- Tunachokijua
- Jenerali Jacob Mkunda ni mkuu wa Majeshi Tanzania. Hivi karibuni kumekuwa na grafiki inasosambazwa ikiwa na nukuu inayodaiwa kuwa ni ya mkuu huyo wa majeshi akieleza kuwa;
"Sitaruhusu utekaji uendelee kwenye nchi yetu"
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa Taarifa hiyo si ya kweli.
Ufuatiliaji kwa kutumia utafutaji wa maneno umebaini kuwa hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo Tanzania na nje ya Tanzania.
Hakuna pia kumbukumbu zozote zinazoonesha kuwa mkuu huyo wa majeshi aliyazungumza hayo hadharani ama kwenye mahojiano ya vyombo vya habari kama inavyoelezwa.
Taarifa ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) inafafanua kuwa:
“Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa taarifa kwa Umma kuwa taarifa zilizosambazwa kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook kwa akaunti iitwayo MJUMBE PLUS sio za ukweli ni Uongo.
“Hivyo umma uzipuuze, hatua kali za kisheria zinachukuliwa dhidi ya yeyote anayesambaza taarifa za uongo zinazolihusu JWTZ.”