- Kwa mara ya kwanza tunashuhudia Bunge likianza kuhoji hukumu zinazotolewa na mahakama.
- Kwa mara ya kwanza mbunge wa kuteuliwa na Rais ndiye analiongoza Bunge.
- Kwa mara ya kwanza tunashuhudia polisi wakianza kutoa hukumu.
- Kwa mara ya kwanza Kanali wa Jeshi anamtishia maisha mtuhumiwa hadharani.
- Kwa mara ya kwanza kumkosoa Rais ni sawa na kuvunja sheria.
- Kwa mara ya kwanza matokeo ya uchaguzi mkuu yafutwa bila kuwepo walalamikaji.
- Pamoja na kuwa na mfumo wa vyama vingi Bunge lageuka kikao cha chama tawala
- Pamoja na kuwa na mfumo wa vyama vingi, siasa yapigwa marufuku.
- Kwa mara ya kwanza Katiba ni kama kipande tu cha karatasi.
- .......
Gestapo kilikuwa ni kikosi rasmi cha polisi katika serikali ya NAZI Ujerumani kilichoanzishwa baada ya kuunganishwa kwa mihimili miwili ya dola na kuwa kitu kimoja. Mihimili hiyo ilikuwa ni utendaji (executive branch) na mahakama (judicial branch). Baada ya kuunganishwa kwa hii mihimili miwili ya dola, hakukuwepo tena na haja ya kuwa na mhimili wa tatu wa kutunga sheria (Legislative branch) au kwa jina lililozooleka Bunge (Parliament)
Kazi maalum ya GESTAPO ilikuwa ni kuhakikisha upinzani wowote dhidi ya chama tawala, NAZI Party, haupewi nafasi na kumkosoa Hitler kulitafsiriwa kama uhaini. Njia iliyotumika kuzima upinzani ilijulikana kama schutzhaft ambapo mtuhumiwa alilazimishwa kusaini hati kwamba ni yeye ndio kaomba kuwekwa kizuizini kwa usalama wake. Hata uhuru wa kuabudu uliminywa na viongozi wa dini wasioafiki walikamatwa na kufungwa kama wahaini wa taifa.