Gerson Msigwa azomewe siku ya Mwananchi

Gerson Msigwa azomewe siku ya Mwananchi

Kwa mashabiki wote wa Yanga mtakaojitokeza kwenye tamasha lenu la siku ya Mwananchi tarehe 12/09/2025 hakikisheni huyo mtu niliyemtaja hapo juu akivamia shughuli ya utambulisho wa wachezaji, viongozi, wadhamini, nk. kwenye siku ya Mwananchi, na kuanza kuleta siasa zake za kujipendekeza na kuwasikilizisha sauti za Bosi wake kwenye kipindi hiki cha kampeni zilizojaa hila, uonevu, ukandamizaji, mauaji, utekaji, unyanyasaji, rushwa, ubabaishaji, na kila aina ya ujinga! AZOMEWE yeye na huyo Bosi wake.

Kwanza huyu jamaa siyo rafiki wa wapenda maendeleo na mabadiliko ya kweli ndani ya hii nchi. Na ikumbukwe ni mwanachama wa jamii forums! Lakini ndiyo mtu huyu huyu aliyetoa hadharani kauli ya dharau kwa Mkurugenzi wa jamii forums Comrade Maxence Melo, pale tu alipotoa taarifa ya kuvamiwa kwa ofisi za jamii forums wiki chache zilizopita. Na bila shaka pia amehusika kwa namna moja au nyingine kufungiwa kwa huu mtandao muhimu kwa jamii, kwa sababu tu ya ubinafsi wao.

Ndugu zangu wapenda michezo, kamwe msikubali wanasiasa kuja kutuharibia furaha yetu. Hawa watu wanatusababishia sana msongo wa mawazo. Na michezo ndiyo inayo tusaidia kupunguza. Sasa wakija kutuvamia na huko, maana yake tutakosa kwa kukimbilia. Na ikitokea na Injinia Hersi naye akaamua kubeba hilo jukumu kwa sababu ya kujipendekeza kwake; na yeye AZOMEWE vizuri kabisa.

MODS msifute huu uzi. Kwanza jamii forums imefungiwa. Kwa hiyo tulieni, kunyweni chai. Kama hamna vitafuno, semeni niwaletee. Bure kabisa.
Huwa tunatofautiana maeneo mengi hasa ya kishabiki, ila katika hili nakuunga mkono.

Watanzania sasa hivi tupo katika kamstari fulani kembamba tukiweza kukavuka hako basi Tanzania itaanza kuongozwa katika misingi sahihi.
 
Kabisa mkuu, hiko ndo watakachoandaa, kuweka watu wao na cameraman kumulika walipo.

Hovyo kabisa.
ccm sasa muda wote wanafanya maigizo, yaani muda wote ni kama wapo location wanafanya cinema,hakuna uhalisia, kila eneo wanaficha ukweli na kutumia mabavu ionekane wanakubalika, kila sehemu ni setup...

uwanjani kwenye kampeni watabeba watu na malori..

mitandaoni wanaajiri vijana kushinda kutwa kufungua posts kuonyesha wanakubalika...

kwenye michezo wanaweka chawa wenye mabango ya Samia huku cameraman akipewa order kuwamulika walipo...
 
Wanayanga wenzangu mtakao hudhuria tamasha la Siku ya Mwananchi hii leo, chonde chonde! Msikubali kutumiwa kama misukule na hawa wanasiasa wabinafsi na mafisadi!

Wakileta porojo zao, wazomeeni ili wajifunze! Na pia watambue kama siasa yenye harufu ya ubaguzi, haina nafasi kwenye michezo. Daima Yanga itabakia kuwa timu ya Wananchi wote! Haijawahi kuwa mali ya ccm au mtu binafsi! Na kamwe tusikubali wahuni waitumie kwa manufaa yao!

Hata kama ni Injinia Hersi, mzomeeni tu. No way out. Kama anaona ccm ni bora zaidi kuliko Yanga, awaachie timu watu wengine na yeye akagombee vyeo ndani ya hicho chama chake.
 
Tatizo lenu mnapenda vya bure.
Msipokee fedha au ndege au ardhi kama ya Jangwani toka serikali au kwa mwanasiasa.
Hakuna cha bure wala nini! Hizo pesa bado zimetokana na kodi/ raslimali zetu. Ardhi ni mali ya wananchi! Na siyo mtu mmoja. Kwa hiyo hakuna kutishana hapa. Yanga ilikuwepo kabla ya GSM na Injinia Hersi. Na itaendelea kuwepo daima.
 
Huyu mama sioni akimaliza miaka mitano ijayo, hichi kitu hakijawah tokea Tanzania
Shida yake kubwa ni kulazimisha gari liende tu hata kama limeharibika/ limekwama kwenye matope.
 
Huyu mama sioni akimaliza miaka mitano ijayo, hichi kitu hakijawah tokea Tanzania
Kapuuzwa na anazidi kupuuzwa na wananchi, huku chini mtaani hata wale wasio na upeo mpana juu ya mambo ya kisiasa au elimu ndogo hawamtaki kabisa, sasa daraja hilo limemkataa je daraja la kati lenye wasomi wengi wasio na ajira??? Hilo la juu tunajua ni wanufaika wa utawala huu nao ni wachache

Maza hapendwi na kila siku anaongeza asilimia ya kutopendwa
 
Nimeshangaa kijijini kwangu ambako ambako miaka nenda ccm ilikuwa haina mpinzani! Leo hii wananchi wanasema huyu mama hawamtaki kwa sababu amesababishia maisha yao kuwa magumu, ameuza bandari kwa Waarabu, nk.

Hakika nilishangaa sana! Sijui ni nani amewaambukiza hii sumu.
 
Na watu wa vijijini wakiweka msimamo mpaka uwahamishe sio kazi rahisi hivyo

Ila kuna wana ccm wanapita kuomba namna za kadi ya mpiga kura kwa ahadi ya kupewa pesa elf 20, CCM ni mafisi aisee
 
Kapuuzwa na anazidi kupuuzwa na wananchi, huku chini mtaani hata wale wasio na upeo mpana juu ya mambo ya kisiasa au elimu ndogo hawamtaki kabisa, sasa daraja hilo limemkataa je daraja la kati lenye wasomi wengi wasio na ajira??? Hilo la juu tunajua ni wanufaika wa utawala huu nao ni wachache

Maza hapendwi na kila siku anaongeza asilimia ya kutopendwa
Ndugu ni lazima achukiwe sbabu hajawai kuchaguliwa na watu kila mahali anajipitisha kwa force huyu mtu sijui anachotutakia Watanzania ni kipi hasa!
 
Ndugu ni lazima achukiwe sbabu hajawai kuchaguliwa na watu kila mahali anajipitisha kwa force huyu mtu sijui anachotutakia Watanzania ni kipi hasa!
Nadhani anachukiwa hasa kwasababu ya hiyo dpworld, ufisadi, rushwa ukititimba yale yote enzi za msoga yamerudi tena na kuzidi, hiyo hasa ndo sababu hapendeki
 
Back
Top Bottom