Je, Julian Assange ni Shujaa au Msaliti?

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,043
Wakati wa masika miaka 10 iliopita, mwanaume mmoja mwenye miaka 41 kwa jina la Julian Assange akiwa amevalia mavazi ya wafanyakazi wa kusafirisha vifurushi kwa pikipiki, huku akiwa nywele zake kazipaka rangi, kapachika lenzi za kubadili rangi ya mboni za macho, na kuweka kipande cha jiwe kwenye moja ya kiatu alichovaa ili kubadili mwondoko wake kutokana na maumivu aliyokuwa anayapata wakati akitembea.

Julian hakuwa na shaka kuwa kuna makachero wa vikosi vya serikali waliokuwa wanamfuatilia ili kumkamata ili wamsafirishe kwenda Marekani apate kufungwa. Alitembea kuelekea kwenye eneo ulipo ubarozi wa Ecuador, katika eneo la katikati mwa Jiji la London. Ilikuwa ni lazima afanikiwe kuingia katika eneo la ubarozi huo kwa kuwa akifanikiwa kuingia ubarozini, hiyo inamaanisha hatakuwa tena kwenye ardhi ya Uingereza, hivyo Uingereza haiwezi kumkamata. Atakuwa salama. Hii inajulikana kama Hifadhi ya Kisiasa.

Siku hiyo, Julian alifanikiwa kuingia ndani ya ubarozi huo. Na baada ya kuingia kwenye ubarozi huo, Julian hakuwahi kutoka ndani ya ubarozi huo kwa miaka 7.

Kisa hiki kinahusiana na nguvu ya siri na taarifa, ambapo viongozi wa serikali ya Marekani waliita kuwa ni Taasisi inayopinga uwepo wa vita huku ikiishambulia serikali ya marekani na sera yake ya vita nchini Afghanistan.

Serikali ya Marekani inajaribu kumfunga Julian kifungo cha miaka 175 kwa kile alichofanya. Serikali yenye nguvu Zaidi duniani ilihisi haiko salama kutokana na kile Julian alichokuwa akikifanya

Na hiki ndicho kisa cha Julian Assange

Julian Assange ni hacker kutoka Australia ambaye alitumia muda mwingi wa Maisha yake akishambulia mifumo ya kompyuta na kupora taarifa mbalimbali ambazo hazikupaswa kuweka wazi kwa umma. Julian yeye aliamini kwamba umma haunabudi kuona taarifa hizo.

Akiwa na umri wa miaka 35, Julian alitengeneza tovuti ambapo wafichua maovu wa kila aina waliweza kupakia taarifa za siri, ambazo Julian aliweza kuzichapisha kwenye tovuti yake ya kuvujisha taarifa.

Kwa kufanya hivi ambapo wafichua maovu hawakuchapisha taarifa wao moja kwa moja, basi aliwahakikishia usalama wao na kutojulikana, Alidai kwamba hata yeye mwenyewe asingeweza kufahamu vyanzo vya taarifa alizokuwa akichapisha mtandaoni.

Na hiyo ilikuwa mwaka 2006 ambapo alitengeneza tovuti la Wikileaks. Na baada ya muda mchache, akaanza kupokea hati mbalimbali za siri kutoka kwa watu mbalimbali duniani. Yeye alikuwa akichapisha hati hizo mtandaoni kuanzia mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani huko Yemen, hadi ufisadi waw a uuzaji wa mafuta huko Peru, hadi ufisadi mkubwa uliokuwa ukiendlea kwenye falme za Kiarabu, mpaka maandamano ya Tibet huko China.

Kwa sasa kilichokuwa kikifanywa na Wikileaks kinaonekana kuwa jambo la kawaida, lakini kumbuka wakati huu ilikuwa mwaka 2007. Jambo hili lilikuwa geni kabisa. Wikileaks ilikuwa tovuti ambayo kila mwenye taarifa ya siri anaweza changia (open source intelligence website) ikiwa inajitanabaisha kuwa haiko chini ya mamlaka ya serikali yoyote na wala haina ofisi eneo lolote.

Maono ya Julian ilikuwa ni dunia ambayo ina uwazi kamili wa upatikanaji wa taarifa. Hii ikijumuisha kufichua ufisadi, na siri za serikali.

Kwa muda wote huo, Wikileaks haikuchukuliwa wka uzito mkubwa mpaka ilipofika mwaka 2010, na mwaka huo lilitokea jambo lililobadilisha kila kitu.

Katika nchi ya Iraq, kulikuwa na mwanadada mwenye umri wa miaka 22 mwenye jina la Chelse Manning. Huyu alikuwa mchambuzi wa taarifa za kiintelijensia wa Marekani. Mwandada huyu aliogopeshwa na kile alichoona na mambo yaliyokuwa yakiendelea nchini Iraq. Hivyo, aliamua kupakua maelfu ya hati za siri (Zaidi ya hati 90,000) kutoka kwenye kompyuta za vyombo vya usalama na kisha kuzipakia moja kwa moja kwenye tovuti ya Wikileaks.

Baada ya hati hizo kuweka mtandaoni, iligeuka kuwa Habari kubwa sana duniani kwenye kila chombo cha Habari kutoka na taarifa za siri zilizokuwa kwenye hati hizo. Uvujishaji wa hati hizi unachukuliwa kuwa ndio uvujishaji wa siri mkubwa Zaidi kuwahi kutokea kwenye historia ya marekani au dunia nzima.

Kwenye hati hizo kulikuwa na mamia ya siri yanayohusu jinsi vita ya Iraq na Afghanistan ilivyokuwa ikiendelea, intelijensia ya jeshi na mambo ya kidiplomasia ya nchi. Hati hizo zilijaa mambo mengi ya kutisha ambayo dunia haikuyajua.

Kwenye hati hizo umma ulipata kujua kuhusu uvamizi wa siri juu ya raia wa Iraq na kuwaua.

Kuna taarifa za matukio yaliyofanywa na wanajeshi wa Marekani yaliyohusisha mauaji ya familia zisizokuwa na hatia.

Pia kulikuwa na data mbalimbali. Wakati serikali ya Marekani ilikuwa ikidai kuwa haikuwa ikiweka rekodi ya vifo vilivyokuwa vikitokea kwenye vita ya Iraq, lakini hati hizo zilionyesha kuwa sio kweli. Serikali ilikuwa ina rekodi ya idadi ya watu waliokufa kwenye vita hiyo. Na ilionyesha kwamba idadi ya majeruhi na vifo vya raia ilikuwa juu kuliko ambavyo watu wengi walidhani.

Pia kulikuwa na kipande cha video ya siri ambapo inaonyesha helkopta ya Marekani ikishambulia familia ya watu, yani familia wakiwemo Watoto wadogo wakiwa wameongozana na waandishi wa wawili wa Reuters waliokuwa wakitembea kwenye barabara wakiwa wameshikilia kamera zao. Kwenye hiyo video yanasikika mazungumzo baina mwanajeshi aliyekuwa na bunduki kwenye helkopta na kamanda wake ambapo kamanda anamwambia washambulie unasubiri nini. Baada ya kuwashambulia anasema “Come on, let’s shoot. Light em all up.” Na jamaa anaitika “Roger that.” Kisha unaona wakiwamiminia risasi. Halafu jamaa baada ya kuwapiga risasi anasema “Oh yeah, look at those dead bastards.”

Kamanda anaitikia, “Nice. That is their faults in bringing the kids to battle.” Upande mwingine unaitikia, “That’s right.”

Kuna pia maelezo ya tukio ambapo Helkopta aina ya Apache, ilikuwa ikiruka juu ya nyumba ambamo wanajeshi pinzani walikuwa wamejificha na wanaamua kujisalimisha kwa kutoka kwenye nyumba hiyo huku wakiwa wamenyanyua mikono. Lakini helkopta inapewa order ya kuwashambulia kwa madai kwamba hauruhusiwi kujisalimisha mbele ya ndege. Kwahiyo hata ukijisalimisha bado wewe ni target.

Pia kwenye hizo hati kuna Zaidi ya raia 15,000 waliuawa kwenye matukio tofauti ambayo hayakuwa na maelezo ya kueleweka. Pia hati hizi ziliwka wazi mateso na utekaji uliokuwa ukifanya na wanajeshi wa Marekani.

Na haya ni machache kati ya maelfu ya matukio yaliyokuwa kwenye hati hizi.

Pia kulikuwa na hati yenye taarifa kutoka kwenye ubarozi wa Belgium inayoonyesha kwamba serikali ya Marekani ilikuwa ikijaribu kuisukuma Serikali ya Belgium ili ikubali kuchukua baadhi ya wafungwa waliokuwa kwenye gereza la Guantanamo kwa malipo ya kupata upendeleo kutoka Marekani. Yani kwamba Marekani itaisaidia Belgium kuwa mojawapo kati ya nchi zenye ushawishi mkubwa barani Ulaya ikiwa ingekubali kuchukua hao wafungwa.

Jambo la kufurahisha na kustaajabisha baada ya uvujaji wa taarif hizi mwaka 2010/2011, Pentagon ilikasirishwa juu ya jambo hili. Wikileaks sasa ilikuwa ndio Habari ya dunia. Kutoka kuwa chanzo kidogo cha uvujishaji wa taarifa za siri na kuwa mtandao mkubwa ambao ulikuwa ukiogopwa na mataifa makubwa. Julian, naye akawa maarufu sana akiwa anaalikwa kwenye mahojiano, kwenye midahalo.

Watu wengine walimwita kama Mwanahabari mwenye uthubutu, huku wengine wakisema ni msaliti wala hafai kabisa. Viongozi wa serikali ya Marekani walimwita mshenzi, ameichafua serikali yao na kuhatarisha Maisha ya watu. Serikali ya Marekani ilijiona iko vitani dhidi ya Julian.



Kwanini Julian Assange alikimbilia kwenye ubarozi wa Marekani



Mwaka 2012 baada ya kuvuja kwa hati hizo, wakati huo Julian alikuwa akiishi London. Lakini kulikwa na hatari ya kupelekwa Sweden ili kukabiliana na uchunguzi wa wa madai kwamba alimbaka mwadada nchini humo. Japokuwa uchunguzi huo wa Sweden kisheria haukuwa na uhusiano wa namna yoyote na uvujishaji wa hati za Marekani, Julian alihisi kwamba serikali za Uingereza na Sweden wanashirikiana na Marekani katika kujaribu kumpeleka Marekani ili akashitakiwe.

Sasa badala ya kwenda Sweden na kushiriki katika uchunguzi, Julian aliamua kukimbilia kwenye ubarozi wa Equador na kuomba hifadhi ya kisiasa. Serikali ya Uingereza haikuwa tena na uwezo wa kumkamata maana kiuhalisia haina mamlaka ya kuingia kwenye ubarozi wan chi nyingine.

Hivyo, waliweka askari nje ya ubarozi wa Uingereza. Na idadi ya askari hao nje ya ubarozi ilikuwa ni kubwa mno kiasi kwamba watu walijua kabisa hii ni Zaidi ya Julian kutoroka uchunguzi wa kesi ya ubakaji. Maana kulikuwa na askari Zaidi ya 50.

Kwenye hati za kiuchunguzi halikuonekana kuwa jambo kubwa, kwani serikali ya Uingereza ilitaka kumkamata Julian na kumpeleka Sweden akashiriki kwenye uchunguzi wa tuhuma zake za kumbaka mwanadada. Lakini kiuhalisia mambo yalikuwa tofauti. Kwa idadi ya polisi na pesa waliokuwa wanatumia, bila shaka halikuwa jambo dogo hapo.

Marekani ilikwua ikimhitaji Julian ili imwadhibu kwa kile alichofanya, na bila shaka Uingereza ilikuwa katika harakati za kuisadia Marekani kutimiza hilo.

Julian anaendelea kuishi pale ubarozini London, wiki zinakuwa miezi, miezi inakuwa miaka. Kila mara alikuwa akitokea kwenye ubaraza ghorofani na kutoa hotuba kwa mashabiki zake waliokuwa wakikaa nje ya ubarozi.

Akiwa hapo ubarozini, Julian aliendelea kuendesha Wikileaks. Aliendelea kuchapisha hati mbalimbali za siri. Akiwa bado ubarozi, ndipo alipoweka wazi kuwa hampendi Bibi Hillary Clinton. Na hapo ndipo alipanga mpango wa kuharibu kampeni zake za kinyanganyiro cha kugombea kuwa raisi wa Marekani kwa kuchapisha barua pepe zake mafungo kwa mafungo wakati wa kampeni. Barua pepe hizi zilikuwa zimeibwa kwenye chama cha Democratic, na kutoka kwa Meneja Kampendi wa Hillary, John Podesta.

Kila siku WikiLeaks ilivujisha barua pepe kadhaa kuanzia Oktoba 2016, mwezi mmoja kabla ya upigaji kura.

Ushahidi uliibuka ulionyesha kwamba WikiLeaks ilipata barua pepe hizi kwa kujua au kutojua kutoka kwa kachero wa serika ya Urusi, ambaye kama alivyo Julian, naye alikuwa anataka kuharibu kampeni za Hillary.

Barua pepe hizi zilimsaidia sana Trump hadi Trump kunukiliwa akisema kuwa anampenda Julian na WikiLeaks. Jambo hili pia lilifanya wakosoaji wa Trump kusema Trump mwenyewe ni adui wa Marekani maana anaunga mkono Julian na tovuti yake ya WikiLeaks.

Trump anshinda uchaguzi anakuwa raisi na haweki mkazo wa kumkamata.

Mwaka 2017, Julian akiwa bado ubarozini anadondosha bomu jipya, na mara hii anachapisha hati za CIA. Hati hizi ziliweka wazi mpango wa vita ya kimtandao wa CIA. Uvujishaji wa hati hizi ulifanya mipango na vitendea kazi vyote vya CIA kuwa havina maana tena.

Sasa Trump ambaye alikuwa akiipenda WikiLeaks, sasa na yeye alikuwa kaksirishwa na Julian na kumchkia sana.

Kwenye mahojiano alidai kwamba haifahamu WikiLeaks wala Julian. Vyombo vya ulinzi vya Marekani viliweka wazi kuwa WikiLeaks ni hatari na lazima iangushwe.

Mwaka 2019, Julian akiwa bado ubarozini, ashalikoroga na kuudhi karibu kila serikali kwa sababu moja au nyingine. Muda huu serikali ya Trump inaanza kuweka mkazo wa jinsi ya kumnasa Julian. Wanaanza kutengeneza kesi juu yake maana lengo sio kumkamata tu, bali lengo ni kumwadhibu pia.

Lakini pia Julian naye amechoka sana Maisha ya kubaki amefungiwa ubarozini. Anaanza kuwa na mashaka na wenyeji wake. Pia barozi wa Equador naye ameanza kumchoka. Anakuwa mchafu, anacheza mpira kwenye korido ya ubarozi.

Na pia wakati huo huo raisi mpya wa Equador yeye hana huruma kwa Julian kwasababu WikiLeaks pia ilihusika katika kuvujisha hati Fulani zilizomchafua. Raisi huyo anadai Julian ni hacker mshenzi ambaye lengo lake ni kutikisa serikali za nchi mbalimbali. Hivyo, wanaamua kumfukuza ubarozini.

Baada ya kutolewa nje anakamatwa na polisi wa Uingereza mara moja.

Kumbuka kwenye hati inaonyesha kuwa serikali ya Uingereza inamhitaji kwa tuhuma za ubakaji aliotenda Sweden mwaka 2012. Hakuna tena uchunguzi huu washaachana nao lakini bado serikali ya Uingereza inamshikilia na kumweka gerezani kwakuwa Serikali ya Marekani ilikuwa imeomba Julian apelekwe Marekani ili akashitakiwe.

Serikali ya Uingereza ilisikiliza na kufanyia tathmini ombi la Marekani, lakini kwasasa julian anabaki gerezani mpaka uamuzi utakapotolewa kama asafirishwe kwenda Marekani au la.

Leo Julian amekaa hap ana inasemekana hayuko sawa. AMechunguzwa na madaktari na wawakilishi wa Umoja wa mataifa ili kubaini kama amepitia mateso. Na wote wamefikia hitimiso kwamba Julian hayuko sawa kiakili kwa kile anachopitia na hii inahatarisha afya yake. Ila serikali ya Uingereza imepinga hili. Wanasema yuko vizuri kabisa hana shida yoyote.

Je, Kosa la Julian Marekani ni lipi?

Jambo ambalo Idara ya Haki ya Marekani imetilia mkazo sana ni matokeo yam waka 2010. Huu ndio mwaka Julian alipopokea maelfu ya hati za siri, kutoka kwa Chelse Manning ambapo hapo kabla alikuwa akijulikana kama Bradley Manning kabla ya kubadili jina na kuwa Chelse Manning baada ya kubadili jinsia yake kutoka kiume kuwa wa kike. Maaning alikuwa na ruhusa ya kiusalama, alivunja kanuni za ruhusa hiyo, kwa kuiba na kuvujisha hati hizo na kupata adhabu ya kifungo cha miaka saba. Ilikuwa afungwe miaka 35 kama utawala wa Obama usingempatia msamaha.

Hivyo wanamashitaka wa marekani wameweka mkazo kwenye hati hizi za mwaka 2010. Wanadai kwamba Zaidi ya hati laki 7 zilivujishwa kwa umma.

Na kwa hili, wana mashitaka 18 juu ya Julian. Ikiwa atakutwa na hatia, huenda kafungwa jumla ya miaka 175.

Mashitaka yote haya 18, yanaweza kuwekwa katika mafungu 3 tu.

  • Hacking
  • Kusaidia
  • Uchapishaji

Kosa la kwanza la Hacking hili halitishi sana maana hata akikutwa na hatia atafungwa miaka 5 tu. Wanadai kwamba Julian alishirikiana na Manning, kupata nenosiri la kompyuta za serikali ili Mannign aweze kuiba hati hizo pasipo wizi huo kugundulika. Lakini mwisho walishindwa, na nenosiri hawakulipata. Lakini wanadai walijaribu na hivyo ana shitaka la kujibu juu ya kupanga jama za kutenda wizi wa taarifa kwenye kompyuta.

Mashitaka mengine 17 yako ndani ya Kuaidia na kuchapisha. Wanadai kuwa Julian alivunja Sheria ya Ujasusi (Espionage Act). Hii sheria ilipirishwa mwaka1977 wakati wa vita ya kwanza ya dunia. Lakini hii sheria ililenga kuwaadhibu watu ambao walikuwa wameajiriwa na serikali au jeshi la Marekani na walikuwa na ufahamu juu ya siri za serikali nao wakaenda kuzivujisha au kuuza. Hii inamhusu chelse Manning lakini sio Julian. Mannign yeye alikuwa mwanajeshi na Mmarekani, alivujisha taarifa za serikali hivyo alivunja sheria hii.

Julian yeye sio raia, wala mwajiriwa wa serikali au jeshi la Marekani. Yeye ni mwanaharakati raia wa Australia.

Hivyo, wanatumia sheria hii na kusema kwamba ni kweli Manning ndiye aliyevunja sheria moja kwa moja, lakini katika sheria za Marekani kuna kipengele kinachosema kwamba, ukimsaidia mtu kutenda kosa, basi na wewe utaadhibiwa, kama mtu aliyetenda kosa.



Na kundi la tatu wanadai kwamba kitendo cha julian kuwa na taarifa ambazo hakupaswa kuwa nazo kuhusu vita ya Iraq na Afghanistan na Idara za nchi, na hati nyingine na kuzichapisha mtandaoni wka ajili ya umma ni kosa. Kwahiyo hapa kosa lake ni kuchapisha hati ambazo hakupaswa kuwa nazo.

 
Jamaa ni bonge la shujaa, alitoa documents za mauwaji waliokua wakifanya majeshi ya marekani nchini Afghanistan, kuna documents moja miongoni mwa hizo ikionyesha raia wa kawaida kama 60 wako sokoni wakishambuliwa kwa risasi na wote kuuwawa bila ya hatia, Juzi Putin aliongea kuwa Assange alifanya kosa kubwa sana kuomba ukimbizi ktk balozi za west ambao hawaaminiki, angefanya kama Snowden ingelimsaidia, Kitu cha kushangaza wanajiita nchi za democrasia lakini hawataki kabisa kuambiwa ukweli magaidi wakubwa
 
Hero, hero according to what?.
In wich framework he should be called hero?
To take someone's privacies and spreed them out is an heronic act?.
Don't you think that government should be accountable for the mistakes? Maana alichoweka wazi ni mambo ambayo serikali ilikuwa inaficha kwenye vita
 
Sheria za Marekani ziko wazi, documents zozote ambazo ziko classified hazipaswi kuvujwa. Adhabu yake ni kinyongo ama kifungo cha maisha.
 
Sheria za Marekani ziko wazi, documents zozote ambazo ziko classified hazipaswi kuvujwa. Adhabu yake ni kinyongo ama kifungo cha maisha.
Huhisi kwamba maovu ya serikali kuna muda yanabidi kuwekwa wazi. Mfano kama hayo mauaji ya halaiki yaliyokuwa yakifanywa na jeshi dhidi ya raia? Serikali haiwezi kuweka maovu yake hadharani, mpaka mtu ayavujishe. Hizo siri za kiharifu zinafichwa kwa maslahi ya nani unadhani mkuu?
 
Hero, hero according to what?.
In wich framework he should be called hero?
To take someone's privacies and spreed them out is an heronic act?.
Kujiweka hatarini Kwa kuchapisha taarifa za Siri za war crimes za taifa kama Marekani ni ushujaa!Huoni mpaka Sasa anavyoteseka?Angekuwa kinyume Cha hero basi angekuwa coward,maana yake angekaa kimya huku akiwa na taarifa za mauaji ya watu wasio na hatia zaidi ya 15,000!
 
Nafaka Asante Kwa makala hii!Leo nimebahatika kusikiliza kipindi Cha hard talk BBC,mgeni alikuwa Stella Morris,mke wa Julian Assenga!
Aiseee,nimesisimka sana,kumbe hata Julian alipokuwa chini ya ubalozi wa Ecuador,CIA waliweka Camera za Siri na microphone katika eneo ambalo Alikuwa akikaa Julian!Kumbe hata akiwa faragha na Stella basi CIA walikuwa wakisikia!Mbaya zaidi walisikia Hadi mikutano yake na wanasheria wake ndani ya ubalozi!
Interview hiyo sio ya kukosa aiseee!
Halafu kumbe jamaa amezaa watoto wawili na Stella ambaye ni raia wa uingereza na watoto wake ni wamezaliwa uingereza!
Je,Uingereza itachukua hatua gani?

Binti amesema anaamini uamuzi wa kumpeleka USA ni kama death sentence!
 
Kujiweka hatarini Kwa kuchapisha taarifa za Siri za war crimes za taifa kama Marekani ni ushujaa!Huoni mpaka Sasa anavyoteseka?Angekuwa kinyume Cha hero basi angekuwa coward,maana yake angekaa kimya huku akiwa na taarifa za mauaji ya watu wasio na hatia zaidi ya 15,000!
Kuingilia preives ya mtu na kuweka mambo yake hadharani si jambo la kishujaa,huo ni uharifu kama uharifu mwingine.
 
Inategemea ni jambo gani!
Tafuta basi hata interview aliyoifanya mke wake Leo kwenye Hard talk ya BBC,huenda ukaongeza maarifa kuliko hivyo ulivyo mtupu!

Hiyo interview haifanyi alichokifanya kiwe halali.
Na kingine:, katika hiyo interview imekujenga nini hata ujione sio empty headed person?.
 
Jamaa ni bonge la shujaa, alitoa documents za mauwaji waliokua wakifanya majeshi ya marekani nchini Afghanistan, kuna documents moja miongoni mwa hizo ikionyesha raia wa kawaida kama 60 wako sokoni wakishambuliwa kwa risasi na wote kuuwawa bila ya hatia, Juzi Putin aliongea kuwa Assange alifanya kosa kubwa sana kuomba ukimbizi ktk balozi za west ambao hawaaminiki, angefanya kama Snowden ingelimsaidia, Kitu cha kushangaza wanajiita nchi za democrasia lakini hawataki kabisa kuambiwa ukweli magaidi wakubwa
Wao wenyewe Ndio waaribifu wa demokrasia. Anaogopa kutoka madarakani kuofia kuuwawa
 
Jamaa unaonekana una shida mahala!JF ni sehemu tu ya kubadilishana mawazo na kupeana maarifa Mapya!
Kutoka kuniita Mtupu hadi kunikumbusha kuwa Jf ni sehemu ya kubadilishana mawazo🙁. sawa, ila mimi ndiye nilipaswa nikukumbushe la Jf kuwa sehemu ya kubadilishana mawazo ila sikufanya hivyo.
Mimi nilitaka kujua nini hasa kimekufanya ujisikie uko full maarifa baada ya kusikiliza hiyo interview.
 
Hapo kwenye mwanadada Chelsea Manning umekosea kidogo. Huyo alikuwa ni mwanaume mwanajeshi aliyezaliwa Kwa jina la Bradley Edward Manning. Jina la Chelsea Elizabeth Manning alilipata baada ya kubadili jinsia na kuwa mdada (gender reassignment), na hili amelifanya baada ya kuwekwa lupango kwa hilo kosa ulilotaja.
 
Back
Top Bottom