GESTAPO yatunyemelea! Je tumerudi nyuma miaka 80?

GESTAPO yatunyemelea! Je tumerudi nyuma miaka 80?

    • Kwa mara ya kwanza tunashuhudia Bunge likianza kuhoji hukumu zinazotolewa na mahakama.
    • Kwa mara ya kwanza mbunge wa kuteuliwa na Rais ndiye analiongoza Bunge.
    • Kwa mara ya kwanza tunashuhudia polisi wakianza kutoa hukumu.
    • Kwa mara ya kwanza Kanali wa Jeshi anamtishia maisha mtuhumiwa hadharani.
    • Kwa mara ya kwanza kumkosoa Rais ni sawa na kuvunja sheria.
    • Kwa mara ya kwanza matokeo ya uchaguzi mkuu yafutwa bila kuwepo walalamikaji.
    • Pamoja na kuwa na mfumo wa vyama vingi Bunge lageuka kikao cha chama tawala
    • Pamoja na kuwa na mfumo wa vyama vingi, siasa yapigwa marufuku.
    • Kwa mara ya kwanza Katiba ni kama kipande tu cha karatasi.
    • .......
Je GESTAPO yapiga hodi Tanzania?

Gestapo kilikuwa ni kikosi rasmi cha polisi katika serikali ya NAZI Ujerumani kilichoanzishwa baada ya kuunganishwa kwa mihimili miwili ya dola na kuwa kitu kimoja. Mihimili hiyo ilikuwa ni utendaji (executive branch) na mahakama (judicial branch). Baada ya kuunganishwa kwa hii mihimili miwili ya dola, hakukuwepo tena na haja ya kuwa na mhimili wa tatu wa kutunga sheria (Legislative branch) au kwa jina lililozooleka Bunge (Parliament)

Kazi maalum ya GESTAPO ilikuwa ni kuhakikisha upinzani wowote dhidi ya chama tawala, NAZI Party, haupewi nafasi na kumkosoa Hitler kulitafsiriwa kama uhaini. Njia iliyotumika kuzima upinzani ilijulikana kama schutzhaft ambapo mtuhumiwa alilazimishwa kusaini hati kwamba ni yeye ndio kaomba kuwekwa kizuizini kwa usalama wake. Hata uhuru wa kuabudu uliminywa na viongozi wa dini wasioafiki walikamatwa na kufungwa kama wahaini wa taifa.
Ni kweli haya tumeyaona , lakini je watu wa leo watakubaliana na upuuzi huu wa haki zao kusiginwa kama wale watu wa enzi zile ?
 
Tatizo lako claytonx ni ujinga...hujui kilichokuja kuwapata viongozi wa GESTAPO. Waliokuwa na bahati walimeza sumu na kujiua ama walijipiga risasi. Ambao hawakuwa na ujasiri wa kujiua walikuja kuwindwa kama wawindwavyo nguchiro na wengi waliihama nchi wakitafuta pa kujificha. Hata hivyo pamoja na kukimbia, wao na vizazi vyao wameendelea kuwindwa hadi leo huku dunia ikizidi kuwa ndogo kwao. Miaka 80 baadaye wanaendelea kukamatwa hata kama wamezeeka kiasi gani na hata kama alikuwa ni mtumishi tu wa nyumbani anayo kesi ya kujibu kwa ukatili walioufanya dhidi ya binadamu wenzao.

Hapa sisi tunatoa onyo tu kwamba ingawa kwa sasa viongozi wetu hawagusiki kwa sababu GESTAPO ya kwetu inastawi kwa damu za raia wa nchi hii, iko siku mambo yatawageuka. Bahati mbaya kwao ni kwamba katika dunia ya leo, hata sehemu za kujificha zinazidi kuwa finyu...dunia imekuwa tambarare. Iko siku wao na vizazi wao watakumbuka haya tunayoyaandika ingawa itakuwa too late kwao. Adolf Hitler, Fuhrer wa Ujerumani na mkewe, Eva Braun, kwa kujua yatakayowapata walijifungia na kujiua. Baada ya miaka 71 GESTAPO imepiga hodi Tanzania, na mlango tuliuacha wazi.
Mungu akulinde sana .
 
Kwanini uuwawe na polisi na si mwingine?
Je wakati wa Adolf Hitler Wajerumani waliuawa wote?
Je wakati wa Idi Amin Waganda wote waliuawa?
Je wakati wa Kim il Sung, Wakorea wote waliuawa?
Je wakati wa madiktetea, wananchi wote huuawa?

Jibu ni kwamba hapana , hawauawi wote...watu kama Msororo69 watabaki. Wanafiki wana namna ya kuwepa mauti ingawa ni kwa muda tu. Wauaji wa sasa zamu yao nayo itafika.
 
    • Kwa mara ya kwanza tunashuhudia Bunge likianza kuhoji hukumu zinazotolewa na mahakama.
    • Kwa mara ya kwanza mbunge wa kuteuliwa na Rais ndiye analiongoza Bunge.
    • Kwa mara ya kwanza tunashuhudia polisi wakianza kutoa hukumu.
    • Kwa mara ya kwanza Kanali wa Jeshi anamtishia maisha mtuhumiwa hadharani.
    • Kwa mara ya kwanza kumkosoa Rais ni sawa na kuvunja sheria.
    • Kwa mara ya kwanza matokeo ya uchaguzi mkuu yafutwa bila kuwepo walalamikaji.
    • Pamoja na kuwa na mfumo wa vyama vingi Bunge lageuka kikao cha chama tawala
    • Pamoja na kuwa na mfumo wa vyama vingi, siasa yapigwa marufuku.
    • Kwa mara ya kwanza Katiba ni kama kipande tu cha karatasi.
    • .......
Je GESTAPO yapiga hodi Tanzania?

Gestapo kilikuwa ni kikosi rasmi cha polisi katika serikali ya NAZI Ujerumani kilichoanzishwa baada ya kuunganishwa kwa mihimili miwili ya dola na kuwa kitu kimoja. Mihimili hiyo ilikuwa ni utendaji (executive branch) na mahakama (judicial branch). Baada ya kuunganishwa kwa hii mihimili miwili ya dola, hakukuwepo tena na haja ya kuwa na mhimili wa tatu wa kutunga sheria (Legislative branch) au kwa jina lililozooleka Bunge (Parliament)

Kazi maalum ya GESTAPO ilikuwa ni kuhakikisha upinzani wowote dhidi ya chama tawala, NAZI Party, haupewi nafasi na kumkosoa Hitler kulitafsiriwa kama uhaini. Njia iliyotumika kuzima upinzani ilijulikana kama schutzhaft ambapo mtuhumiwa alilazimishwa kusaini hati kwamba ni yeye ndio kaomba kuwekwa kizuizini kwa usalama wake. Hata uhuru wa kuabudu uliminywa na viongozi wa dini wasioafiki walikamatwa na kufungwa kama wahaini wa taifa.

Kusema uongo, kuzusha na kutia chumvi matukio ili upate cha kusema katu hakuwezi kujenga nchi. Angalau dhamira yako ikusute, japo sijui umri wako lakini naamini u mtu mzima. Kuna watu kwa vile hawakufanikiwa kushinda uchaguzi basi mioyo inawauma kwelikweli na wangependa kuona nchi hii inaharibikiwa kama vile wao hawaishi humu. Eti wana hamu hawajawahi kuona machafuko. Umesikia nchi gani inafanya kampeni kwa miaka mitano mfulululizo, taja nchi moja tu. Siasa za kampeni zina muda wake, siasa za kujijenga pia zina namna yake ya kufanyika. Tusikubali wazandiki na wanafiki wenye kuchezea maneno watuletee dhiki. Wamezoea uongo na usaliti kwa familia zao sasa wanataka kuona kama uwezo wao huo unaweza kukubalika katika ngazi ya kitaifa.
 
Kuchangiwa na watoto wa baba mdogo ni kielelezo fulani lakini kizuri.
Sheria ya makosa ya mtandao imelalamikiwa na watu wengi ndani na nje.
Kwa hiyo muathirika wa sharia hiyo angeweza kuchangiwa na hela nyingi sana kama angepata mtu wa kupeleka appeal yake nje ya mipaka. Ikiwa appeals za mashoga zinashika kasi mpaka mataifa na wafalme wanatikiswa, itakuwa hii ya kuzuia uhuru wa watu kujieleza.

Mungu saidia tunaishi katika nchi yenye watu wastaarabu sana. Ila kwa hili, chama tawala kinakosea kwa sababu kinapeleka ujumbe huu bila kujua:
-Kwamba, kinaunga mkono uvunjaji wa katiba na haki za msingi wa watu
-kwamba, chama cha jirani ndicho chama kinachotetea haki za watu.

Hii ni kona mbaya wanajiweka kama walivyojiweka bungeni, ambapo:
-Wamewatangazia watanzania kuwa watetezi wa haki za watu ni wale waliondoka
-Waliobaki ni wakandamizaji kwa sababu wamepandisha kozi za kikatili mpaka za vocha ya
500

Kumbe unataka kujieleza mpaka zile hisia zako za ushoga zilizokataliwa juzi? Mi nilishangaa mbona povu jingi namna hii? Anyway shoga, utapata nafuu tu ukiweza kuvuka mipaka katika nchi ambazo ushoga umeruhusiwa, tena huko utapata mwenzi unless kama mwenzi wako nae ni mtanzania kidogo ndipo utapata tabu.
 
Umesikia nchi gani inafanya kampeni kwa miaka mitano mfulululizo, taja nchi moja tu. Siasa za kampeni zina muda wake, siasa za kujijenga pia zina namna yake ya kufanyika.
Unaishi dunia ya peke yako, siyo hii tunayoishi.
 
Unaishi dunia ya peke yako, siyo hii tunayoishi.

Ofcourse, unaishi dunia ya kutunga uongo na kusambaza uongo na wenzako, kukuza na kutia chumvi mambo mkiwa na ajenda mbaya ambazo hazina manufaa kwa nchi.
 
*Kwa mara ya kwanza tunaona serikali imesimamia ipasavyo zoezi la watumishi hewa na kuokoa zaidi ya bil 25 tulizokuwa tunapoteza kila mwezi
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia wanafuzi wanasoma bure kutoka chekechea hadi form four.
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia serikali inafunga mkanda na kukata matumizi ya kipuuzi kama vile safari za nje ya nchi zisizo na tija, sherehe zisizo na tija
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia serikali inapambana ma mafisadi na rushwa (kwa vitendo)
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia serikali inapambana na kuhakikisha wagonjwa hawalali chini wala wanafunzi kukaa chini
* Kwa mara ya kwanza nchini tunashuhudia serikali haiendeshwi "kishwaiba" na rais anatumbua hata rafikizake wa karibu wanapokosea
* Kwa mara ya kwanza tunashuudia bajeti inayoangalia kusaidia masikini- ambayo zaidi ya 45% ni miradi ya maendeleo
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia wapinzani wanaishiwa na hoja na kubakia na viroja
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia dunia nzima inaiangukia tanzania na kuomba walau watuazime rais walau kwa miezi mitatu ili akasaidie kunyoosha mamboyao

Nadhani naipenda hiyo "GESTAPO" ya Magufuli...bring it on
eti kwa Mara ya kwanza we una umri gani?? umejitoa ufahamu almradi utetee ujinga, hayo yote yalikuwrpo yaliondolewa na chama fisadi kinachotawala, ni ujinga kusifia walioharibu makusudi alafu baadaye wanarekebisha kwa gharama kubwa
 
Muda si mrefu hata Jf itafungiwa...Maana dalili zote zipo na zinajionyesha na kama akina Invisible hawajaanza kutiwa kashikashi basi wajiandae maana muda si mrefu kashikashi zitaanza.Dalili ya mvua ni mawingu na mwenzio akinyolewe wewe tia maji au kaa mkao wa kunyolewa..
 
Je wakati wa Adolf Hitler Wajerumani waliuawa wote?
Je wakati wa Idi Amin Waganda wote waliuawa?
Je wakati wa Kim il Sung, Wakorea wote waliuawa?
Je wakati wa madiktetea, wananchi wote huuawa?

Jibu ni kwamba hapana , hawauawi wote...watu kama Msororo69 watabaki. Wanafiki wana namna ya kuwepa mauti ingawa ni kwa muda tu. Wauaji wa sasa zamu yao nayo itafika.
Majibu mazuri sana. Kumbe huo utawala uliweka masharti ya namna ya kuendana nao na waliopinga utawala huo waliathirika kwa namna mbalimbali na kuuwawa. Hivyo makosa ni ya marehemu.
Nikupe ushauri kuwa mara nyingi kwa shujaa huenda kilio. Bob Marley katika wimbo wake uitwao Heathen anatushauri kuwa Shujaa ni yule anayepigana na kukimbia kwasababu anaweka nguvu na uhai ili aje kupambana baadaye. Vilevile mazingira kama hayo yakitokea iga busara ya mmea uitwao mwanzi wenyewe ikitokea hali ya hewa ni ya upepo mkali huinama kuupisha upepo na huinuka pale upepo umeisha. Usifuate busara za mwembe wenyewe hushindana na upepo na matokeo yake huangushwa na kuwa kuni.
 
Kwa mara ya kwanza tunashuhudia wanafuzi wanasoma bure kutoka chekechea hadi form four.
Sio kweli! Wakati wa Mwalimu watu walisoma bure na vifaa na nauli juu na wengine walilipwa posho hapakuwa na shida ya madawati!
But Icould put it to be "The Silent Revolution"
Na zaidi wakati wa mwalimu ilikuwa kutoka chekechea hadi chuo kikuu, nini kidato cha nne!
 
Ni kweli haya tumeyaona , lakini je watu wa leo watakubaliana na upuuzi huu wa haki zao kusiginwa kama wale watu wa enzi zile ?
Watakubali tu. Sioni mtu yeyote mwenye ujasiri wa kuchomoa zaidi ya kulia lia humu mitandaoni. Tena hata huku mitandaoni naona watu wamepunguza baada ya kale kasheria ketu kapya kuanza kazi yake.
 
Kusema uongo, kuzusha na kutia chumvi matukio ili upate cha kusema katu hakuwezi kujenga nchi. Angalau dhamira yako ikusute, japo sijui umri wako lakini naamini u mtu mzima. Kuna watu kwa vile hawakufanikiwa kushinda uchaguzi basi mioyo inawauma kwelikweli na wangependa kuona nchi hii inaharibikiwa kama vile wao hawaishi humu. Eti wana hamu hawajawahi kuona machafuko. Umesikia nchi gani inafanya kampeni kwa miaka mitano mfulululizo, taja nchi moja tu. Siasa za kampeni zina muda wake, siasa za kujijenga pia zina namna yake ya kufanyika. Tusikubali wazandiki na wanafiki wenye kuchezea maneno watuletee dhiki. Wamezoea uongo na usaliti kwa familia zao sasa wanataka kuona kama uwezo wao huo unaweza kukubalika katika ngazi ya kitaifa.
Sikujua mikutano hata mahafali ni kampeni, kwa hiyo ccm bungeni pia wanafanya kampeni kwa kusema wanatekeleza ahadi zao
 
Muda si mrefu hata Jf itafungiwa...Maana dalili zote zipo na zinajionyesha na kama akina Invisible hawajaanza kutiwa kashikashi basi wajiandae maana muda si mrefu kashikashi zitaanza.Dalili ya mvua ni mawingu na mwenzio akinyolewe wewe tia maji au kaa mkao wa kunyolewa..
JF ilishawahi kufungiwa na waanzilishi wake walikamatwa na polisi tena Enzi za Kikwete ambaye leo watu wameguka wanamsifia alikuwa raisi bora anayeheshimu uhuru wa vyombo vya habari na utawala bora
 
JF ilishawahi kufungiwa na waanzilishi wake walikamatwa na polisi tena Enzi za Kikwete ambaye leo watu wameguka wanamsifia alikuwa raisi bora anayeheshimu uhuru wa vyombo vya habari na utawala bora
Lazima wamsifie kwa sababu binadamu tuna tabia ya ku-take things for granted. Au kwa maneno mengine huwa hatujui thamani ya kitu hadi tukikose.
 
Back
Top Bottom