Generali Ojukwu Ni Kwanini?


Mkandara kwa nini Biafra walikuwa wakipinga utawala wa wanajeshi Waislam?

Na yale mauaji ya watu milioni 2 yalisababishwa na nini?
 
Last edited by a moderator:

Well said Jasusi, na mimi hapo penye red ndio ninajiuliza zaidi. Je toka Mwalimu aondoke walikua hawajashtuka ndio wameshtuka sasa au Mwalimu anafanywa a scapegoat?
 
Mkandara kwa nini Biafra walikuwa wakipinga utawala wa wanajeshi Waislam?

Na yale mauaji ya watu milioni 2 yalisababishwa na nini?

ritz,

..zilitumika mbinu za kikatili sana kuzima maasi hayo ikiwemo kuwa-starve wananchi wa Biafra.

..kwa kweli ingekuwa ni zama hizi nadhani Gowon angenyakuliwa na Mzee Ocampo na kupelekwa kwenye mahakama ya ICC.
 
Mkandara kwa nini Biafra walikuwa wakipinga utawala wa wanajeshi Waislam?

Na yale mauaji ya watu milioni 2 yalisababishwa na nini?
Ritz1
Unakosea unapoingiza Uislamu kwenye kisa hiki cha Nigeria na Biafra. Ni kweli wote Gowon na Ojukwu walishiriki katika kupindua serikali halali ya Tafawa Balewa. Lakini wote Ojukwu na Gowon hawakuwa waislamu. Mapinduzi hayo ya kijeshi yalianzia eneo la Waislamu la Kaduna, January 15, 1966. Wakati huo kiongozi wa jeshi alikuwa ni Muibo Meja Jenerali Aguiyi Ironsi, ambaye yeye alikuwa anaunga mkono serikali ya shirikisho. Lakini baada ya waziri mkuu kuuawa, pamoja na waziri wa fedha na maafisa kadhaa wa kijeshi, alikubali kuongoza nchi. Lakini kukatokea mapinduzi mengine July 28-29 1966 ambapo Ironsi na maafisa wengine wa Kiibo waliuawa. Hapo ndipo uhasama ulipoanza baina ya Waibo na Gowon ambaye alichukua uongozi baada ya mapinduzi ya pili. Kwa hiyo unafanya kosa kubwa kuhusisha kadhia hiyo ya Nigeria na udini. Ungesema ukabila, ningekubali. Lakini endelea kubukua mabuku.
 
:A S cry: It's a pity kuwa we cannot talk about our situation here -- kweli Mwl. Nyerere amefanya makosa sana lakini pia amekua na busara sana in the sense that he got rid of Ukabila ambae inatesa sana wenzetu wa Kenya na wa Ganda. Lakini kwa maendeleo kweli amkill kabisa laiti akiacha wale wazungu kutuendeleza at least we would have been very far and the best country all over Africa. Moreover, Mwl. thought tukiweza wenyewe lakini ulafi, uchi ya madaraka n.k. ndio imetufikisha nchi yetu hapo tulipo. I think we should concentrate on our country problems kuliko kuzugumza mambo ya Nigeria. Au baba anatupa adisi ya Alfa Ulela ulela ???? Ongea zako.
 
Mkandara kwa nini Biafra walikuwa wakipinga utawala wa wanajeshi Waislam?

Na yale mauaji ya watu milioni 2 yalisababishwa na nini?
Kwasababu ni masultan, na hawakutaka utawala wa kisultan, same as waliofanya mapinduzi ya Zanzibar, tatizo si uislam, ni usultan.

Sasa nyie misukule ndo hamjui utofauti,mnaenda kichwa kichwa tu mkiimbishwa kama kasuku, poor you!Pole sana.
 
Hayo ni maneno ya kujifariji angekuwa anapendwa angekimbilia Ivory Coast?
Wakumshukuru ni Rais wa Nigeria kipindi hicho Shehu Usman Shagari, kumsamehe.
ritz, asingemsamehe, nchi ingeingia matatani, alikuwa na influence, especialy politicaly.Na ushahidi ni kabla na hata baada ya kufa.
 
Kumbe Wlly wewe una majibu yako unayoyajua umekuja humu kutuchanganya tu mbona kila unachoambiwa hutaki? Umeambiwa reja vitabu umekataa umepewa taarifa ya aliyekuwepo siku Mwalimu alivyotoa uamuzi wa kuiunga mkono Biafra huku akijilaumu bado unapinga tu sasa unataka kwenda polisi au unataka jibu gani litakalofurahisha mtima wako?
 
Ni kwasababu ya visirani tu........visirani vinawafanya watu washindwe kufikiri.......na hata kuzuia ability ya kufikiri.......it is pathetic..........

- ha! ha! ha! yaani hoja zingine bwana, sasa visirani na pathetic hapa ni nani hasa? ha! ha! ha!

William.
 
Well said Jasusi, na mimi hapo penye red ndio ninajiuliza zaidi. Je toka Mwalimu aondoke walikua hawajashtuka ndio wameshtuka sasa au Mwalimu anafanywa a scapegoat?

- Angeanza na kuongela hilo lijumba la Balali kwanza ndio aseme mengine ya binafsi za watu, kutesa ni kwa zamu zamu yao iliiisha sasa ni ya wengine ndio maisha!!!

William.
 
- ha! ha! ha! yaani hoja zingine bwana, sasa visirani na pathetic hapa ni nani hasa? ha! ha! ha!

William.

Ulishindwa kujenga hoja na kutia huruma kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa EAC.........sasa unaleta visirani na vioja.........haitakusaidia........hata kidogo.......
 
Mkuu ritz naona umezama sana kuhusu historia ya Nigeria! Unawajua mageneral wote waliokuwa wakitamba wakati huo
 
Last edited by a moderator:
Kwasababu ni masultan, na hawakutaka utawala wa kisultan, same as waliofanya mapinduzi ya Zanzibar, tatizo si uislam, ni usultan.

Sasa nyie misukule ndo hamjui utofauti,mnaenda kichwa kichwa tu mkiimbishwa kama kasuku, poor you!Pole sana.

jmushi1.

Kabla ya ukoloni Nigeria ilikuwa na falme mbalimbali Kaskazini ilikuwa chini sultani za kiislam Kano na Sokoto...Kusini ilikuwa na falme za Benin, Ife na Oyo.

Naimani wewe unapenda kujua na kufahamu jaribu kuangalia historia ya Nigeria kwenye mjimbo yao Kebbi, Niger, Kaduna, Yobe, Borno, Zamfara, Kastina, Bauchi, Kano, kwa nini wanatumia Sharia.

Labda nikuulize mwaka 1966 sehemu ya jeshi la Nigeria walifanya uasi na wakamuua Waziri Mkuu Abubakar Tafawa Balewa, aliyekuwa na asili ya Kaskazini, kwa nini walifanya hivyo?
 
Mkuu ritz narudia tena, tatizo halikuwa uislam, bali usultan, waislam wengine mnaunganishia tu, lakini usultan si uislam, naomba kusahihishwa.

Sasa kama hayo majimbo yanatumia sharia ndo waibo wakusini wauwawe?Ama ndo Naijeria nzima watumie sharia? Hiyo ya 1966 lazima walikuwa waki "defend themselves" kutokana na mauwaji hayo ya serikali ya kinyama ya masultan.
 
Ulishindwa kujenga hoja na kutia huruma kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa EAC.........sasa unaleta visirani na vioja.........haitakusaidia........hata kidogo.......

- Fungua thread ya EAC hapa ni ya Biafra! ha! ha! ha! ha! kinyonga wewe! ha! ha! ha!, ndio unasema unakuaj bongo uje nikutembeze kwenye viwanja! ha! ha! ha! ha!

William.
 
Mkandara kwa nini Biafra walikuwa wakipinga utawala wa wanajeshi Waislam?

Na yale mauaji ya watu milioni 2 yalisababishwa na nini?
@ritz, kwanza nieseme kweli sikuelewi kabisa hapa. Lakini nadhani unachozungumzia ni mfululizo wa vita baina ya vyama na ushabiki ulotokana na mgogoro wa uongozi ndani ya chama cha Chief Awolowo - AG baada ya Shangari kuunda muafaka na chama hicho kwa kumteua Akintola kwa Premier wa jimbo lao.

Ikumbukwe tu kwamba anayoyafanya JK ndio historia ya Nigeria hivyo, nimesema sana hapa JF kuhusu wapi tunakwenda lakini inaonyesha watu mmeweka pamba masikioni. Matatizo hayakuanza na wakristu vs waislaam hata kidogo isipokuwa matatizo yalianza kwa wayoruba. SDijui kama unaelewa kwamba uongozi wa kwanza wa nchi hiyo ulikuwa wa mseto baina ya chama cha wa Hausa who happened to be dominant Muslim na kile cha wa Ibo ambao pia dominant ni wakristu kwa sababu NDC hawakupata majority vote ktk uchaguzi mkuu..

Sasa sikuelewi unaposema Biafra walikuwa wakipinga uongozi wa wanajeshi Waislaam wakati aliyekuwa rais wa nchi hiyo toka uhuru alikuwa Azikiwe Myoruba na mkristu maana Balewa alikuwa Prime minister tu. Vijana wa kijeshi waliompindua Azikiwe inasemekana walikuwa Waibo sawa lakini inahusiana nini na Uislaam na Ukiristu ikiwa rais alopinduliwa alikuwa Mkristu?..Na hawa vijana nao wakaja pinduliwa na Generali Johson (mkristu) aliyetaka kuvunja Federation na kuunda Republic... Wewe unazungumzia wakati gani haswa?

Kuhusu Biafra mkuu wangu nimeshasema sana kwamba sababu kubwa ya Biafra kupingana na the rest of Nigeria ni pale walipoona rasilimali zao zote zinakwenda North kujenga kwa Wahausa na Wayoruba ambao walikuwa na mseto wao. Kweli Waibo walikiunga mkono zaidi chama cha NCNC kwa sababu strong hold yake ni jimbo la East na kwao, na kuna ukweli kwamba Waibo wengi ni wakristu lakini haina maana kabisa kwamba kilikuwa chama cha Wakristu, wala sikubaliani na wale wanaodai kwamba NDC kilikuwa chama cha waislaam wakati chama hicho kilikuwa cha Wahausa who happened to be dominant Muslim. Lakini Biafra imetokana na nchi kutokuwa na UMOJA, kutokuwa na rais aliyechaguliwa na wananchi baada ya wanajeshi kupigania madaraka wao kwa wao hadi Gowon kuingia kati..

Sikubaliani na dhana inayotaka mimi niamini kwamba CUF ni chama cha Waislaam na Chadema ni chama cha Wakristu japokuwa kuna ukweli kwamba waumini wengi wa dini hizo wamejiunga na vyama hivyo lakini the main reason ni strong hold za vyama hivi zimekuwa sehemu ambazo wananchi wake wengi ni wa dhehebu mojawapo. Haiwezekani kabisa strong hold ya CUF iwe Zanzibar halafu wanachama wake wawe dominant wakristu au Chadema kuwa Moshi na Arusha tukitegemea Waislaam ndio watakuwa wengi ndani ya chama hicho. Mbona hatujiulizi kwa nini CUF kimejaa Wangazija, Wanyamwezi, Waoman na shihiri ambao ni makabila ya Zanzibar ya leo kama wanavyosema Chadema ni ya wachagga? Lini mchagga akawa Muislaam kama sii kutiliwa ubani na shahada?.

Kwa hiyo Biafra walipigania haki yao, na haya maswala ya kuchimba Gas Mtwara na kuisafirisha Dar inaujenga mji wa Dar na Arusha wakati Mtwara mnaiacha haina kitu itakuja watokea puani mkisema waislaam hivi na vile. Shinyanga mnaiacha na mashimo na toxic ktk mito yao - Yarabi Maghfir mtasema Wakristu wamechachamaa Shinganya. Ipo siku watu tutamalizana vibaya. Kuna Uzuri wa serikali ya Majimbo na kuna ubaya wake lakini binafsi yangu naanza kuamini ni bora madhara yanayoweza kutokana na majimbo kuliko madhara tunayoyajenga ktk mfumo huu wa Chukua Chako Mapema. Je, unajua ya kwamba ile Biafra ilisambaratishwa iligawanywa into 12 states ktk mpango wa divide and rule, hivi sasa chuki imeingia hadi kwa Waibo wenyewe kwa wenyewe kugombania sinia la biriani kwa umaskini walokuwa nao?. That's what I expect kwa Zanzibar baada ya kuvunja Muungano.
 
- Angeanza na kuongela hilo lijumba la Balali kwanza ndio aseme mengine ya binafsi za watu, kutesa ni kwa zamu zamu yao iliiisha sasa ni ya wengine ndio maisha!!!

William.
Na wewe mkuu uko kwenye zamu ya wanaotesa sasa hivi?
 
- Angeanza na kuongela hilo lijumba la Balali kwanza ndio aseme mengine ya binafsi za watu, kutesa ni kwa zamu zamu yao iliiisha sasa ni ya wengine ndio maisha!!!

William.
Na wewe utaendelea kuishi tu outside looking in. Muongo mkubwa wewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…