GESTAPO yatunyemelea! Je tumerudi nyuma miaka 80?

Ukiongozwa na mtu ambaye hajui kuoongoza hayo ndio madhara...anasema anataka kuipeleka nchi mbele lakini hata yeye hajui hapo mbele ni wapi...
Kuwatisha watu na kunyamazisha demokrasia sio suluhisho la kuharakisha maendeleo..siasa na maendeleo havigawanyiki...

Atafika mahali atakwama maana hata yeye ndani ya chama chake anahitaji siasa...

Mambo mazito kama katiba kwake sio hoja ya msingi...

sasa mwenzako anaamini kwamba anajua kuongoza na antumia mbinu za wacommunist ambazo zinahakikisha hamna upinzani. CCM iliundwa na mcommunist na wote wanaoiunga iwe wanajua au hawajui watalazimika kubadilisha fikra zao ziwe kicommunist au watafukuzwa. Ndiyo maana Tanzania na china wana uhusiano mzuri kwasababu wachina ndiyo waliomfundisha nyerere ucommunist.
 
Wakomunisti watu wabaya sana,sasa nawaelewa wamarekani kwa nini walikuwa wanaupinga,ukomunisti
 
Kumbuka hii;

In Germany they came first for the Communists, and I didn't speak up because I wasn't a Communist.
Then they came for the Jews, and I didn't speak up because I wasn't a Jew.
Then they came for the trade unionists, and I didn't speak up because I wasn't a trade unionist.
Then they came for the Catholics, and I didn't speak up because I was a Protestant.
Then they came for me, and by that time no one was left to speak up!

-- Martin Niemöller, 1945​
Umeongea hoja ya msingi sana, kila mwenye masikio atakuwa amesikia.

Kila mtu akidhani hili jambo halimuhusu, lakini at the end of the day, hakuna mtu atakayesalimika na maamuzi haya...........
 
Unaandika vizuri sana. Hongera

Turudi kwenye Mada: Hoja ya Msingi ya Nkamia ni kwa nini mtuhumiwa aliruhusiwa kwenda nje kutafuta fedha ya kulipa...hiyo ndiyo hoja yake kubwa. na kwa kuwa huyo mtuhumiwa aliruhusiwa na mahakama, ni sahihi kusema bunge linahoji maamuzi ya mahakama.

Kama hoja hiyo si nzito, na tukikubaliana kwamba ni halali akatafute fedha, basi sioni tatizo lolote kama atazipata kwa harambee, kuuza nguo zake au mali zake zingine mradi tu apate hizo pesa. Cha msingi ni kwamba pesa zipatikane kwa njia halali. najua kilichomkera Nkamia na wewe ni kwa sababu kuna "watoto wa baba mdogo" walionekana wakichanga pesa...
Masuala mengi yamezuiliwa kujadiliwa bungeni kwasababu yapo katika mahakama

Hapa mhimili wa bunge 'unaheshimu'mhimili wa sheria. Mifano ipo mingi sana kuhusu hili

Bunge lilipitisha maazimio kama mhimili wa kuitaka serikali ichukue hatua dhidi ya watu waliohusika na kashfa mbali mbali. Bunge lilikuwa mhimili unaojitegemea

Serikali haikuchukua hatua na baadhi ya watuhumiwa waliachwa kustaafu.
Sababu kubwa ilikuwa kutoingilia mhimili wa 'utawala' na bunge lilishafanya kazi yake

Suala la kijana lilikuwa katika mkondo wa sheria .

Sheria hizo zilitungwa na mhimili wa bunge na kusainiwa na mhimili wa 'serikali' kuwa sheria zinazotumiwa na mhimili wa mahakama.

Hakimu alitoa hukumu na masharti kwa kuzingatia kanuni, na sheria husika.
Utaratibu wa mahakama ni kuwa kama mtuhumiwa au malalamikaji hakuridhika na maamuzi, kuna nafasi ya kukata rufaa.

Serikali ndiyo ilimshtaki mtuhimiwa, na ndiyo yenye haki ya kukata rufaa.
Si kazi ya bunge kujadili mwenendo wa kesi mahakamani.

Kulijadili suala hilo bungeni ni kuingilia mhimili wa mahakama.

Endapo ipo haja, wabunge wangeomba mhimili wa serikali ulete mswada wa kuangalia marekebisho ya sheria inayotumika mahakamani. Si kujadili kesi ya mtu mmoja
 
Safi sana Kuna siku bunge litaanza kusikiliza kesi kama mahakama,.
 
Tumefika pabaya. Lakini wanachoogopa ni nini wakati wanasema wanatumikia wananchi? Au wanaogopa wananchi watajua kitu?
Hii hofu ya watawala kupita kiasi hadi kupiga marufuku shughuli zote za vyama vya upinzani hadi 2020 ndiyo inaanza kuzua maswali mengi yanayokosa majibu......

Ingawa nimekuwa sizipi uzito mkubwa kauli za EL anazodai kuwa yeye ndiye aliyeibuka mshindi kwenye uchaguzi mkuu October mwaka jana.

Lakini kwa hofu hii kubwa ya kupita kiasi ya watawala naanza kushawishika kuwa kile kituo cha Mlimani City cha kufanya tallying, ndiyo pengine kilichozalisha haya yote..........
 
Kiwewe cha Uchaguzi wa mwaka 2015, Kiufupi kwenye ule uchaguzi walikuwa wanang'oka mazima Mkuu. Haya wanayoyafanya ni option B ya kujilinda wao otherwise the Worst Case Scenario ni kufanya kama ya Zanzibar katika chaguzi zijazo.
 
*Kwa mara ya kwanza tunaona serikali imesimamia ipasavyo zoezi la watumishi hewa na kuokoa zaidi ya bil 25 tulizokuwa tunapoteza kila mwezi
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia wanafuzi wanasoma bure kutoka chekechea hadi form four.
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia serikali inafunga mkanda na kukata matumizi ya kipuuzi kama vile safari za nje ya nchi zisizo na tija, sherehe zisizo na tija
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia serikali inapambana ma mafisadi na rushwa (kwa vitendo)
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia serikali inapambana na kuhakikisha wagonjwa hawalali chini wala wanafunzi kukaa chini
* Kwa mara ya kwanza nchini tunashuhudia serikali haiendeshwi "kishwaiba" na rais anatumbua hata rafikizake wa karibu wanapokosea
* Kwa mara ya kwanza tunashuudia bajeti inayoangalia kusaidia masikini- ambayo zaidi ya 45% ni miradi ya maendeleo
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia wapinzani wanaishiwa na hoja na kubakia na viroja
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia dunia nzima inaiangukia tanzania na kuomba walau watuazime rais walau kwa miezi mitatu ili akasaidie kunyoosha mamboyao

Nadhani naipenda hiyo "GESTAPO" ya Magufuli...bring it on
*Hv unayemsifu anafanya vtu vzur kwa mara ya kwanza ni wa chama gani vile?
*Hv chama kinachotuongoza kimebadilika au ni kilekile?
*Huyo unayesema kavurunda ni wa chama gani vile?
Ngoja ni subscribe ili utakapoanza kumsema mh Rais atakapomaliza muda wake nikukumbushe jinsi ulivyo
 
*Kwa mara ya kwanza tunaona serikali imesimamia ipasavyo zoezi la watumishi hewa na kuokoa zaidi ya bil 25 tulizokuwa tunapoteza kila mwezi
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia wanafuzi wanasoma bure kutoka chekechea hadi form four.
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia serikali inafunga mkanda na kukata matumizi ya kipuuzi kama vile safari za nje ya nchi zisizo na tija, sherehe zisizo na tija
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia serikali inapambana ma mafisadi na rushwa (kwa vitendo)
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia serikali inapambana na kuhakikisha wagonjwa hawalali chini wala wanafunzi kukaa chini
* Kwa mara ya kwanza nchini tunashuhudia serikali haiendeshwi "kishwaiba" na rais anatumbua hata rafikizake wa karibu wanapokosea
* Kwa mara ya kwanza tunashuudia bajeti inayoangalia kusaidia masikini- ambayo zaidi ya 45% ni miradi ya maendeleo
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia wapinzani wanaishiwa na hoja na kubakia na viroja
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia dunia nzima inaiangukia tanzania na kuomba walau watuazime rais walau kwa miezi mitatu ili akasaidie kunyoosha mamboyao

Nadhani naipenda hiyo "GESTAPO" ya Magufuli...bring it on
umenena vyema mkuu kwa kujibu hoja kwa hoja, ila haya mazuri ya utendaji wa serikali yanafanyika on the expense of democracy.. sina shaka nia ya serikali inaweza kuwa njema ila the means zinazotumika zinatia shaka kwa ustawi wa demokrasia na maendeleo tuliyoyafikia ya uhuru wa mawazo
 
    • Kwa mara ya kwanza tunashuhudia Bunge likianza kuhoji hukumu zinazotolewa na mahakama.
    • Kwa mara ya kwanza mbunge wa kuteuliwa na Rais ndiye analiongoza Bunge.
    • Kwa mara ya kwanza tunashuhudia polisi wakianza kutoa hukumu.
    • Kwa mara ya kwanza Kanali wa Jeshi anamtishia maisha mtuhumiwa hadharani.
    • Kwa mara ya kwanza kumkosoa Rais ni sawa na kuvunja sheria.
    • Kwa mara ya kwanza matokeo ya uchaguzi mkuu yafutwa bila kuwepo walalamikaji.
    • Pamoja na kuwa na mfumo wa vyama vingi Bunge lageuka kikao cha chama tawala
    • Pamoja na kuwa na mfumo wa vyama vingi, siasa yapigwa marufuku.
    • Kwa mara ya kwanza Katiba ni kama kipande tu cha karatasi.
    • .......
Je GESTAPO yapiga hodi Tanzania?

Gestapo kilikuwa ni kikosi rasmi cha polisi katika serikali ya NAZI Ujerumani kilichoanzishwa baada ya kuunganishwa kwa mihimili miwili ya dola na kuwa kitu kimoja. Mihimili hiyo ilikuwa ni utendaji (executive branch) na mahakama (judicial branch). Baada ya kuunganishwa kwa hii mihimili miwili ya dola, hakukuwepo tena na haja ya kuwa na mhimili wa tatu wa kutunga sheria (Legislative branch) au kwa jina lililozooleka Bunge (Parliament)

Kazi maalum ya GESTAPO ilikuwa ni kuhakikisha upinzani wowote dhidi ya chama tawala, NAZI Party, haupewi nafasi na kumkosoa Hitler kulitafsiriwa kama uhaini. Njia iliyotumika kuzima upinzani ilijulikana kama schutzhaft ambapo mtuhumiwa alilazimishwa kusaini hati kwamba ni yeye ndio kaomba kuwekwa kizuizini kwa usalama wake. Hata uhuru wa kuabudu uliminywa na viongozi wa dini wasioafiki walikamatwa na kufungwa kama wahaini wa taifa.

Unaongelea ukweli unaouma ,lakini chunga kucha na meno yako
 
Maneno ya Sumaye yanatimia haraka kuliko hata ilivyotarajiwa.... Naogopa huenda yakaenda mbali zaidi na zaidi na kisha... Mungu atuhurumie!!!

Tuliambiwa amechaguliwa na Mungu ahhhhhhh Samahani ni MTEULE wa MUNGU,akamalizia anataka kuwa RAIS WA MALAIKA,inshort anataka kuwa MUNGU mtu.Hapo ndipo nilianza kuona rangi zake kamili
 
    • Kwa mara ya kwanza tunashuhudia Bunge likianza kuhoji hukumu zinazotolewa na mahakama.
    • Kwa mara ya kwanza mbunge wa kuteuliwa na Rais ndiye analiongoza Bunge.
    • Kwa mara ya kwanza tunashuhudia polisi wakianza kutoa hukumu.
    • Kwa mara ya kwanza Kanali wa Jeshi anamtishia maisha mtuhumiwa hadharani.
    • Kwa mara ya kwanza kumkosoa Rais ni sawa na kuvunja sheria.
    • Kwa mara ya kwanza matokeo ya uchaguzi mkuu yafutwa bila kuwepo walalamikaji.
    • Pamoja na kuwa na mfumo wa vyama vingi Bunge lageuka kikao cha chama tawala
    • Pamoja na kuwa na mfumo wa vyama vingi, siasa yapigwa marufuku.
    • Kwa mara ya kwanza Katiba ni kama kipande tu cha karatasi.
    • .......
Je GESTAPO yapiga hodi Tanzania?

Gestapo kilikuwa ni kikosi rasmi cha polisi katika serikali ya NAZI Ujerumani kilichoanzishwa baada ya kuunganishwa kwa mihimili miwili ya dola na kuwa kitu kimoja. Mihimili hiyo ilikuwa ni utendaji (executive branch) na mahakama (judicial branch). Baada ya kuunganishwa kwa hii mihimili miwili ya dola, hakukuwepo tena na haja ya kuwa na mhimili wa tatu wa kutunga sheria (Legislative branch) au kwa jina lililozooleka Bunge (Parliament)

Kazi maalum ya GESTAPO ilikuwa ni kuhakikisha upinzani wowote dhidi ya chama tawala, NAZI Party, haupewi nafasi na kumkosoa Hitler kulitafsiriwa kama uhaini. Njia iliyotumika kuzima upinzani ilijulikana kama schutzhaft ambapo mtuhumiwa alilazimishwa kusaini hati kwamba ni yeye ndio kaomba kuwekwa kizuizini kwa usalama wake. Hata uhuru wa kuabudu uliminywa na viongozi wa dini wasioafiki walikamatwa na kufungwa kama wahaini wa taifa.

Mzee kwa mabandiko yako ya siku za nyumaw na siku hizi kuna mabadiliko makubwa sana kwenye msimamo wako juu ya vita dhidi ya ufisadi.
 
*"Nitawafanya wanaoishi kama malaika waishi kama mashetani"*, hii ni kauli ya kuogopwa kuliko kawaida, maana hakuna aasiyejua kuwa Shetani kazi yake ni fujo na ukatili na mambo yote mabaya.
 
Back
Top Bottom