunge as long as ametimiza matakwa ya katiba, na hiyo ndiyo demokrasia. Inashangaza Mag3 unalalamikia kuwa na Naibu Spika asiye mbunge wa kuteuliwa ila unasahau Uspika 2010 CDM walimsimamisha Marando na 2015 CDM walimsamisha Ole Madeye.

Marando na Ole Medeye walikuwa si tu hawakuwa hata na huo ubunge wa kuteuliwa ila hawakuwa wabunge kabisa. Unafiki huu nyie wazee mnajifunzia wapi siku hizi, au gia za angani zinawapotezea kumbukumbu haraka hivi.
mtanzania1989, Je unaijua Katiba ya Tanzania? Je unazijua sifa za mgombea Uspika? Je unajua tofauti iliyopo katika sifa Kati ya mgombea Uspika na Unaibu Spika?

Naomba nikueleweshe kama ifuatavyo. Katika kugombea Uspika hakuna sharti la kuwa mbunge ama wa kuchaguliwa au wa kuteuliwa lakini katika kugombea Unaibu Spika sharti uwe mbunge.

Marando na Ole Mideye waliruhusiwa kugombea Uspika lakini hawangeruhusiwa kugombea Unaibu Spika. Usiniulize kwa nini, soma Katiba.

Utawala ulijua Ndugai anaumwa lakini bado akateuliwa kugombea Uspika. Inawezekana walijua toka awali kuwa hataweza kuliongoza Bunge.

Katika hali hiyo haishangazi kuteuliwa kwa Dr. Tulia kuwa mbunge na baadaye kupendekezwa kugombea Unaibu Spika.

Kwa jinsi anavyoendesha Bunge sitashangaa...uteuzi wake kuwa Mbunge unazua maswali mengi Tu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nyiye maccm tatizo hampendagi kusikia ukweli, as far ukweli huo utakuwa wa kuwakosoa nyiye.

Huyo mdada analiendesha Bunge kwa kuibeba serikali waziwazi.

Wabunge wa upinzani wakiomba miongozo katika masuala ya msingi kabisa, huyo NS huwa anawapuuzia.

Hebu nitoe mifano michache namna gani huyo mdada anavyoliendesha Bunge kama kikao cha NEC ya chama chake.

Wakati wa suala la sakata la serikali kuwafukuza wanachuo wa Udom ndani ya masaa 24 wawe wameondoka Chuoni, huyo mdada aliombwa mwongozo wa jambo hilo na wabunge wakataka jambo hilo lijadiliwe kama jambo la dharula, huyo mdada alipuuzia. .

Wakati Mbunge wa CCM wa jimbo la Ulanga alipotoa madai ya uwongo na ya udharirishaji wa kusema wabunge wote wa Chadema wa viti maalum ni 'mabebi' kwa maana nafasi hizo wamezipata baada ya kufanya ngono na mabosi wao na huyo mdada kuombwa mwongozo, badala ya kuwa fair kwa kumtaka Mbunge huyo aljyetoa madai huyo athibitishe madai yake kama kanuni za Bunge zinavyotaka, yeye alipuuzia.

Ndiyo maana waTz wengi wanaamini kuwa huyo mdada amewekwa na Mkulu kwenye kiti hicho cha NS kwa 'special mission' ya kuibeba serikali, ambapo ni kinyume cha wajibu mkuu wa Bunge ambao ni kuisimamia serikali.....
Unataka kuujua ukweli?
Kazi ya Bunge ni kuisimamia na kuishauri serikali na si kupinga pinga tu na kukwamisha serikali. CDM ya sasa wamejaa matusi, kejeli, mipasho na dharau, wanabadilika rangi zaidi ya kinyonga, hawana jema wao. Kwa sifa hizi usitegemea utachukuliwa kwa umakini sawa na CDM ya bunge lililopita.
 
Back
Top Bottom