GESTAPO yatunyemelea! Je tumerudi nyuma miaka 80?

GESTAPO yatunyemelea! Je tumerudi nyuma miaka 80?

Unaandika vizuri sana. Hongera

Turudi kwenye Mada: Hoja ya Msingi ya Nkamia ni kwa nini mtuhumiwa aliruhusiwa kwenda nje kutafuta fedha ya kulipa...hiyo ndiyo hoja yake kubwa. na kwa kuwa huyo mtuhumiwa aliruhusiwa na mahakama, ni sahihi kusema bunge linahoji maamuzi ya mahakama.

Kama hoja hiyo si nzito, na tukikubaliana kwamba ni halali akatafute fedha, basi sioni tatizo lolote kama atazipata kwa harambee, kuuza nguo zake au mali zake zingine mradi tu apate hizo pesa. Cha msingi ni kwamba pesa zipatikane kwa njia halali. najua kilichomkera Nkamia na wewe ni kwa sababu kuna "watoto wa baba mdogo" walionekana wakichanga pesa...

Wakuu hivi hii hoja ya Mh. Nkamia hatima yake ilifika vipi hapo bungeni?
 
Kama hiyo GESTAPO itatufikisha kwenye uchumi wa viwanda acha ije tu maana porojo zilikuwa nyingi awamu ya nne na hazijatufikisha popote.

Kama GESTAPO ndiyo ilijenga misingi ya Ujerumani ya leo then ni nzuri sana hii.
 
KISUTU MATERIAL,get ready for the court hearings, dont say i didnt tell u



unafikiri kuwa ili linaepukika?kwa utawala kama huu,husipo muabudu mkuu,kisutu na segerea ni mahali pako pa kujidah/kusitareheka
kama unaitaka kweli na kupitia iyo kweli utakuwa huru,KISUTU ione kawaidi tu
ktk historia ya dunia hakuna pahala ambapo wapigania uhuru hawakufungwa,kuuwawa,kunyanyaswa na wengine kupotea kabisa bila kufahamika kama walikufa au la.
ivyo wote wanao fungwa au kukamatwa ktk utawala huu hawana tofauti na waliokamatwa UGANDA,ZAIRE,GERMANY,na mataifa mengine yaliyo pitia utawala wa aina hii
 
*Kwa mara ya kwanza tunaona serikali imesimamia ipasavyo zoezi la watumishi hewa na kuokoa zaidi ya bil 25 tulizokuwa tunapoteza kila mwezi
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia wanafuzi wanasoma bure kutoka chekechea hadi form four.
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia serikali inafunga mkanda na kukata matumizi ya kipuuzi kama vile safari za nje ya nchi zisizo na tija, sherehe zisizo na tija
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia serikali inapambana ma mafisadi na rushwa (kwa vitendo)
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia serikali inapambana na kuhakikisha wagonjwa hawalali chini wala wanafunzi kukaa chini
* Kwa mara ya kwanza nchini tunashuhudia serikali haiendeshwi "kishwaiba" na rais anatumbua hata rafikizake wa karibu wanapokosea
* Kwa mara ya kwanza tunashuudia bajeti inayoangalia kusaidia masikini- ambayo zaidi ya 45% ni miradi ya maendeleo
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia wapinzani wanaishiwa na hoja na kubakia na viroja
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia dunia nzima inaiangukia tanzania na kuomba walau watuazime rais walau kwa miezi mitatu ili akasaidie kunyoosha mamboyao

Nadhani naipenda hiyo "GESTAPO" ya Magufuli...bring it on
Serikali kutimiza wajibu wake ni jambo la msingi lakini hakuipi mamlaka ya kuvunja sheria ya demokrasia na kutoheshimu katiba. Hayo yote uliyosema Kule Libya yalifanyika lakini kutoheshimu demokrasia kumeipeleka nchi hapo ilipo. Jee ungependa nasi tuishie kuwa kama Libya?
 
Nimekupa heshima kubwa sana mtanzania1989, si kawaida yangu kujibizana na watoto aina yako ambao uelewa wao ni mdogo kiasi hicho. Pamoja na kwamba inawezekana umesoma nilichoandika umetoka kapa, hukuelewa chochote. Nimepitia majibu yako yote yaliyofuatia na sasa nimejua jinsi uwezo wako wa kuelewa ulivyo finyu. Nakushauri ukae utulie, urudie tena kusoma niliyoyaandika bila papara wala kukurupuka na labda utaweza kubahatika ukaelewa nazungumzia nini.
Mag3,
Si lazima unijibu ila hatuwezi acha upotoshaji wa wazi na unafiki wa namna hii, unajiona una uwezo wa ajabu, sishangai, hiyo ni sifa ya CDM wote siku hizi, mmelewa na kupofushiwa na sifa za 2015, hamuoni janga lililo mbele yenu.

Angalia, unajiona umeongea cha ajabu, wakati ni wewe ndio unashindwa kuelewa ni nini nilichoandika, ila kwa kuwa nia yangu nikuondoa upotoshaji wa wazee kama wewe, nitarudia tena.

Umeleta hoja ya si " demokrasia " kwako wewe kuwa na Naibu Spika ambaye ni Mbunge wa kuteuliwa, unasema ni demokrasia kuwa na Naibu Spika ambaye ni Mbunge wa kuchaguliwa tu, kwako unaamini hii ndio "demokrasia", ingawaje huyu Naibu Spika kikatiba amefikisha vigezo vyote pamoja na kuwa Mbunge ila unaamini hii si "demokrasia" yako.

Nimekuuliza, Spika kikatiba, si lazima kuwa Mbunge ila kwa kutumia vigezo hivyo hivyo vya demokrasia yako kwa nini haulalamiki Spika awe Mbunge wa kuchaguliwa , hii double standards yako imetokea wapi hadi kwa Spika unajificha kwa kutumia katiba ila kwa Naibu Spika unaona katiba si sawa? Na hii ni Rocket science mzee?
 
Nimekupa heshima kubwa sana mtanzania1989, si kawaida yangu kujibizana na watoto aina yako ambao uelewa wao ni mdogo kiasi hicho. Pamoja na kwamba inawezekana umesoma nilichoandika umetoka kapa, hukuelewa chochote. Nimepitia majibu yako yote yaliyofuatia na sasa nimejua jinsi uwezo wako wa kuelewa ulivyo finyu. Nakushauri ukae utulie, urudie tena kusoma niliyoyaandika bila papara wala kukurupuka na labda utaweza kubahatika ukaelewa nazungumzia nini.
Mag3,
Uhuru wa Mahakama,
Si sahihi kwa yoyote kuingilia mhimili wa mahakama iwe Bungeni au katika vyama vya siasa, unalalamika Tz hakuna demokrasia kwa kuwa tu kuna Mbunge bungeni ameongelea mambo ya mahakama. Mbona haulalamiki CDM hakuna hii demokrasia kwa kuwa na katiba kandamizi juu ya wanachama wa CDM kwenda mahakamani kwa miongo sasa.

CDM ukienda mahakamani na ukishindwa kesi, umejifukuzisha uanachama, hii kwako ni demokrasia ila Mbunge mmoja akiropoka bungeni huko inakuwa Tz hakuna uhuru wa Mahakama. Mzee ni bora unyamaze tu utunze heshima yako...
 
Mteule wa rais anakuwa Spika...watanzania maneno mengi lakini weupe sana,linchi hata haijulikani linaenda wapi,watu wamebaki kukenua menu tu kinafiki

Wabunge wa ccm wanatia aibu mnooo!!!
Hili jambo wao hata hawakuliona kweli?? Ndio tatizo la hawa watu, wanafanya maamuzi kwa ushabiki...sasa nao wanisoma namba yao wao wenyewe.
 
Kilichokudanganya mpaka ukamuamini ni hilo neno Imam? Hata kipindi hicho kinakibwetere kama Mbowe walikuwapo kuwataka wenzao kufa wenyewe wakikimbia na kuweka nguvu ya kupambana baadaye. Alphonso Drakama huko Msumbiji alishawishi wengi wenye akili kama zako kufa yeye kaweka nguvu ya baadaye kwa kukimbia na sasa anaendesha maisha yake na familia yake.
A coward fear death.
 
Nilianzisha hii thread mwezi Juni mwaka jana, hata hivyo je, kwa ambao awali hawakukubaliana nami, mnaweza sasa kukiri kwamba tunakoelekea hatuna tofauti na Ujerumani miaka ya 1940s? Sina hakika wengi wa Watanzania wanasemaje lakini nina hakika namba ya wanaokubaliana nami kwa sasa inazidi kuongezeka siku hadi siku.

Nawakaribisha tena ambao walinipinga wakati huo nijue wanasemaje leo...Mbunge Lema yuko ndani, Mbunge JuaKali anatumikia kifungo, Wabunge wengi wa Upinzani wanakabiliwa na kesi, vyombo vya habari vinatishiwa kufungiwa, wakuu wa wilaya na mikoa wamepewa amri ya kukamata wakosoaji wa serikali na kuwaweka ndani...

Naomba maoni yenu...
 
Nilianzisha hii thread mwezi Juni mwaka jana, hata hivyo je, kwa ambao awali hawakukubaliana nami, mnaweza sasa kukiri kwamba tunakoelekea hatuna tofauti na Ujerumani miaka ya 1940s? Sina hakika wengi wa Watanzania wanasemaje lakini nina hakika namba ya wanaokubaliana nami kwa sasa inazidi kuongezeka siku hadi siku.

Nawakaribisha tena ambao walinipinga wakati huo nijue wanasemaje leo...Mbunge Lema yuko ndani, Mbunge JuaKali anatumikia kifungo, Wabunge wengi wa Upinzani wanakabiliwa na kesi, vyombo vya habari vinatishiwa kufungiwa, wakuu wa wilaya na mikoa wamepewa amri ya kukamata wakosoaji wa serikali na kuwaweka ndani...

Naomba maoni yenu...
Upendo peneza naye kakamatwa kwa kusema kuna njaa nchini......

Uzuri waliomchagua ndiyo wanateswa sana na guilty....
 
Ile ya Hitler itakuwa GESTAPO phase 1 na hii ya sasa ni GESTAPO phase II
 
Mtanzania 1989,

..ukisema naibu spika ni mbunge wa kuteuliwa unakuwa uko sahihi kwa asilimia 50.

..ulipaswa kusema ni mbunge wa kuteuliwa na raisi dr.john pombe magufuli.

..ikiliangalia suala hili kwa undani, in "3D", basi utaelewa kwa Raisi ameteua Naibu Spika.

..hilo limetokea baada ya jitihada za kumteua kuwa Spika kushindikana.

..sasa baada ya hapo uchanganye na yale majibu/mtizamo kuwa kuna mihimili yenye mizizi mirefu kuliko mihimili mingine.

..katika mazingira kama hayo unadhani bunge litakuwa huru kweli?

..haya mambo usiyashangilie kwasababu yanawatokea cdm. Akimalizana nao atahamia hata kwenu wana ccm.

Cc Mag3
 
JokaKuu said:
..haya mambo usiyashangilie kwasababu yanawatokea cdm. Akimalizana nao atahamia hata kwenu wana ccm.
Mkuu dikteta yeyote hawezi kufanikiwa mpaka wawepo watu kama mtanzania1989, na kwa bahati mbaya, ingawa idadi yao inapungua lakini uelewa wao finyu bado uko pale pale. Kila dikteta anavyozidi kushangiliwa ndivyo anavyozidi kukomaa kwa kauli chafu akiamini yuko sahihi kwa matendo na kauli.

Juzi nilikuwa nikitazama video ya Hitler na ushawishi aliokuwa nao kwa baadhi ya Wajerumani wa wakati huo ulitisha. Wako ambao hawakutaka kabisa kukiri kwamba alikuwa anawapeleka kusiko na neno lake hata pale lilipoonekana dhahiri kukiuka misingi ya haki, lilishangiliwa kwa vifijo na nderemo.

Lakini taratibu baadhi ya washangiliaji walipoanza kuonja ladha ya machungu yaliyowakuta wenzao ndipo walianza kujiuliza kuwa huenda wanakoelekea si salama. Wengine wao pamoja na kukiri hali hiyo, woga ambao walikuwa wameshiriki kuulea ulitawala mioyo yao wasiweze hata kupaza sauti zao.

Wakosoaji waliitwa wasaliti na wito wa kutaka hatua kali zichukuliwe dhidi yao zilisikika huku baadhi ya ndugu zao wakiitaka serikali kuwashughulikia bila huruma. Ukisoma hii thread toka mwanzo, wapo wengi tu wameniita majina mengi tu wakitaka nisakwe na kukamatwe kwa wanachoita uchochezi.

Lakini iko siku itafika kama ilivyomfikia Hitler na historia itatoa hukumu.
 
Back
Top Bottom