Gen Z Mnakimbiza sana Magari!

Wa Die Tu
 
Balaa nimeona huko Instagram video an ni mbio tu kama wezi
 
Unaweza kukuta wamepost wanakupita utafikiri ulikubaliana nao kwamba mnashindana.
Ndio kwa sasa league ni wajermani na wajapani,,sasa huku kwa wajapani ni crown kwa sababu sijui ni gari pendwa kwa vijana,,wao wanakuvizia TU shwaaaa harafu wanapost hatakama ulikuwa na safari zako kivyako wanasema mjerumani amekalishwa.
 
Halafu kuna issue siku hizi uko barabarani mdogo mdogo huna Habari wala mood ya kukimbia, linatokea gari huko nyuma linakupita as if mlikuwa mmepanga ligi ya kushindana, akiona Huna interest na mbio basi na yeye anapunguza mnakwenda taratibu, anaweza hata akakusubiri mahali, nahisi hata kurikodi pia wanarikodi ili Tu wajisifu yaani ilimradi Tu mkatoane roho barabarani...
 
😀😀😀 Gen Z wana vituko sana.
 
Adrenaline rush.

Baadae wakishayakanyaga, waulize kwa nini ulikumba mbio hivyo?

Majibu hawana.

Kuna magari automatically ukiwa unaendesha upo speed, lakini chuma bado inaita. Huoni tofauti kabisa.

Kuna siku, nilikuwa naendesha.
Sioni kama nakimbia, baadae nachungulia dashboard na mawani yangu, nipo speed ambayo kwa hakika sikuitarajia.

Ilinibidi nisimame, niheme kwa nguvu. I was worried. Nisingethubutu kufika huko kama my eyes were on the speedometer.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…