GESTAPO yatunyemelea! Je tumerudi nyuma miaka 80?

GESTAPO yatunyemelea! Je tumerudi nyuma miaka 80?

Kama wengine tulivyowahi kuonya huko awali kuwa GESTAPO ilikuwa inatunyemelea, hatimaye imetua na kupiga kambi Tanzania na tunakoelekea si salama tena! Je bado yuko anayebisha?
 
Tumefika pabaya. Lakini wanachoogopa ni nini wakati wanasema wanatumikia wananchi? Au wanaogopa wananchi watajua kitu?
Wanatumikia wananchi au wanajilinda dhidi ya wananchi?
 
Kama wengine tulivyowahi kuonya huko awali kuwa GESTAPO ilikuwa inatunyemelea, hatimaye imetua na kupiga kambi Tanzania na tunakoelekea si salama tena! Je bado yuko anayebisha?
You are a great thinker
 
*Kwa mara ya kwanza tunaona serikali imesimamia ipasavyo zoezi la watumishi hewa na kuokoa zaidi ya bil 25 tulizokuwa tunapoteza kila mwezi
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia wanafuzi wanasoma bure kutoka chekechea hadi form four.
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia serikali inafunga mkanda na kukata matumizi ya kipuuzi kama vile safari za nje ya nchi zisizo na tija, sherehe zisizo na tija
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia serikali inapambana ma mafisadi na rushwa (kwa vitendo)
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia serikali inapambana na kuhakikisha wagonjwa hawalali chini wala wanafunzi kukaa chini
* Kwa mara ya kwanza nchini tunashuhudia serikali haiendeshwi "kishwaiba" na rais anatumbua hata rafikizake wa karibu wanapokosea
* Kwa mara ya kwanza tunashuudia bajeti inayoangalia kusaidia masikini- ambayo zaidi ya 45% ni miradi ya maendeleo
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia wapinzani wanaishiwa na hoja na kubakia na viroja
* Kwa mara ya kwanza tunashuhudia dunia nzima inaiangukia tanzania na kuomba walau watuazime rais walau kwa miezi mitatu ili akasaidie kunyoosha mamboyao

Nadhani naipenda hiyo "GESTAPO" ya Magufuli...bring it on
bado msimamo wako ni huuhuu?
 
Kama wengine tulivyowahi kuonya, miezi sita tu baada ya awamu hii ya tano kuingia madarakani, kuwa GESTAPO ilikuwa inatunyemelea, hatimaye imetua na kupiga kambi Tanzania na tunakoelekea si salama tena! Je bado yuko anayebisha?
 
Kwa ukumbusho niliwahi kusema hivi...

Hitler hata angetembea uchi, hakuna mwana NAZI angethubutu kumwambia achutame. Aliyediriki alilazimika kusain hati ya kuomba hifadhi gerezani na mara nyingi huo ndio ulikuwa mwisho wake wa kuonekana tena. Kuwa chini ya ulinzi wa GESTAPO kwa sheria iliyojulikana kama sheria ya usiku na ukungu, wengi sana walipotea na hadi leo hawajulikani walipotelea wapi.

Kwa GESTAPO mwongozo walioufuata ni "as long as the police carries out the will of the leadership, it is acting legally". Hapa kwetu tunaelekea huko kwamba kama polisi wanatekeleza maagizo ya viongozi (wa CCM), basi wanachokitenda ni halali kisheria na hali hii imesababisha polisi wetu kuwaonea raia hadi kufikia hata kuua na wasifanywe chochote.
 
Back
Top Bottom