PostGE2025 Gerson Msigwa: Vituo 672 vya mafuta vilichomwa moto

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Katika mahojiano yake na Chief Odemba, Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ametaja kuwa vituo 672 vilichomwa moto kufuatia vurugu zilizojitokeza Oktoba 29 na siku nyingine. Amesema idadi hiyo ni ile ile aliyowahi kuitaja Waziri Mkuu, licha ya kuwepo kwa taarifa tofauti tofauti kuhusu idadi ya vituo vya mafuta vilivyoharibiwa.

Msigwa ameongeza kuwa, katika matukio hayo, kuna mmiliki mmoja ambaye takribani vituo vyake 38 vya mafuta vilichomwa moto.

Pia Soma: Vituo vya Mafuta kuchomwa; Tuamini takwimu za Serikali dhalimu (vituo 672), au Wamiliki wa Vituo (41)?
 
Hivi sheria ya takwimu ni kwa raia tu au hadi kwa viongozi? Chama cha wamiliki wa petrol station walisema ni 41 pekee zilichomwa au kuharibiwa sasa hizo 600+ zimetoka wapi? Nchi nzima ina sheli 800+ je ina maana 90% ya sheli zilichomwa?

Sheria ya takwimu ifuate mkondo wake
 
Gerson Msigwa ametaja kuwa vituo 672 vilichomwa moto kufuatia vurugu zilizojitokeza Oktoba 29

Msigwa, ni raia wangapi waliuawa? Lini Tanzania tulianza kuabudu mali kiasi hichi?
 
Watu wanataka kujua idadi ya watu waliokufa, sio idadi ya mali zilizoteketezwa. Maisha ya watu yana thamani kubwa kuliko mali
 
Katika mahojiano yake na Chief Odemba, Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ametaja kuwa vituo 672 vilichomwa moto kufuatia vurugu zilizojitokeza Oktoba 29 na siku nyingine. Amesema idadi hiyo ni ile ile aliyowahi kuitaja Waziri Mkuu, licha ya kuwepo kwa taarifa tofauti tofauti kuhusu idadi ya vituo vya mafuta vilivyoharibiwa.

Msigwa ameongeza kuwa, katika matukio hayo, kuna mmiliki mmoja ambaye takribani vituo vyake 38 vya mafuta vilichomwa moto.

Pia Soma: Vituo vya Mafuta kuchomwa; Tuamini takwimu za Serikali dhalimu (vituo 672), au Wamiliki wa Vituo (41)?
Tuna serikali yenye viongozi waongo sana vitu 600 vichomwe moto watu wangekuwa wanaangaika kupata mafuta now..!
 
Takwimu za mali zilizoharibiwa wanazo ila takwimu ya vifo vya binadamu hawana.... Alafu wanapenda sana ionekane kwamba idadi ya mali zilizoharibiwa ni kubwa sana ila idadi ya vifo vya binadamu ni ndogo sana na ikiwezekana wanapenda ionekane kwamba hakuna mtu yoyote aliyefariki.
 
Hivi sheria ya takwimu ni kwa raia tu au hadi kwa viongozi? Chama cha wamiliki wa petrol station walisema ni 41 pekee zilichomwa au kuharibiwa sasa hizo 600+ zimetoka wapi? Nchi nzima ina sheli 800+ je ina maana 90% ya sheli zilichomwa?

Sheria ya takwimu ifuate mkondo wake
Waongo hawa
Ridhiwani alisema vituo 90 vya Lake Oil, Lake Oil wao wakasema vituo 39
Huyu leo ana idadi yake
Mwigulu naye ana yake
 
Katika mahojiano yake na Chief Odemba, Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ametaja kuwa vituo 672 vilichomwa moto kufuatia vurugu zilizojitokeza Oktoba 29 na siku nyingine. Amesema idadi hiyo ni ile ile aliyowahi kuitaja Waziri Mkuu, licha ya kuwepo kwa taarifa tofauti tofauti kuhusu idadi ya vituo vya mafuta vilivyoharibiwa.

Msigwa ameongeza kuwa, katika matukio hayo, kuna mmiliki mmoja ambaye takribani vituo vyake 38 vya mafuta vilichomwa moto.

Pia Soma: Vituo vya Mafuta kuchomwa; Tuamini takwimu za Serikali dhalimu (vituo 672), au Wamiliki wa Vituo (41)?
Yaani wanachojua ni kusema uongo,mbona hasemi idadi ya watu waliokufa
 
Viko nchi gani hivyo tanganyika hii?

Tuchome vyote ili wapate idadi nzuri.
 
Back
Top Bottom